Wakili Kibatala ahoji kwanini video ya ushahidi haionyeshi kwamba ilirekodiwa kwenye viwanja vya buibui?!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Mbowe na viongozi wenzake wa Chadema amehoji uhalali wa video ya ushahidi iliyopokelewa kama kielelezo kwa kuwa haionyeshi kama ilirekodiwa katika viwanja vya Buibui sehemu ulipofanyika mkutano wa Chadema.

Akijibu hoja hiyo shahidi wa upande wa mashtaka amesema eneo hill Halina kibao kinachoutambulisha uwanja huo kuwa unaitwa Buibui.
----------------------
SEHEMU YA I*

*Kesi Namba 112/2018 inayowakabili Viongozi wakuu wa Chadema na baadhi ya wabunge, Shahidi wa 6, Koplo Charles akiendelea na ushahidi wake na kujibu maswali ya Wakili wa Upande wa utetezi Wakili msomi Peter Kibatala.*

Kibatala - Vifaa vile tulivyotumia kuangalizia picha ulivitoa katika ushahidi wako kama vielelezo katika ushahidi wako, waya uliotumika kupeleka picha kwenye projector?

Shahidi - Sikutoa.

Kibatala - Ulisikia Hakimu akisema ni mali ya nani, eneo tunalotumia kutazama video, eneo lile?

Shahidi - mali ya mahakama

Kibatala - Yule I.T aliyekusaidia kuonyesha picha aliapishwa hajaapishwa?

Shahidi - sifahamu

Kibatala - Unasema ulipiga picha zoezi zima kwa ukamilifu hakuna sehemu imekatwakatwa?

Shahidi - haijakatwa

Kibatala - Kabla ya kusoma Diploma ya Uandishi wa habari, ulipitia form four, form six ?

Shahidi - form 4, nikafanya Certificate baadae Diploma

Kibatala - Form 4 shule gani?

Shahidi - Yombo Secondary School

Kibatala - Matokeo yako ya kidato cha 4?

Shahidi - Division 3

Kibatala - ya point ngapi?

Shahidi - Pointi 24

Kibatala - Katika zoezi zima wakati unaonyesha picha, uliongozwa na mtu yoyote kumtambulisha Washtakiwa mmoja mmoja kwamba huyu ni Mbowe, huyu, Msigwa, huyu, Heche,huyu, Ester Bulaya, huyu Halima Mdee?

Shahidi - Sikuelekezwa

Kibatala - Ni nani aliyekuwa anatoa ushahidi wa kielelezo namba 5, (P.5) ?

Shahidi - Mimi

Kibatala - Ester Matiko alisema chcohote kwenye kielelezo P.5?

Kibatala - Ni sahihi hata leo hii hapa hukumtaja Ester Matiko?

Shahidi - Ni sahihi

Kibatala - Unafahamu kwamba alikuwa jimboni kwake kwa shughuli za kikazi kama Mbunge?

Shahidi - Sio kazi yangu kufahamua alikuwepo au hakuwepo

Kibatala - Unafanya kazi Kitengo Cha Forensic investigation katika Kitengo hiko?

Shahidi - Forensic iko Makao Makuu mimi niko ofisi ya mpelelezi Oysterbay Kinondoni

Kibatala - Kazi ya Kitengo Cha Forensic investigation ni kufanyia uchunguzi wa kitaalam kuchunguza nyaraka na kutoa nyaraka sambamba na kielelezo?

Shahidi - sifahamu

Kibatala - Katika ushahidi wako ulishaonyesha nyaraka yoyote kwamba kielelezo ulichokileta kilifanyiwa uchunguzi na Kitengo Cha Forensic investigation?

Shahidi - Sikuonyesha

Kibatala - Unafahamu au ufahamu kwa mujibu wa sheria kuna certificate hutolewa katika makosa ya jinai, kuthibitisha uchunguzi uliofanywa?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Ni sahihi picha zilianza kuonekana mwisho, ilianza mwisho alafu uka-rewind?

Shahidi - Ni sahihi

Kibatala - Ulitoa ufafanuzi wowote?

Shahidi - Hapana

Kibatala - Kuna wakati wowote uliwahi kuwapa kielelezo P.5 Kitengo cha Mashtaka?

Shahidi - sikuwahi kuwapa

Kibatala - Kuna mwendesha Mashtaka yoyote alikuwepo siku ya tukio pale leo yupo hapa?

Shahidi - Hapana

Kibatala - Ni sahihi kusema kwamba kuna mashtaka yamekwa hayapo kwenye ushahidi wako wa picha P.5?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Ni sahihi umekuja kutoa ushahidi kuthibitisha yaliyopo kwenye hati ya mashtaka?

