Wazo la CHADEMA la kuwa na wabunge wawili kila jimbo si sahihi

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,015
12,288
Hili ni moja la wazo la kipuuzi kupata kulisikia toka kwa kiongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo.

"Aina za Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna aina kadhaa za Wabunge kwa mujibu wa Ibara ya 66(1)(a) na (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambapo ni kama ifuatavyo; Wabunge wa Majimbo, Wabunge wa Viti Maalum, Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwao, Mwanasheria Mkuu, Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais na Spika ikiwa hatachaguliwa miongoni mwa Wabunge, Tunapendekeza Ibara hiyo ifanyiwe marekebisho kwa kuzingatia yafuatayo:

Mapendekezo ya Chadema:

(i)Kuwe na wabunge wawili wa kuchaguliwa kwa kila Jimbo la uchaguzi, Mmoja Mwanaume na Mmoja mwanamke ambao kila mmoja atachaguliwa kwa kura zake kwenye kundi analogombea.
20240117_161937.jpg

Pia soma

1. Gharama zitazoongezeka endapo hoja ya CHADEMA kuongeza idadi ya wabunge itapita
2. CHADEMA yashambuliwa na kukosolewa kila kona mitaani kwa kupendekeza kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo
 
Yani mzigo tulionao uongezeke mara mbili. Na maraisi wawe wawili sasa. Hii nchi bana kila mtu anajari tumbo lake.
Tuwe tunasikiliza na kuelewa Mnyika alisema jimbo la uchaguzi iwe Wilaya na Wilaya zipo 133 pekee hivyo ni 133 x 2 = 266 pekee badala ya kuwa na wabunge 393 kama sasa, chukua 393 - 266 = 127, vilaza muwe mnaelewa
 
Nyote ni mbuzi mbuzi. Soma katiba ya warioba, alipendekeza hivyo lakini kwa kupunguza majimbo. Au sikiliza press ya leo ya Mnyika utapata jibu la thinking ya chadema
Muwe mnasoma, tatizo ni kuwa watanzania kusoma kwenu ni laana
 
Jimbo liwe halmashauri nyie mko dunia ya wapi msiojua yasioendelea na huku mnatumia JamiiForums
 
Tuwe tunasikiliza na kuelewa Mnyika alisema jimbo la uchaguzi iwe Wilaya na Wilaya zipo 133 pekee hivyo ni 133 x 2 = 266 pekee badala ya kuwa na wabunge 393 kama sasa, chukua 393 - 266 = 127, vilaza muwe mnaelewa
Kuwe na wabunge wakike na wakiume katika hilo jimbo kuweka mzani sawa ?
 
Tuwe tunasikiliza na kuelewa Mnyika alisema jimbo la uchaguzi iwe Wilaya na Wilaya zipo 133 pekee hivyo ni 133 x 2 = 266 pekee badala ya kuwa na wabunge 393 kama sasa, chukua 393 - 266 = 127, vilaza muwe mnaelewa
Hahaha! Wakikujibu niambie?

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Nyote ni mbuzi mbuzi. Soma katiba ya warioba, alipendekeza hivyo lakini kwa kupunguza majimbo. Au sikiliza press ya leo ya Mnyika utapata jibu la thinking ya chadema
Muwe mnasoma, tatizo ni kuwa watanzania kusoma kwenu ni laana
Hayo maneno yaliyo kolezwa sio ya Mnyika ?
 
..Mnyika ameshafafanua hoja hiyo.

..wewe mtoa mada na Makonda ndio wapuuzi

..hoja ya Chadema imeeleza jinsi idadi ya wabunge itakavyopungua.
Naomba nifafanulie hayo maneno yaliyo kolezwa ili mjinga na mpumbavu kati yetu ajulikane hapa
 
Tuwe tunasikiliza na kuelewa Mnyika alisema jimbo la uchaguzi iwe Wilaya na Wilaya zipo 133 pekee hivyo ni 133 x 2 = 266 pekee badala ya kuwa na wabunge 393 kama sasa, chukua 393 - 266 = 127, vilaza muwe mnaelewa

Watu hawaelewi vitu vidogo vidogo kama hivi halafu wako busy kutoa matusi. CCM wakiamua hivyo utasikia watu wanabadili midundo .... Hilo linawezekana kabisa although personally siiungi mkono hiyo system. Lakini hiyo system ni bora kuliko hii ya sasa ya upendeleo inayowaweka Covid 19 bungeni.

Waende hapo Namibia tu waone 50/50 ilivyo Bungeni.
 
Kabisa asee
 
Elewa mzee mambo ya jinsia hata Rwanda yapo hivyo hivyo achana na mfumo dume
Mataifa takataka hayana chochote cha maana cha kutufunza sisi na hata kama wazo hili la kipuuzi lingefanywa na mataifa makubwa bado lingeendelea kuwa la kishenzi.

Uongozi sio suala la kubalance mzani, mwenye uwezo anakuwa kiongozi sio upuuzi wa jinsia yake
 
Back
Top Bottom