Hawa wanamuunga mkono Lowassa ktk CCM. Nani mwingine unamjua?

Ha! Ha! tunajua agizo ni kumsema Rais kwa mafumbo mnaogopa nini kama mna ukweli?

kuna watu mnatia kichefuchefu kwa unafiki...yaani haujajiweka tofauti na akili za akina Ridhwan! kusema EL mwizi na kumwacha Kikwete ni kutofikirisha ubongo wako kwa mapana, na kubaka hisia zako wazi wazi! CCM nyie wote wezi tu...hapa unajikomba kwa JK unapata nini na faida gani unajua mwenyewe!

Tumeamka hatutaki kundi lolote nyie wote wezi tu na Lowassa amevuna sawa sawa kuwa kwenye kundi la majambazi......kuwa umseme vibaya EL, na kumlinda JK , na wenzenu wengi ni kutaka kutupumbaza! I know your goals is to be one of the great thief through CCM, hii ni targets ya nyie wote watoto wa hao vibopa! Kaa kimya itakusaidia hapa unajianika na watu wanakuchora mkuu.....mlinyimana nini na Lowassa ,mlikorofishana wapi na kuweka magubu...inajulikana! pia ni adui wa Nyerere kwa sababu unamsaidia mzee ule uchungu wake wa kuitwa mhuni

Kaa kimya.....dunia inajua na sasa tumetambua na slogan hii iko very active na utaona mapinduzi yanayoenda kutokea...slogan ni kuwa CCM wote wezi!!! ukiwamo mkuu...I mean wewe mwizi!

x-mass isiwe njema kwako tumewachoka!
 
Juma Kidogo, kama ni tuhuma huwa zinathibitishwa, Lowassa hajamtuhumu jambo lolote JK bali tuu ame disclose asilimia 01% ya unknown facts kuhusu Richmond. Ile asilimia 99 iliyobakia ndio karata yake ya utakaso na ataitumia wakati muafaka!.

Alichosema Lowassa ndio ukweli wa mambo yenyewe na ukimya wa upande wa pili ndio uthibitisho kuwa hana la kujibu ambapo kimahakama silence means addmission of guilt!.

Naomba kusisitiza kwenye majibu yangu sijataja mtu sasa mshishangae watu wao wakija na kutaja taja majina humu!.

Kwanini unaamini kuwa alichosema Lowassa ndiyo ukweli wenyewe?
 
Katika harakati zake za kujinasua katikaa kufukuzwa uanachama wa CCM na vikao vya chama, EL ana watu ambao wapo tayari kufa nae.

Hawa ni:

Mbunge wa Kigoma Mjini mhe. Peter Serukamba,
Januari Makamba,
Karamagi Nazir,
Sofia Simba,
Kusila (m/kiti wa CCM Dom),
John Guninita (m/kiti Dar)

Ongeza orodha, wewe unamjua nani???

Nawasilisha

Nape Nnauye
Wilson mukama
Jakaya kikwete
Anna makinda
Andrew Chenge
 
Mimi naamini CCM wote wezi!! naamini zaidi tena siku ya leo ya X-MASS!
Waberoya, naomba kutofatiana na wewe, sio kweli kuwa CCM wote ni wezi!. Naomba tuwe more realistic bila kuendekeza hisia!
Japo ni kweli CCM wengi ni wezi, ila sio wote!. Ndani ya CCM bado kuna wasafi wachache, wengine nawajua ila usiombe niwataje!

Kuna wana CCM wanaishi kwenye object poverty, simply ni destitute!. They have nothing at all, hata kama labda wanamawazo ya kiiwizi but have nothing at all hata hicho cha kuiba hakuna!. Watu kama hawa kuwaita wezi, sio kuwatendea haki!.

Kuna viongozi wakubwa wa CCM, walikuwa na kila opportunities za kuiba na kujilimbikizia mali na kugeuka mabilionea!. Unaamini kuna viongozi wakuu waliokuwa wakiishi maeneo ya Oysterbay, walikuwa wajijifugia tu mbuzi /kuku kama miradi yao?. Unaweza kuamini kiongozi mkuu anaishi aneo la Sea View by the beach, anaishi na ng'ombe eneo hilo!. Sasa watu kama hawa, kuwaita wezi, kiukweli sio kuwatendea haki!.