Shahidi - Ni sahihi

Kibatala - Hukuwahi kutoa mahakamani karatasi yoyote kuthibitisha vitu ulivyovileta mahakamani?

Shahidi - Sahihi

Kibatala - Isaidie kuikumbusha Mahakama ni maneno gani aliyasema Mwita Waitara?

Shahidi - Siwezi kuyakumbuka mpaka niangalie video

Kibatala - Unamjua Mwita Waitara?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Hufahamu kama Naibu Waziri TAMISEMI?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Waitara unamuona hapa?

Shahidi - hayupo

Kibatala - Ushawahi kusikia kitu kinaitwa Selective Justice?

Shahidi - Hapana

Kibatala - Jeshi la Polisi linawezaje kujua Kama linapendwa au kuna chuki dhidi yake, au unadhani jeshi la Polisi linachukukiwaje?

Shahidi - Vizuri

Kibatala - kwa ufahamu wako, unadhani wanachama wa Chadema wanalichukiliaje jeshi la Polisi?

Shahidi - Vizuri na kutoa ushirikiano

Kibatala - Upendo ni ule ule licha ya yote ambayo yalitokea toka siku ile na matukio mengine mbalimbali?

Shahidi - Ni sahihi

Kibatala - Ni sahihi kwamba sifa za jeshi la Polisi ni kutatua uhalifu?

Shahidi - Ni sahihi

Kibatala - Wakili ambae hashindi kesi utakwenda kwake?

Shahidi - Huwezi

Kibatala - Jeshi la Polisi kama hawawezi kutatua uhalifu utaliamini na kulipenda?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Kwa mfano nikisema silioendi jeshi la Polisi ni kosa la jinai?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Nikiwaambia wenzangu 20 tulichukie jeshi la Polisi ni kosa au sio kosa?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unamfahamu Ben Sanane?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Mwandishi wa habari Azory Gwanda?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Mdude Nyagali?

Shahidi - Simfahamu

Kibatala - Lissu?

Shahidi - Namfahamu

Kibatala - Ni mwanachama wa chama gani?

Shahidi - Ni Chadema

Kibatala - Unafahamu ni Mbunge?

Shahidi - sio Mbunge

Kibatala - Unafahamu alikuwa Mbunge?

Shahidi - Nafahamu

Kibatala - Unajua alishambuliwa kwa risasi katika eneo la nyymbani kwake?

Shahidi - Nafahamu lakini sijui alishambuliwa wapi

Kibatala - Unafahamu amewahi kukamatwa mara kadhaa na kulala ndani polisi?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Toka Lissu ashambuliwe kwa risasi kumelijenga au kubomoa heshima ya jeshi la Polisi?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unamjua Diwani wa Morogoro Fares Nangoye

Shahidi - Simfahamu

Kibatala - Kusema kutoogopa mabomu ni kosa jinai?

Shahidi - Sifahamu Mheshimiwa

Kibatala - Ni sahihi maneno haya yalitumika kwenye mkutano wa kufunga kampeni katika mkutano wa Chadema?

Shahidi - Ni sahihi

Kibatala - Kuna yoyote kati ya washtakiwa hawa ulimsikia akisema wananchi wasishiriki kupiga kura?

Shahidi - Sikusikia

Kibatala - Ni sahihi walihamasisha wananchi kwenda kupiga kura?

Shahidi - sio sahihi

Kibatala - Hakuna mahali Mhe Halima Mdee alisema watu wakapige kura?

Shahidi - hakusema

Kibatala - Magufuli ni M/kiti wa chama gani?

Shahidi - Ccm

Kibatala - Katika Uchaguzi ule Ccm ilikuwa na mgombea haikuwa na mgombea?

Shahidi - ilikuwa na mgombea

Kibatala - Jina lake ?

Shahidi - Mtulia

Kibatala - Magufuli alimpigia kampeni hakumpigia?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Magufuli alitakiwa kuchinjwa lini?

Shahidi - maneno hayo yalitamkwa tarehe 16/2/2018

Kibatala - Ni kweli alisema kesho yake wakamchinje?

Shahidi - Sahihi

Kibatala - alisema wakamchinje Magufuli tarehe ngapi, mwezi gani, na mwaka gani?

Shahidi -

Kibatala - Wewe ni mtaalam wa lugha zote Tanzania?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unafahamu maudhui (content) kuchinja katika Uchaguzi, hujui kuna vichinjio, kadi ya mpiga kura?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unafahamu uchaguzi ulifanyika kwa mujibu wa Katiba, sheria na sio kwa hisani ya mtu?

Shahidi - sahihi

Kibatala - Magufuli amechinjwa hajachinjwa?

