Hawa ndiyo wabunge wa viti Maalum CHADEMA, CCM na CUF

siku hizi sisomi habari leo, mtanzania sijui deile nyuzi na mengine yanayofanana hayo
 
kwa hiyo kama ccm wanachaguwana kiundugu, chadema nao wakifanya hivyo ni sawa!!!! Au ulikuwa unataka kumaanisha nini sijui!!!
Sidanganyikiiiii!!!! Msinichanganye nipoteze focus hapa!! Hebu tukumbuke wapi vile tuliishia kwenye yale mambo ya msingi kama kupanga mikakati na kuhamasishana kulinda kura zetu j2, na kuiweka serikali tunayoitaka kazini. Wakubwa tuachane na hawa wafa maji!!
 
CCM iko hivi...
The Dreamer, asante kwa nondo kali za kilio cha Waislamu, hukuwa na haja ya cut and paste document yote kwenye post yako, ungeweza tuu kuiweka kama attachment, hivyo ku save time kwa wale ambao huwa wana pelusi tuu jf.

Mode, saidia kuiattach hiyo document.
 
Kuwapendekeza wanawake wote walio pata ujasiri wa kugombea majimboni ni jambo la maana sana na lenye kuwaongezea ujasiri wanawake hao mashujaa. Ukiangalia list hiyo hakuna aliyebebwa kwa undugu/uswahiba wake na viongozi ila kila mtu ana lake alilolifanyia chama ambalo kwa wale walio karibu na Chadema wanaelewa.
Hata wasemeje mwaka huu ni kifo cha mende.
 
Zubeda;
Nakushauri siku nyingine tafuta ukweli ndani ya chama chako kabla hujaleta habari kama hii ndani ya JF;hawa chini wafuatao ndiyo baadhi ya walioshinda ktk viti maalum ndani ya CCM

Je Zubeda unajua akina mama hawa ama wazazi wao au waume zao walikuwa au ni akina nani ndani ya CCM?Walioshinda viti maalum CCM ni:

Tina Andrew Chenge -Shinyanga

Namelok Edward Moringe Sokoine-Manyara

Salma Musa Bilal-ZNZ

Anna Margreth Abdallah Msekwa -NGO

Magretth Samwel Sitta-Tabora

Rosemary Kasimbi Kigirini-Mara

Janeth Maurice Masaburi-Dar

Rukia Masasi-Iringa

Zarina Shamte Madabida-Dar

Mboni Mohamed Mhita-youth

Asha Bakari Makame-ZNZ

Aziza unawajua akina mama hao niliowataja juu ndugu zao ndani ya CCM;madudu ya kuwapa vyeo ndugu zao yanaongozwa na CCM na ushahidi ni huo hapo juu ambapo karibu vigogo wote wa CCM wana ndugu zao kwenye viti maalum!
Malafyale Umemaliza/Umalile, Tofauti ya CCM na Chadema, Chadema wanangalia sifa kwanza, Linganisha CVs za hao wateule wa CCM na Chadema. CCM wanangalia either Sura, uhusiano na kigogo fulani na kimbelembele cha kukiimbia chama.
 
The Dreamer, asante kwa nondo kali za kilio cha Waislamu, hukuwa na haja ya cut and paste document yote kwenye post yako, ungeweza tuu kuiweka kama attachment, hivyo ku save time kwa wale ambao huwa wana pelusi tuu jf.

Mode, saidia kuiattach hiyo document.

Mkwe, mtoto, even first lady. Eti mliajiri consultant kuchagua ndugu zenu. Unbelievable. Yaani mke wa Slaa yupo kwenye viti maalumu. This is over the top.

Kitu kibaya zaidi ni notion kwamba watu wanagombea katika majimbo yao, halafu still wako kwenye viti maalum. This is over the top upendeleo. Yaani hakuna kina mama wengine wenye uwezo hadi mchague hao wakwe zenu kwenye nafasi mbili mbili.

Halafu mnataka tuwape nchi. Hamko serious nyie.
 
mbona JK alitaka kumpa unaibu balozi wa uingereza? tuangalieni maslahi
 
mmmh ..............viongozi familia ya vigogo inamaanisha chama hakina sample ya kutosha ya kupata variety ya viongozi au?
 
Huu ushabiki usio na kichwa wala miguu ni vema tukaupuuzia.
Mleta hoja angetwambia ni nani ambaye aliomba nafasi na ana vigezo sahihi na ailiachwa????
Kama kuna mtu ana sifa ya kuwa kiongozi ana haki jamani!! wengi tunakataa kumpa mtu nafasi swababu ni mtoto wa fulani hata kama hana uwezo.
 
Habari leo kwani inatofauti na Gazeti la Uhuru na Mzalendo! mimi nilifikiri habari hii imetoka kwenye Gazeti makini kumbe! Hawa ni walewale wazushi waliobanwa mbavu na CHADEMA.

Hatudanganyiki!
 