Nimefika kwa baadhi yao ambao walikuwa safi, walilitumikia taifa hili kwa uadilifu mkubwa mpaka wakastaafu kwa heshima.Lakini baada ya kustaafu waligeuka masikini wa kutupwa na kuonewa huruma, sasa watu kama hawa, unapoaita wezi, sio kuwatendea haki!

Waberoya, wakati mwingine, tuwe wakweli, japo sio lazima sana kuwa wakweli kwenye keyboard ila tuwe wakweli ndani ya nafsi zetu!.
 
Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na
Serikali. Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:
"Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma'. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali".

Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.
Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma". Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!

Watanzania wote, leo nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.

Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam". Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.

Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?"

by:
Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere
Simu: 0754 372141

NOTE:Wapambe wa lowassa mtusaidie kumuuliza lowassa kwa nini alikacha kikao cha msasani?? na Lowassa akipitishwa na ccm kugombea urais(kitu ambacho ni ndoto) kwa gharama zangu Huu waraka nimejitolea kuutembeza kila kijiji cha nchi hii na kuuonyesha kama zile sinema za yomba yomba zilivyokuwa zikionyeshwa bure kwenye viwanja vya wzi vijijini na kugawa kopi za kutosha kila kijiji,mjini ntawaachia chadema washughulike nae.....nyie endeleeni kula hela zake na kumdanganya hapa!!!!
 
Pasco argument yako ya Rais atoke North ni debatable, lakini kwamba lazima awe Lowassa ni an insult kwa sisi wananchi wengi wa Tanzania tunaomjua vizuri the man, Mwalimu alikuwa anamfananisha na Mcolombia Ochoa a Drug dealer aliyekuwa ananunua ardhi kwa hela chafu!
 
Kwanini unaamini kuwa alichosema Lowassa ndiyo ukweli wenyewe?
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza heri ya X-mass! na wengine wote pia heri zenu za x-mass, nilidhamiria leo iwe siku ya kuzungumzia yaliyo mema tuu na furaha hizi na zile.

Uaminiji wangu wa alichokisema Lowassa ni ndiyo ukweli wenyewe kwa sababu, he is genuine, genuinity unaiona machoni, usoni na kusikia moyoni. Naamini toka moyoni mwangu, Lowassa ni mkweli, ila pia hao mnaowadhania ndio wakweli, hao ndio waongo.

Mzee Mwanakijiji, kama utakumbuka katika ile thread yako ya "Wapiganaji walioko CCM, wanapigania nini" nilitoa maoni yangu kuhusu hao mnaowategemea kama ni wapiganaji wa ufisadi, wengine wao ndio mafisadi wenyewe!. Na hawa mnaowaona kama mafisadi kumbe sii lolote sii chochote!.

Hata kule kwenye ile thread ya ufisadi wa Mzee wa Vijisenti, nilisema, yuko right, hizo fedha alizokutwa nazo, nyinyi mnaziana kama ni nyingi!, hivyo ni vijisenti tuu, ukilinganisha na fedha za wengine ambako ziko safe kule Credit Sussie!, sasa kama hizo zake ambazo ni vijisenti tuu mnapiga kelele, jee ngeziona hizo acconts za wenyewe?! si mngezimia!.

Mzee Mwanakijiji, politics is a game, kwa hili game kwa nchini kwetu ambalo tumetawaliwa na chama kimoja kwa miaka 50, determinant ya mabadiliko ya kweli kwa nchi yetu, ni mgombea wa CCM 2015!, kama na wewe unaemgombea wako in mind ambaye unaamini he can make a best president for this country, ili huyo mgombea wako asinde, lazima ujue atashindana na nani as a pace maker wake!.

Nawashauri wapenda mabadiliko ya kweli Tanzania, lets rally behind Lowassa ndie awe mgombea wa CCM 2015, vinginevyo!, akisimamishwa mtu kama Magufuli inajua nini kitafuatia!

Lawassa for CCM 2015!.
 