Shahidi - Magufuli hajachinjwa

Kibatala - Nani alikamatwa akijaribu kumchinja Magufuli?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Kadi ya kura ni kichinjio?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Kibatala, Mhe Halima Mdee alisema tukamchinje Magufuli na utawala wake?

Shahidi -

Kibatala - Unafahamu hadi saa 12 jioni, kesho ikiwa ni uchaguzi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni alikuwa hajatoa viapo vya mawakala wa Chadema?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Hivi viapo ni haki ya kisheria au hisani?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unajua zinatolewa kwa utaratibu gani?

Shahidi Sifahamu

Kibatala - Mbowe alisema hatutaki fujo, hatutaua hata inzi?

Shahidi - Ni sahihi

Kibatala - Ni sahihi aliyasema maneno haya akitaka kuelekea kwa Mkurugenzi kuchukua viapo, barua za utambukisho wa mawakala?

Shahidi - Sahihi

Kibatala - Washtakiwa wote walihojiwa walionyeshwa video, wewe uliwahi kuwapa ofisi ya upelelezi kielelezo P.5 ?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Ni sahihi wewe hukuwahi kuwapa polisi P.5 ili kiwasaidie kuwahoji washtakiwa?

Shahidi - sijawapa

Kibatala - Unasisitiza washtakiwa walihojiwa na video nyingine kabisa sio yako?

Shahidi - sahihi

Kibatala - Kielelezo P.5 kinaonyesha hatua ya maandamano au hakionyeshi?

Shahidi - Kinaonyesha maandamano kuanzia uwanjani

Kibatala - Mpaka wapi?

Shahidi - Kama nilivyoeleza katika ushahidi wangu wa awali kazi yangu ilikuwa ni kupiga picha pale kwenye viwanja vya Bui Bui tu?

Kibatala - Kielelezo P.5 kinaonyesha maandamano yaliishia wapi?

Shahidi - Sifahamu
Kielelezo P.5 kinaonyesha maandamano yaliishia wapi?

Shahidi - Maeneo ya Kinondoni

Kibatala - Kinondoni ipi?

Shahidi - Mkwajuni

Kibatala - Ni sahihi kuna bonde hivi kuelekea Magomeni?

Shahidi - .........

Kibatala - Picha ulipiga ulikuwa kwenye gari au?

Shahidi - Nikiwa kwenye gari

Kibatala - gari ya aina gani, namba za gari?

Shahidi - Ushahidi wangu wa awali nilishaeleza

Kibatala - Gari gani au ya Nani

Shahidi - OCD

Kibatala - Jina lake?

Shahidi - Doto

Kibatala - alikuwepo Mkuu wa upelelezi ?

Shahidi - Siwezi kufahamu
Kibatala - Kwa ufahamu wako kuna waandishi wa habari walikuwa wanarekodi ?

Shahidi - Sifahamu kama walipiga picha au waliondoka

Kibatala - Kwenye kielelezo P.5 video ukiangalia unaona hata mtu mmoja ameshika mawe, fimbo, marungu, panga?

Shahidi - sikuona

Kibatala - Ni sahihi kwenye mkutano walikuwepo police officers mbalimbali ?

Shahidi - Sahihi walikuwepo

Kibatala - Tukienda kuangalia kielelezo P.5 tutaona wananchi wakishambulia polisi?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Angalau wananchi wakizomea polisi?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Kielelezo P.5 kinaonyesha Kiongozi yoyote wa Chadema akirusha mawe?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Ni Kiongozi gani alisema tukaandamane?

Shahidi - Mhe Mbowe

Kibatala - Mwambie Hakimu Salum Mwalim alisema maneno gani ambayo yanavunja sheria?

Shahidi - tarehe 16/2/2018 alisema, wananchi wafuatilie familia zao

Kibatala - Ni sahihi kwamba kwa sababu ilikuwa Ijumaa, aliienda msikitini akaswali akawa amefunga, ameomba vitu vingi kwamba watakaomdhulumu katika Uchaguzi wafuatilie familia zao wazione, dua zitawapata, watawahukumiwa na Mungu, katika muktadha huo?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Mimi ukinidhulumu, nikaapa Wallah Wallah Mungu akuue ni kosa la jinai?

Shahidi - Ni kosa ni kutishia kuua

Kibatala - Kosa linaitwaje?

Shahidi - Kutishia kuua kwa maneno

Kibatala - Wakati Wakili wa Serikali anasoma hati ya Mashtaka alisoma kosa la kutishia kwa maneno?

Shahidi - Halijasomwa

Kibatala - Mhe Mnyika alisema nini?

Shahidi - Mimi kazi yangu nilienda kupiga picha, sijui alisema nini

Kibatala - Ester Matiko aliongea kipi ambacho ni kosa la jinai?