Je Zubeda unajua akina mama hawa ama wazazi wao au waume zao walikuwa au ni akina nani ndani ya CCM?Walioshinda viti maalum CCM ni:

Tina Andrew Chenge -Shinyanga

Namelok Edward Moringe Sokoine-Manyara

Salma Musa Bilal-ZNZ

Anna Margreth Abdallah Msekwa -NGO

Magretth Samwel Sitta-Tabora

Rosemary Kasimbi Kigirini-Mara

Janeth Maurice Masaburi-Dar

Rukia Masasi-Iringa

Zarina Shamte Madabida-Dar

Mboni Mohamed Mhita-youth

Asha Bakari Makame-ZNZ

Aziza unawajua akina mam

Habari Leo tupasheni na hizi za CCM kidogo bila ya ubaguzi............
 
Kuwapendekeza wanawake wote walio pata ujasiri wa kugombea majimboni ni jambo la maana sana na lenye kuwaongezea ujasiri wanawake hao mashujaa. Ukiangalia list hiyo hakuna aliyebebwa kwa undugu/uswahiba wake na viongozi ila kila mtu ana lake alilolifanyia chama ambalo kwa wale walio karibu na Chadema wanaelewa.
Hata wasemeje mwaka huu ni kifo cha mende.


Uchaguzi huu umetulia, umeenda shule kwa ku-focus mbele kama mcheza Chess anavyopanga kete, umeeangalia all angles,all properbilities etc..hongereni Chadema wala msihangaike nao kujibu lolote kwa hili endeleeni kushambulia jukwaa mpaka 31 kieleweke
 
Hata hizo 3000 ninamashaka nazo, halisomeki, pia kuna redio fulani inatabia ya kusoma vichwa vya habari kila asubuhi, kuna baadhi ya habari za wale wasema kweli huwa wanaziruka lakini zikiwa mbaya kwa chadema zitasomwa kwa kirefu. Tutawakimbia ndipo watajua jamii ina nguvu
 
Hivi nyie hao WAISLAMU mnaowaona wajinga sana ama vipi? Huyo Slaa alihusika kikamilifu kwenye sakata la Mwembechai. Na vile aeleze msimamo wake kuhusiana na Mahakama ya Kadhi na OIC?

Hizi cheap propaganda zenu zishapitwa na wak'ti.
 
Zubeda;
Nakushauri siku nyingine tafuta ukweli ndani ya chama chako kabla hujaleta habari kama hii ndani ya JF;hawa chini wafuatao ndiyo baadhi ya walioshinda ktk viti maalum ndani ya CCM

Je Zubeda unajua akina mama hawa ama wazazi wao au waume zao walikuwa au ni akina nani ndani ya CCM?Walioshinda viti maalum CCM ni:

Tina Andrew Chenge -Shinyanga

Namelok Edward Moringe Sokoine-Manyara

Salma Musa Bilal-ZNZ

Anna Margreth Abdallah Msekwa -NGO

Magretth Samwel Sitta-Tabora

Rosemary Kasimbi Kigirini-Mara

Janeth Maurice Masaburi-Dar

Rukia Masasi-Iringa

Zarina Shamte Madabida-Dar

Mboni Mohamed Mhita-youth

Asha Bakari Makame-ZNZ

Aziza unawajua akina mama hao niliowataja juu ndugu zao ndani ya CCM;madudu ya kuwapa vyeo ndugu zao yanaongozwa na CCM na ushahidi ni huo hapo juu ambapo karibu vigogo wote wa CCM wana ndugu zao kwenye viti maalum!

Malafyale,

Tofauti ni kwamba hao wa CCM wamechaguliwa na wanachama wanawake wenzao wakati hawa wa CHADEMA wameteuliwa na panel.

Ndio maana walikuwa wanaficha majina kwasababu ni unafiki tu umejaa, unapinga jambo moja na kufanya hilo hilo.
 
Yaani nimecheka mpaka mbavu zikauma!!!
Yaani mke wa Slaa, mama mkwe, mtoto wa Ndesamburo, dada wa Mbowe, shemeji wa zitto Kabwe, na ndugu na marafiki wa vigogo wa Chadema wako katika listi ya wabunge wa kuteuliwa!!!!!!!!!!!

Sasa mbona Slaa anatudanganya ktk midahalo na kampeni zake kuwa utawala wake utafuata katiba na sheria!! Undugu na urafiki hautaangaliwa ktk kuchagua viongozi?

SASA CHADEMA MUNAMLAUMU JK KUTUMIA FAMILIA YAKE KTK KAMPENI WAKATI NYINYI MUNACHAGUANA KINDUGU NA KIFAMILIA NA HII NI HATARI ZAIDI!!!

Sasa huu kama sio unafiki ni nini? Tutamuamini vipi slaa kuwaRais wetu? Kama ameweza kuingiza undugu na urafiki ktk uteuzi wao, basi sitashangaa kama ukabila na udini ukipewe nafasi ya juu ktk serikali ya Chadema!!!! Na ushahidi ni huu wa kuteua wabunge wa kuteuliwa zaidi ya asilimia 90 wakiwa ni wa dini moja!!!