Mkuu Romantic eventually Mwalimu alikutana naye Msasani alienda kwa kumtumia Mbunge wa NCCR wakati ule Makongoro, Mwalimu akamuonyesha document za ununuzi wa magari ya Wabunge ambayo Lowassa alisimamia kama waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu wizi mtupu akaishia kuondoka kimya kimya!
 
mkuu romantic eventually mwalimu alikutana naye msasani alienda kwa kumtumia mbunge wa nccr wakati ule makongoro, mwalimu akamuonyesha document za ununuzi wa magari ya wabunge ambayo lowassa alisimamia kama waziri wa ofisi ya waziri mkuu wizi mtupu akaishia kuondoka kimya kimya!

alaa sasa nimeelewa kwa nini makongoro anampinga lowassa....kumbe anajua mengi kumhusu sio!
 
Makongoro was right there wakati Mwalimu anamshukia Lowassa na kumuita Ochoa, ndio maana nafsi yake inamsuta kupokea hela chafu kama Wenyekiti wenziwe kina Mgeja na Guninita!
 
Ndigu yangu Jumakidogo, utaambiwa umepokea pesa!. Kuna watu wanaamini kila mtetezi wa EL, kapewa pesa!.

Mbona walisha semda nimepewa pesa, sasa sijui na sisi tuseme wao wamepewa pesa na wapinzani wa EL Kisiasa. Ndio maana nikasema bora kila mtu abaki na imani yake.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza heri ya X-mass! na wengine wote pia heri zenu za x-mass, nilidhamiria leo iwe siku ya kuzungumzia yaliyo mema tuu na furaha hizi na zile.

Heri ya Krismasi na kwa Pasco na vyote vilivyo vyako.

Uaminiji wangu wa alichokisema Lowassa ni ndiyo ukweli wenyewe kwa sababu, he is genuine, genuinity unaiona machoni, usoni na kusikia moyoni. Naamini toka moyoni mwangu, Lowassa ni mkweli

Umejibu vizuri. Ulivyosema kuwa alichosema Lowassa ndio ukweli wenyewe haitokani na kujua kuwa kilichosemwa ni kweli. Unaamini ni kweli kwa sababu Lowassa kasema si kwa sababu alichosema ni kweli. Kwamba, akisema Lowassa huhitaji kuhoji kama kina ukweli bali unaamini kwa sababu yeye kasema. Na ni kutokana na hilo ndio unaamini kuwa anafaa kuwa Rais wetu. Nilimjibu Waberoya kwenye ila mada nyingine kuwa facts zinasimama zenyewe na mtu yeyote anaweza kuzipima na kuona kuwa ni kweli. Nikikuambia kuwa "njia ile ina miiba" nitakuwa nasema kweli au nadanganya. Lakini, hata kama huniamini mimi unaweza kumuuliza mtu mwingine. Kama yule mtu mwingine akaangalia barabarani na kukuta kweli kuna miiba naye atakuambia "njia ile ina miiba". Sasa hiyo fact.

Tatizo ninaloliona ni kuwa wewe huhitaji kujua kama hiyo njia ina miiba. Yaani huhitaji facts ili kufikia kuamua kama kitu ni kweli au la. Nilivyokuelewa ni kuwa kwa vile tayari unaamini Lowassa ni "is genuine, genuinity unaiona machoni, usoni na kusikia moyoni" na ni kutokana na hilo unahitimisha na kusema " Naamini toka moyoni mwangu, Lowassa ni mkweli" Sasa imani siwezi kupinga hata siku moja kwani watu wanaamini vitu mbalimbali kwa sababu mbalimbali lakini imani haiwezi kufanywa kuwa ni fact.

Mimi naweza kuonesha kuwa Lowassa si mkweli - kwa kudai kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea au kuwa alionewa na Kamati ya Mwakyembe. This is factually not true. Lowassa aliposema ndege yetu ya Tanzania "inapaa" he was not telling the truth. That too is a fact. Kama unakumbuka Nyerere alipodai kuwa anaweza kuiacha CCM kwa kuwa si mamake mzee Kawawa yeye akasema atafia CCM. Unakumbuka Nyerere alimwambia nini Kawawa?