Shahidi - Sikumbuki

Kibatala - Halima Mdee alisema sihitaji kusimulia madhila yote yanayomkumba kila mmoja wetu, haya yanatokana na utawala wa awamu ya 5, kesho tukamchinje Magufuli na vibaraka wake, kosa liko wapi?

Shahidi - ilisababisha chuki dhidi ya wananchi

Kibatala - dhidi ya Nani?

Shahidi - Serikali

Kibatala - Ni kosa kumchukia Rais na Serikali, hujamrushia mawe hujamtukana, ni kosa kumchukia?

Shahidi - Sijui

Kibatala - Mhe Halima Mdee alisema wampige mawe?

Shahidi - mimi kwa ufahamu wangu naona Ni kupandikiza chuki

Kibatala - baada ya kupandikiza chuki alisema waende Ikulu wakarushe mawe?

Shahidi - Kielelezo P.5 Kinaonyesha maneno hayo

Kibatala - alichochea wampige mawe Rais Magufuli?

Shahidi - sijasikia

Kibatala - Ni sahihi maneno haya yalisemwa siku moja kabla ya Uchaguzi wa marudio Jimbo la Kinondoni?

Shahidi - tarehe 16/2/2018

Kibatala - tumejipa kibali kutangulia mbele ya haki, Niko hapa kuliandaa Taifa, Afrika Kusini Jacob Zuma ametolewa kwa nguvu ya watu, hatima ya nchi hii ipo mikononi mwa wananchi, tupo tayari kubeba majeneza lakini nchi ikakombolewe, Kuna tatizo gani ?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - kesho patachimbika, watu wanauawa, wanapotea wanatekwa tabia hiyo lazima ikomeshwe, ni kesho yake patachimbika au ?

Shahidi - Sijui

Kibatala - Unafahamu iwapo kesho patachimbika ni kwamba wanachadema wajitokeze kwa wingi wakapige kura ?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unafahamu kuna watu wameokotwa kwenye mitaro, wamepotea wengine?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unafahamu Boss wako wa zamani Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Nchemba akiwahi kusema ile miili iliyookotwa ni wahamiaji haramu?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - tabia ya kuteka watu, kupitezwa tabia hiyo lazima ikomeshwe unajua Mhe Heche alitaka tabia hiyo ikomeshwe kwa namna gani?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unajuaje ili ukomeshwe wananchi wachague mgombea ambae atawatetea na kupipigia kelele tabia hiyo kwa nguvu ili ikome?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unajua ni mapambano ya aina gani ambayo Mhe Mbowe alisema atayaongoza ?

Shahidi - sijui

Kibatala - watu 100 watakao kufa wataleta haki ulijua watakufaje?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - nchi hii inadharaulika wanaume kama mademu, kuna mwandishi amepotea siku ya 87 leo, waliokuwa wanaambiwa wanaume kama mademu ni watu gani?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Nini kilitokea mpaka ukakimbia ?

Shahidi - vurugu na ghasia

Kibatala - Ulitishiwa kufanywa nini ukakimbia?

Shahidi - maneno ya kutishia

Kibatala - maneno gani ya mshtakiwa gani yalikufanya kuondoka uwanjani uwepo Mkwajuni?

Shahidi -

Kibatala - Kutoka uwanja wa Bui Bui Mwananyamala hadi Mkwajuni ukikadiria kuna umbali gani?

Shahidi - sijui

Kibatala - kielelezo P.5 kinaonyesha ukishambuliwa?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Watu waliokushambulia wako hapa?

Shahidi - Hawapo

Kibatala - Ulishambuliwa hukushambuliwa?

Shahidi -

Kibatala - Ester Bulaya alisemaje?

Shahidi - Sikumbuki yote mpaka tuangalie video lakini nakumbuka vita Ni vita mura

Kibatala - Unajua alimshinda gwiji wa siasa, Wasira katika Jimbo la Bunda Mjini?

Shahidi - sifahamu

Kibatala - maneno haya alitamka tarehe 16/2/2018 alitamka Kama alivyoshinda Bunda ndivyo watakavyoshinda Jimbo la Kinondoni vita ni vita mura?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unajua hii ni kauli ya kupeana hari hata wakati wa kulima shamba au kufanya bila kukata tamaa?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Ni sahihi alisema kule kwetu Musoma Vita ni vita?

Shahidi - ..........

Kibatala - maneno ya Nhe Peter Msigwa alisemaje?

Shahidi - watu watembee na silaha

Kibatala - Ni Sahihi alisema haihitaji kibali cha polisi kutembea na panga rungu mkuki au fimbo ?

Shahidi - yapo kwenye kielelezo P.5

Kibatala - inahitaji kibali cha polisi kutembea na rungu, panga, fimbo au mkuki?

