Niliandika kwamba namfahamu Prof Mwandosya kwa kiasi fulani. Kwanza hakuna mtoto wake aliyesoma Afrika kusini, sasa labda ungesema alihongwa ticket ya kumpeleka mtoto wake Afrika kusini. Sasa hata kama Mwandosya angekuwa mtu wa hongo, asingekuwa mtu wa kumhonga tiketi ya mtoto wake kwenda Afrika kusini. Akili yake ni kubwa sana zaidi ya hongo ya ticket, au kuweza kuhatarisha hadhi yake ya waziri kwa hongo ya ticket ya ndege kwenda Afrika ya kusini, ambayo kwa sasa gharama yake ni kama Tshs 1M. Najua unafikiri kila mtu ni wa aina ya watu wa kuhongwa suti na vitu vidogo kama hivyo wakaingilika. Kama huna la kusema kaa kimya, maana kwa watu wengine upumbavu wao unakuwa dhahiri wanapofungua midomo.
Kutokana na unavyo shadadia hili jambo kuna mambo mawili yaliyo dhahiri, kwanza huenda hujui ulisemalo, pili huenda umependa hivyo chongo unaita kengeza.
Ukweli ni kwamba mtoto wa kike (sikumbuki jina lake) wa Mwandosya alihongwa scholarship ya kwenda kusoma South Africa, na kampuni ya simu lengo likiwa Mwandosya aipendelee hiyo kampuni kwenye tenda iliyokuwa imeomba serikalini, wakati huo Mwandosya akiwa waziri wa mawasiliano.
Pili Mwandosya mwenyewe alihongwa air ticket ya kwenda S. Africa na kulipiwa 3 nights stay in a five star hotel na same company alipokwenda kum-visit huyo binti yake. The reccord is there. Mimi sisemi binti huyo hakuwa na akili the question here ni kwamba alihongwa scholarship. Ingekuwa ni nchi za wenzetu hata huo uwaziri "unaomtafuna leo afya yake" asingekuwa nao. Eti hawezi kuhongwa air ticket atahatarisha uwaziri wake (poor reasoning) kama rais anaweza kuhongwa suits 5 tu itakuwa waziri, get real dude.
Ninakupa challange ndogo wewe unayemshadadia Mwandosya. Miaka yote ya Mwandosya tangu akiwa PS na baadaye waziri amewafanyia kitu gani watanzania cha kupigiwa mfano? Mention a single outstanding achievement of Prof. Mwandosya to this nation?
Sawa mimi mpumbavu sasa wewe mwerevu the ball is in your court, and the JF will be the judge!