Sasa, ninaheshimu uamuzi wako wa kumuunga mkono Lowassa lakini usiende mbali kiasi cha kupoteza uhuru wako wa kupima ukweli na kuufuata kokote utakakokuelekeza. Na kama ulivyosema hii ni siasa nakusihi tu uelewe kuwa Lowassa ni Mwanasiasa. DO NOT FORGET THAT. Niliwahi kuandika kuwa katika Tanzania sasa hivi hakuna a more calculating, methodical and cunning politician like Lowassa. Hii nayo ni kweli. He is smart probably more than any politician within the ruling party. Lakini kusema kuwa anafaa kuwa Rais hili bado sijashawishika.
 
kuna diwani wa kondoa huko kila leo anaimba lowassA ht huyu mfilisi wa jf ila kuhusu DR SLAAAA NO NO NOOOOOO
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, yote uliyoyasema kuhusu mimi ni kweli, namkubali Lowassa kwa sababu hizi hizi ulizozisema wewe "Niliwahi kuandika kuwa katika Tanzania sasa hivi hakuna a more calculating, methodical and cunning politician like Lowassa. Hii nayo ni kweli. He is smart probably more than any politician within the ruling party. Lakini kusema kuwa anafaa kuwa Rais hili bado sijashawishika"

Baada ya kuyasema hayo kuhusu Lowassa umeshanirahisishia sana kazi, ni kukushawishi na wewe, tumpiganie Lowassa mwisho wa siku, we'll all sail the same boat!.

Humu jf, wewe Mzee Mwanakijiji, uu miongoni mwa ma great thinkers wa ukweli mliosimama na kuhesabiwa!. Pia humu jf, kuna ma great thinkers wa ukweli na wengine wala hawaandiki sana, wengine wanajisomea tuu na kujinyamazia lakini ni really great thinkers na wapo, na wengine kwa kunyamaza kwao, hapo ndipo u great thinkers wao, ulipolalia!.

Ila humu pia tunao ma great thinkers ambao wanajidhania ni ma great thinkers kutokana na amount of rich information iliyomo kwenye vichwa vyao ama kwa kuitafuta ama simply by privilage ambao wanaamini kila mtetezi wa Lowassa kapewa pesa!.

Maadam wewe bado hujashawishika kwamba Lowassa anafaa kuwa rais wa nchi hii, nakuomba sana usiutumie ushawishi wako kutuaminisha sisi tunaoamini kwa imani tuu kuwa Lowassa ndio the best option CCM has for 2015!, nakuomba usituharibie dili letu!
 
Mkuu W. J. Malecela, mimi huwa nakuaminia sana linapokuja suala la inside CCM, ila kumbe kuna zile za inside inside uvunguni wewe pia zinakupiga chenga!?. Hivi mpaka leo hujagundua vile vimemo vya EL kushinikiza Richmond ipewe tenda, alikuwa anafanya kwa niaba?. Hivi hujui kwa nini EL hakuhojiwa na tume ya Mwakiembe?. Ulitegemea ahojiwe amvue nguo aliyemkingia kifua?. Hivi hujui kwa nini EL aliwajibika?. Unadhani aliwajibika ili kuonyesha uwajibikaji, au aliwajibika ili kumfichia aibu mtu fulani?!. Hivi kwa nini hujiulizi kwa nini EL mpaka kesho hajasema his role kwenye Richmond Saga?!. Hasemi kwa sababu kuna mtu anamsitiri aibu ya mwaka!.

Mkuu W. J. Malecela, jee unaujua msingi wa ile kauli ya "Mimi na JK hatukukutana Barabarani"!?. Kauli hiyo ilifuatia EL kukasirishwa na vuvuzela nyie wana CCM msio elewa mambo ya ndani, mliokuwa mkizivurumisha katika dhana ya kujivua gamba!, hasira zilizidi baada ya mmoja wenu kudanyanya umma eti vuvuzela analopuliza lina ok ya JK!, EL akajiuliza, hivi inawezekana vipi, mtu umfichie aibu yake, halafu upate taarifa ati anatuma vijana wajinga wajinga kupuliza tarumbeta la Ufisadi wa Richmond!?. EL akaamua kuwa mstaarabu, kutojibisha vuvuzela kwa vuvuzela, bali akawaambia "hatukukutana barabarani".