Shahidi - inategemea

Kibatala - inategemea Nini?

Shahidi - inategemea na mandhari, inajulikana wamasai ndio wanatembea na fimbo na silaha

Kibatala - Unajuaje alimaanisha wamasai?

Shahidi - Sifahamu

*Inaendelea........*

SEHEMU YA II*

WAKILI KIBATALA VS P.W 6 - KOPLO CHARLES

Kibatala - Askari Fikiri na Rahim waliumia siku hiyo kwenye kielelezo P.5 tumeona?

Shahidi - Hapana

Kibatala - Kuna mahali tumeona Ngichi akitoa ilani kwenye ushahidi wako?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Unajua kilitokea kifo cha Akwilina Akwilin, kwenye kielelezo P.5 tutaona washtakiwa kusababisha kifo hiko?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - tukiangalia kwenye kielelezo P.5 tutaonana wananchi Mkwajuni wakikimbia huku na huku na kufunga maduka?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Kielelezo P.5 kinaonyesha washtakiwa 1 hadi 9 wakiandamana?

Shahidi - Hapana

Kibatala - Je wanaonekana wamekaa kikao wakijadili jambo?

Shahidi - Hapana

Kibatala - kupitia kielelezo P.5 na uwepo wako pale unaweza kujua idadi ya mawakala?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Tunaomba kupata facility ili tutazame tuweze kumuuliza shahidi maswali zaidi.

*Kesi imeahirishwa dakika 20 kuelekea kwenye chumba maalum kutazama ushahidi wa picha na maswali mengine kuendelea kuulizwa*

*Video Mwita Waitara "Watajaza polisi, tushaanza kazi ya kuwashughulikia polisi kabla hawajatushughulikia, Vijana tushawapa kazi maalum, Vijana washaanza kuifanya kazi hiyo Vizuri, polisi wapotee kabla wananchi hawajapotea, Kama kuna polisi watazuia watu wasilinde kura kesho polisi apotee, kabla wananchi hawajapotea, Vijana wanataka hata sasa wako tayari, na haya maneno namwambia IGP Sirro awaambie Vijana wake watulie tuli kama maji ya mtungi, katika mkutano huu Hakuna Mwananchi wa kawaida wote ni wanajeshi"*

Kibatala - Hakuna kosa la jinai kwenye maneno hayo?

Shahidi - Hakuna kosa

Kibatala - Kwanini Hakuna kosa?

Shahidi - kazi yangu ni kupiga picha, Ila kwa ufahamu wangu hakuna kosa.

Kibatala - polisi watashughulikiwa huoni ni kosa?

Shahid - kwa ufahamu wangu Hakuna kosa

Kibatala - Kuna chochote kiliwatokea maafisa wa polisi baada ya maneno ya Waitara?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Kielelezo P.5 kuna mahali Kinaonyesha haya ni mazingira ya Bui Bui?

Shahidi - Mimi ndiyo nilikuwa nachukuwa kwa hiyo naweza kusema nilirekodi nikiwa uwanja wa Bui Bui

Kibatala - Acha ushahidi wako kuna sehemu yoyote inaonekana ukakua hapa ni uwanja wa Buibui?

Shahidi - vinakwenda sambamba na Mimi ndo naweza kusema nilirekodi eneo gani

Kibatala - Unaweza ukaonyesha kwenye Kielelezo P.5 kwamba hapa ni uwanja wa Buibui?

Shahidi - Hakuna

Kibatala - Ni wapi picha itainyesha ilipigwa tarehe 16/2/2018?

Shahidi - mimi nilikuwepo eneo la tukio hivyo najua tarehe niliyorekodi ilikuwa tarehe 16/2/2018
Kibatala - Kielelezo P.5 inaonyesha tarehe iliyorekodiwa?

Shahidi - Hakuna tarehe

Kibatala - Inaonyesha muda ambao ilianza kurekodi (Duration)?

Shahidi - ndio inaonyesha

Kibatala - Ni sahihi kwamba mpaka unaacha kurekodi ilikuwa na space ya kuweza kuhifadhi picha?

Shahidi - Ndio zilibaki kama dakika 30

Kibatala - Ni sahihi hizo dakika 30 hazikutumika kurekodi yale Mambo niliyokuuliza kwanini hukuyarekodi?

Shahidi- unarekodi matukio muhimu sio kila tukio unarekodi

Kibatala - Kwa ufahamu wako watu kukimbia huko na huko haikuwa matukio muhimu?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Unasema kuna vitu vilikuogofya ukaondoka eneo la tukio ni vitu gani hivyo ambavyo vilikuogofya ambavyo hukuvirekodi?