Wananchi wenzangu tuwe macho na ahadi na sera za chadema kwani ni za uongo na watairudisha nchi nyuma kimaendeleo!!!
Adabu yao ni kuwanyima kura jumapili na afadhali tuwape CUF ambao ni waadilifu na wala hawana kashfa yoyote isipokuwa fitina na uzushi wa chama hiki cha wa Chagga kuwa CUF ni chama cha waislamu!!!

...kigezo kilikuwa ni uwezo binafsi na jinsi anavyotumikia chama na mapenzi kwa taifa lake. mtoto wa kigogo hapotezi haki yake kwa sbb tu baba yupo madarakani,kigezo ni uadilifu. ulitaka wampe sofia Simba?au ulitaka wawaombe wanachichiem kuwapa nafasi?au ni nani mwenye sifa amekosa nafasi hizo?....
 
Lawama hizo zimejidhihirisha kwani katika orodha hiyo, mbali na watoto na ndugu wa vigogo wa chama hicho, pia wabunge wote wa viti maalumu wa Chadema waliomaliza muda wao, wakiwamo wanaogombea katika majimbo ya uchaguzi, wamerudishwa katika orodha hiyo na kupewa nafasi za juu.

Wabunge waliomaliza muda wao walioko katika orodha hiyo ni Lucy Owenya ambaye ni mtoto wa mgombea ubunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo; na ni wa kwanza, jambo linalomhakikishia ubunge ikiwa uteuzi utafanyika kwa kufuata wa kwanza mpaka wa mwisho.

Wengine ni Mhonga Ruhwanya (namba 3), Halima Mdee (5), Grace Kiwelu (9) ambaye ni mkwewe Ndesamburo, Anna Komu (13) na Susan Lyimo (10).


Pia yumo Rose Kamil Sukum (19) ambaye ni mke wa mgombea urais wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa. Aidha, kwa mfumo huo wa Chadema, wagombea ubunge ambao wamo miongoni mwa majina hayo, watajihakikishia ‘ulaji’ bungeni endapo watashindwa katika majimbo hayo.

Wagombea hao wa majimbo walioko katika orodha hiyo ni Mdee wa Kawe, Leticia Nyerere (16), Kwimba; Regia Mtema (11), Kilombero na Sukum, Hanang. Wengine ni Christina Lissu Mughiwa (20) na Paulina Slaa Narcis (84).

Orodha hiyo pia imewataja Easther Matiko(2), Anna Mallac (4), Paulina Gekul (6), Conjesta Rwamlaza (7), Susan Kiwanga (8), Christowaja Mtinda (12), Mwanamrisho Abama (14), Joyce Mukya (15), Naomi Kaihula (17), Chiku Abwao (18), Raya Hamisi (21), Philipa Mturano (22) na Mariam Msabaha (23).

Wengine ni Rachel Mashishanga (24), Sabrina Sungura (25), Rebecca Mngodo (26), Cecilia Pareso (27), Subira Waziri (28), Leticia Musore (29), Helen Kayanza (30), Rosana Chapita (31), Mona Bitakwate (32), Evarim Mpangama (33), Asha Kayumba (34), Hija Wazee (35), Mary Martin (36), Sophia Mwakagenda (37), Bupe Kyambika (38), Magreth Mangowi (39), Esther Daffi (40), Jane Pesha (41), Aikande Kwayu (42) na Helga Mchomvu (43).

Pia orodha hiyo iliwataja walioteuliwa kuwa ni Rebecca Magwisha (44), Neema Msuya (45), Anastazia Manyanda (46), Selina Nguma (47), Bertha Matanwa (48), Christina Ngola (49), Lydia Mwaipaja (50), Zaituni Lubinza (51), Adelastela Kilindi (52), Hawa Mwaifunga (53), Loyce Iboma (54) na Rita Kanoro (55).

HabariLeo | Siri ya wabunge viti maalumu Chadema yavuja

1. Mbona habari Leo hawakuandika habari za kampeni ya Slaa ya jana pale Temeke?

2. Mbona wakina Vicky Kamata wamepewa uvitii maalum wakati wengine tunajua kabisa kwamba ni mademu wa Rais flani. Hipi mbaya? Kwanza nasikia yule balozi wa London ni demu wa Rais flani na yule chekbobu balozi wa Malaysia sijui Sisqo pia amechaguliwa kimshkaji mshkaji. :A S angry:
 
Pia orodha ya viti maalum ya ccm wapo akina vicky Kamata, na wengine. Nadhani cha muhimu hapa ni kwamba kila chama kilikuwa na vigezo vyake vya kuteua wabunge wa viti maalum, na walioteuliwa ni wale wenye sifa waliogombea, ndio maana ccm wamechomeka hata nyumba ndogo za muheshimiwa jk
 
Back
Top Bottom