Nakuhakikishia subiri uchaguzi wa ndani ya chama chenu mwakani, utashuhudia anguko kuu la wapuliza vuvuzela wote, na tutakutana humu humu tukumbushane!.

Ukiondoa wasiwasi kuhusu afya yake, na kama Mungu wa TB Joshua ndie Mwenyewe aliye Juu, nakushauri endelea tuu na yale mazoezi ya Rambo, Chuck Norris na Anodi Shwaziniga ili tuje tuishuhudie ile movie yako ya kuingia msituni uliotuahidi!.

Tumshutumu na kumlaumu EL kwa mengine, lakini ni la Richmond tuu, EL ni mshika pembe tuu, wakati muafaka ukifiki, mtamjua mkamua maziwa ni nani na tayari ameshatayarishiwa lile fungu la tozo!
Mkuu, ukikamatwa na mali ya wizi wewe ni mwizi pia haijalishi kama umewekeshwa au la, EL angekuwa mzalendo asingeshiriki mchezo mchafu wa kulifilisi taifa. Hafai hata akipakwa jibini!!!!
 
ninachoelewa ni kuwa lowassa ana uungwaji mkono ila si kwa kiasi kilichoonyeshwa hapo juu. Pia mleta mada anapenda kujua sababu ya uungwaji mkono wa huyu jamaa ila naona list inaongezeka tu
 
''CCJ
Isingekufa kama waanzilishi wake wasingeahidiwa Lowassa kutopewa nafasi''.

Mkuu Malecela naomba ufafanuzi hapa maana naparudia ila natoka kapa
 
Waberoya, naomba kutofatiana na wewe, sio kweli kuwa CCM wote ni wezi!. Naomba tuwe more realistic bila kuendekeza hisia!
Japo ni kweli CCM wengi ni wezi, ila sio wote!. Ndani ya CCM bado kuna wasafi wachache, wengine nawajua ila usiombe niwataje!

Kuna wana CCM wanaishi kwenye object poverty, simply ni destitute!. They have nothing at all, hata kama labda wanamawazo ya kiiwizi but have nothing at all hata hicho cha kuiba hakuna!. Watu kama hawa kuwaita wezi, sio kuwatendea haki!.

Kuna viongozi wakubwa wa CCM, walikuwa na kila opportunities za kuiba na kujilimbikizia mali na kugeuka mabilionea!. Unaamini kuna viongozi wakuu waliokuwa wakiishi maeneo ya Oysterbay, walikuwa wajijifugia tu mbuzi /kuku kama miradi yao?. Unaweza kuamini kiongozi mkuu anaishi aneo la Sea View by the beach, anaishi na ng'ombe eneo hilo!. Sasa watu kama hawa, kuwaita wezi, kiukweli sio kuwatendea haki!.

Nimefika kwa baadhi yao ambao walikuwa safi, walilitumikia taifa hili kwa uadilifu mkubwa mpaka wakastaafu kwa heshima.Lakini baada ya kustaafu waligeuka masikini wa kutupwa na kuonewa huruma, sasa watu kama hawa, unapoaita wezi, sio kuwatendea haki!

Waberoya, wakati mwingine, tuwe wakweli, japo sio lazima sana kuwa wakweli kwenye keyboard ila tuwe wakweli ndani ya nafsi zetu!.

Mkuu pasco...naona unalazimisha!

Logic inakataa katakata katu kuwa kuna wasafi CCM yet ....ni wana CCM na wanaishi kutegemeana humo humo! hao unaowaita wasafi..wako kimya, simply because they are coward, wanapokea check safi zilizosainiwa na wachafu....wanapendekezwa kugombea ubunge na hao hao wachafu....wanapokea fedha za uchaguzi kutoka kwa wachafu...hata kupigiwa kampeni na wachafu!! ila katika umoja huu still hao wasafi ni wasafi, cant they resign??!!! you must be kidding! really!
 
Back
Top Bottom