Shahidi - ngoja ni-play

*Heche kabla Mambosasa hajaja hapa alikuwa Tarime nilishinda akiwa Tarime anajua mziki wetu*

Kibatala - Hayo maneno ndiyo yaliyokutisha?

Shahidi - Baada ya kumtaja Boss wangu na maneno yale ni viashiria vya vurugu na maisha yangu

Kibatala - anayefahamu mziki wa Heche Ni wewee au Mambosasa?

Shahidi - nilijua ni mimi nikiwa miongoni mwao

Kibatala - wewe ni Mambosasa?

Shahidi - Hapana

Kibatala - Heche ameutaja huo muziki unaujua ni muziki gani?

Shahidi hajautajwa

Kibatala - ulikuwepo Tarime wakati Heche anaonyesha muziki?

Shahidi - sikuwepo

Kibatala - ulishawahi kuongea na Mambosasa kuhusu kilichotokea Tarime?

Shahidi - sijawahi

Kibatala - Unafahamu kwamba Heche ni mwanamuziki mzuri na ndiye anayetunga nyimbo za Chadema?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - Ulitishika na nini hasa hapo?

Shahidi - Hayo yalikuwa Ni maneno yenye viashiria vya uvunjifu wa amani na hata akisema polisi nirekodi nilikuwa ni mimi naambiwa

Kibatala - mstari gani hapo ulikutisha?

Shahidi - yote

*Inaendelea.....*

SEHEMU YA III*

KIBATALA - Uliona kuna kura pale uwanjani zinatakiwa kulindwa?

Shahidi - Hapana

Kibatala - Siku ya tukio ulikuwa umevaa uniform au kiraia?

Shahidi - Uniform

Kibatala - Askari wengine waliondoka au niwewe tu?

Shahidi - sikuona

Kibatala - Waandishi wa habari waliondoka au waliendelea kurekodi?

Shahidi - Sijui

Kibatala - Kitu kingine kilichokutishia?

Shahidi - Ester Bulaya, aliniambia Askari nirekodi Vizuri

Kibatala - mtu akiakwambia rekodi anakusaidia ufanye kazi kwa ufasaha ni vibaya?

Shahidi - ilikuwa Ni tushio

Kibatala - Uliandika maelezo ya kutishiwa

Shahidi - sikuandika maelezo

Kibatala - katika shtaka la 5, 6, 9 na 10, Kuna mahali Mhe Mbowe alitamka tuandamane ?

Shahidi - Sikusikia/Hakuna

Kibatala - Wapi Mhe Ester Bulaya alisisitiza watu waandamane?

Shahidi - sijaona

Kibatala - Jana Ulisema utamuonyesha Mhe Ester Matiko akiwa uwanja wa Bui Bui

Shahidi - sikusema

Kibatala - Ni sahihi kielelezo P.5 kinamuonyesha Mhe Mnyika akiwa amefanya mkutano usio halali?

Shahidi - Sijui

Kibatala - Ni sahihi kielelezo P.5 kinamuonyesha Mhe Mashinji akiwa amefanya mkutano usio halali?

Shahidi - Sijui

Kibatala - Ni sahihi kielelezo P.5 kinamuonyesha Mhe Msigwa akiwa amefanya mkutano usio halali?

Shahidi - sijui

Kibatala - Wakati unaambiwa nenda kafanye kazi mkutano wa Chadema, uliambiwa ni mkutano halali au sio halali?

Shahidi - Sikuambiwa ni halali au sio halali

Kibatala - Uliambiwa mkutano wa Chama gani?

Shahidi - Chadema

Kibatala - Ni sahihi kwa dakika 56 hukuona afisa wa polisi akisema ondokeni ondokeni mkutano huu sio halali?

Shahidi - sikuona

Kibatala - Ni sahihi kielelezo P.5 hakionyeshi sehemu inaonyesha ile ni barabara ya Kawawa ?

Shahidi - hakuna

Kibatala - Ni sahihi kielelezo P.5 hakionyeshi watuhumiwa wakiandamana?

Shahidi - hakionyeshi

Kibatala - Ni sahihi Mhe Mbowe alisema hatutaki fujo, hatokufa inzi, tunafuata vitambulisho kwa Mkurugenzi?

Shahidi - Ni sahihi, huwezi kufuata vitambulisho kwa umati wa watu wote ule

Kibatala - hayo maneno aliyasema kuhusiana na tukio gani?

Shahidi - Sifahamu

Kibatala - kwenye kielelezo P.5 kuna mahali Mhe Mbowe anaoneka akiwaambia wananchi wafanye fujo?

Shahidi - Ndio

Kibatala - Tuonyeshe

Shahidi - Anatafuta eneo la Mhe Mbowe

*Bado hajapata, Wakili Kibatala anamuachia Wakili Msomi Jeremiah Mtobesya*

Mtobesya - Unamjua mlalamikaji kwenye kesi hii?

Shahidi - Sifahamu

Mtobesya - ikumbushe Mahakama nani alikutuma uende kurekodi mkutano wa Chadema?

Shahidi - RCO

Mtobesya - Ni sahihi ulimpa mrejesho kwa maandishi?

Shahidi - Hapana kwa mdomo

Mtobesya - baada ya kumpa mrejesho kwa mdomo alikwambia ufanyaje?

Shahidi - alisema nitunze ushahidi sababu kuna kesi imefunguliwa
Mtobesya - wewe ndiye uliyerekodi, ukatunza na kuleta mahakamani?

Shahidi - Ni sahihi
Mtobesya - Ieleze Mahakama kama wewe Ni mtaalam wa sauti?

Shahidi - Mimi ni mpiga picha

Mtobesya - Unawezaje ukajua hii ni sauti ya fulani na hii sio fulani?

Shahidi - Picha na sauti

Mtobesya - Kwanini unasema yule ni fulani ndo kasema vile?

Shahidi - sababu nilikuwepo pale nilirekodi

Mtobesya - Sauti ilikusaidia kujua huyu ni fulani?

Shahidi - ndio

Mtobesya - ulishawahi kuleta sauti ili ulinganishe sauti uliyosema uliwasikia wakisema hayo maneno?

Shahidi - sijaleta

Mtobesya - Una utaalamu na kompyuta?

Shahidi - Sifahamu

Mtobesya - Unafahamu kitu kinaitwa deep fake?

Shahidi - Sifahamu

Mtobesya - nitakuwa Sahihi nikisema matukio yamekatwa katwa kuhaririwa ?

Shahidi - sio sahihi

Mtobesya - Ni sahihi hayakuwa kwenye mtiririko mmoja?

Shahidi - Sijaedit , hiyo Ni kutokana na ku-pause nakuwa nimeacha kurekodi baadae naendelea kwenye tukio lingine

Mtobesya - Uki- pause Ina maana na really life matukio mengine yanapause?

Shahidi - sio kweli

Mtobesya - Ndo nakuuliza kwa hiyo unaacha kurekodi matukio mengine, Yani ukiweka pause na matukio mengine yanakusubiri mpaka nawewe uje uanze kurekodi?

Shahidi - Narekodi tukio la muhimu ambacho sijarekodi sio tukio muhimu

Mtobesya - Tukio ni nini?

Shahidi - Ni kama hapa tulipo ni tukio linaweza likawa recorded au tukio lingine ni kama lile mkutano wa Chadema tarehe 16/2/2018.

Mtobesya - Ni sahihi Jana hukueleza ni jinsi gani hiyo DIV haiwezi kuhaririwa?

Shahidi - sio jana nilieleza tangu ushahidi wangu mwanzo wakati nawasilisha vielelezo hivi mahakamani

Mtobesya - Ni sahihi Jana hukueleza ni jinsi gani hiyo DIV haiwezi kuhaririwa?

Shahidi - nilishaonyesha mwanzo kwenye ushahidi wa mwanzo

Mtobesya - Wapi?

Shahidi - wakati natoa ushahidi mwanzo

Mtobesya - wakati unaweka seal Mahakama ilikuwepo?

Shahidi - Mahakama haikuwepo

Mtobesya - ni Sahihi kuhariri unatumia software na kurekodi ni software?

Shahidi - Sifahamu

Mtobesya - Ni sahihi kitu kinachorekodiwa kinaweza kuhaririwa kwa kutumia teknolojia?

Shahidi - Sifahamu

Mtobesya - Isaidie mahakama ni wakati gani wapelelezi walisema itakuwa ni Kielelezo?

Mtobesya - Sikupewa na upelelezi nilipewa na RCO

Mtobesya - Nitakosea nikisema RCO ni Mkuu wa upelelezi?

Shahidi - Hukosei

Mtobesya - ni wakati gani uliwapatia wapelelezi Kielelezo?

Shahidi ..........

Mtobesya - Uliandika statement wakati unakabidhi , uliandika tarehe?

Shahidi - tarehe 16/2/2018

Mtobesya - Baada ya kuandika ulimkabidhi nani?

Shahidi - RCO

Mtobesya - Unajua Kuna teknolojia ya ku-edit watu na sauti?

Shahidi - Sijui

Mtobesya - Ieleze Mahakama ulifundishwa Masuala ya kompyuta na level yako ya kompyuta?

Shahidi - Kawaida tu, kuwasha kompyuta, kutype documents

Mtobesya - Hakuna sehemu umejifunza ku-edit?

Shahidi - Sikumbuki

Mtobesya - Diploma ya Uandishi wa habari umemaliza lini?

Shahidi - 2011

Mtobesya - Almost 8 years

Shahidi - I think so

*Wakili Hekima Mwasipu Vs PW 6 Koplo Charles*

Hekima - Wewe unafanya kazi chini ya RCO?

Shahidi - sahihi

Hekima - Kwa maana hiyo huwezi kufanya chochote bila RCO?

Shahidi - Sahihi

Hekima - Ni sahihi RCO tarehe 16/2/2018 alikutuma kurekodi mkutano wa Chadema?

Shahidi - Ni sahihi

Hekima - Ni sahihi kuna alienda kurekodi mkutano wa Ccm?

Shahidi - Sifahamu

Hekima - Baada ya kurekodi ulipeleka vifaa kwa RCO?

Shahidi - sahihi

Hekima - Ulimwambia nini!

Shahidi - matukio

Hekima - Matukio yapi?

Shahidi - vurugu

Hekima - RCO alikupa taatifa kuna vurugu kupitia vyanzo vyake?

Shahidi - sio sahihi
Hekima - Mpelelezi wa kesi hii unamfahamu

Shahidi - Simfahamu

Hekima - Kwanini unasema hivyo?

Shahidi - kila kesi inakuwa mpelelezi wake

Hekima - Mtu akisema ukicheka polisi na Ccm amefanya kosa?

Shahidi - Sifahamu
Hekima - Ulishawahi kusikia kuna watu wameuawa na kupotea?

Shahidi - Sifahamu

Hekima - Nini maana ya kuchimbika?

Shahidi - vurugu

Hekima - Kuchimbika ni nini?

Shahidi - vurugu

Hekima - Unafahamu wizi unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano?

Shahidi - Sifahamu

Hekima - Sahihi Lissu amepigwa risasi

Hekima - ni kosa mtu kukemea mtu kupigwa risasi?

Shahidi - Sifahamu

Hekima - Suluhu ya nchi hii iko mikononi mwa wananchi Unajua maana yake?

Shahidi - Sijui

Hekima - Kusema kubeba majeneza ni kosa?

Shahidi - ni kosa ukiwa kwenye mkutano

Hekima - Unajua maana ya Kama mbwai na iwe mbwai?

Shahidi - Nafahamu

Hekima - Unajua madhila yanayomkumba kila mmoja?

Shahidi - Sijui

Top of Form
Bottom of Form
 
Wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Mbowe na viongozi wenzake wa Chadema amehoji uhalali wa video ya ushahidi iliyopokelewa kama kielelezo kwa kuwa haionyeshi kama ilirekodiwa katika viwanja vya Buibui sehemu ulipofanyika mkutano wa Chadema.

Akijibu hoja hiyo shahidi wa upande wa mashtaka amesema eneo hill Halina kibao kinachoutambulisha uwanja huo kuwa unaitwa Buibui.

Source Star TV habari!

Maendeleo hayana vyama!


Wale wa ukweli na uhakika wameiwasilishaje hii
 
Mimi nina imani kesi hizi ndogo za kisiasa, mwenyekiti wa Sadc ataziondosha kutoa somo kwa wengine.
 
Wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Mbowe na viongozi wenzake wa Chadema amehoji uhalali wa video ya ushahidi iliyopokelewa kama kielelezo kwa kuwa haionyeshi kama ilirekodiwa katika viwanja vya Buibui sehemu ulipofanyika mkutano wa Chadema.

Akijibu hoja hiyo shahidi wa upande wa mashtaka amesema eneo hill Halina kibao kinachoutambulisha uwanja huo kuwa unaitwa Buibui.

Source Star TV habari!

Maendeleo hayana vyama!
Kwahiyo hiyo vidio ni feki itakuwa imeletwa toka Kongo hongera wakili kwa kuwagundua wahuni.
 
Wakili wa utetezi katika kesi inayomkabili Mbowe na viongozi wenzake wa Chadema amehoji uhalali wa video ya ushahidi iliyopokelewa kama kielelezo kwa kuwa haionyeshi kama ilirekodiwa katika viwanja vya Buibui sehemu ulipofanyika mkutano wa Chadema.

Akijibu hoja hiyo shahidi wa upande wa mashtaka amesema eneo hill Halina kibao kinachoutambulisha uwanja huo kuwa unaitwa Buibui.

Source Star TV habari!

Maendeleo hayana vyama!
Sasa huku ulikoleta huu uzi ndio mahakamani?unataka tukubali au tukanunesha,halafu itasaidia nini mahakamani tukijibu huku,Ufipa mnafurahisha sana kwa kuifanya JF ,Mahakama,Bunge,Polisi ,TISS ...
 
Back
Top Bottom