Hatimaye Hamad Rashid, Shoka Hamis na wenzao wawili wafukuzwa CUF!

Hili ni tatizo la CCM.Kwa yeyote anakuwa CCM ama karibu na Chama hicho kama M. Seif basi hufikiri yupo juu ya sheria.Huu mfumo mbovu wa kutoheshimu mamlaka iliyoweka kisheria umeanzishwa na CCM kwa hiyo sioni ajabu M. Seif akitimiza/tekeleza ambayo ndugu zake CCM A wanafanya
 
kimenukaaaa! napita mtaani nikipiga mruzi mkono mfukoni.........................................! ndoa ya CCM na CUF,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!
 
ccm mfukuzeni JK mbona anawaaangushaaaa!,mbona wameweza CDM na NCCR Mageuzi wanawawakilishuin wachache kwenye nafasi za uwakilishi nyie mna wabunge na madfiwani wengi fukuzeni mwenyekiti hawezi kusimamia nidhamu ya chama,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Kwa upande wake, Shoka Khamis ambaye alikuwa Mbunge wa Micheweni, Kaskazini Pemba katika Bunge la Tisa, alisema kwa mujibu wa katiba ya CUF hamjui aliyemtuhumu kwani haiwezekani mtu asomewe shtaka bila kujua anayemtuhumu.

“Nimejifundisha mengi sana CUF mazuri na mabaya, lakini leo kwa sababu wamenifukuza ngoja niseme mabaya, CUF sisi ni CCM B kama wanavyosema wenzetu. Chama kina sifa mbaya ya kufukuza watu, lakini anayefukuza wenzake, Seif Sharif Hamad yeye anajiona kama mungu hafanyi makosa,” alisema Shoka.

Alisema hawapo tayari kujiunga na chama chochote cha siasa kama maneno yanavyosambazwa kuwa watahamia Chadema. Alisema watafufua Chama Cha Wananchi (CCW) ambacho kiliungana n Kamahuru na kuipata CUF.

“Tuna mpango wa kuanzisha chama kingine kwani CUF kwa sasa kimeshakuwa chama cha mtu ambaye ni Seif na siyo cha wananchi kama kinavyojulikana katika siasa za nchi hii,” alisema Shoka.

Hayo hapo juu ni maneno ya Shoka_________source Gazeti Mwananchi

Sizitaki mbichi hizi, sungura anagumia.
naona nafanya kazi, bila faida kujua.
yakamtoka machozi, sungura anagumia

maneno ya mkosaji.

Baada ya kukosa ubunge kule micheweni, na sasa kufukuzwa Chama, ndio anaamua kusema.

Pole sana ammi Shoka
 
Aende tu akapumzike! Kazi aliyotumwa imeshakamilika! Kasha wavuluga, CUF kuinuka tena ni ndoto za alinacha!
 
WanaJF: Kitendo cha Maalim Seif na kundi lake kupuuza amri ya Mahakama Kuu ya Tz kusitisha kikao cha baraza kuu la CUF si ukiukwaji wa sheria?

Mie nadhani ujeuri au uhuni huu wa Maalim seif unatoka kwa serikali ya CCM ambayo huwa ndiyo kawaida yake katika kutotii amri za mahakama zake. Kwa kuwa seif yumo katika serikali hiyo, basi anaona hakuna chochote kinachoweza kutokea kuhusu kutotii amri ya mahakama halali ya Tz.

Tulijadili suala hili na naomba tu-stick kwenye mada yenyewe.

Ndugu.

Ni vizuri kwanza kujua unachokiandika kabla kukurupuka na kuweka kitu kisichojulikanaLabda nikuulize suala kidogo.

1. Je ni nani aliyeweka pingamizi hilo?
2. Kama ni Hamad Rashid, mbona na yeye mwenyewe alihudhulia mpaka maamuzi yakatokea akiwemo ndani?
3. Je unaweza kutujuza ni jaji au hakimu gani alitoa maamuzi hayo ya kuzuia kikao hicho.

lakini mwisho tumehabarishwa kuwa kikao hicho kilifanyika Zanzibar? vipi amri ya kuzuia itoke mahakama kuu ya Tz badala ya mahakama kuu ya Znz. Kumbuka kuwa mahakama kuu ya Tz hukumu zake mwisho Chumbe. hazifiki Zanzibar. Zanzibar ni nchi yenye mamlaka kamili yaani kuna Serikali, Mahakama na Bunge lake (baraza la wawakilishi.
 
Nategemea maneno hayo hayo aliyoyasema Shoka leo, yatakuja kutoka mdomoni kwa Mtatiro very soon. Hata Shoka alikuwa anatupinga sana wakati ule tunasema CUF ni CCM B kama anavyofanya Mtatiro sasa. Kama anabisha aingie Anga za Maalim Seif uone.
 
Duh! Je, kumbe na mtizamo tofauti na mwenyekiti au katibu mkuu wa chama ni UHAINI? nilikuwa sifahamu kwamba demokrasia ya kuchagua unachoamini ni kosa.

Pamoja na yooote alotenda hamad rashid siamini kufukuzana ndo ujenzi wa demokrasia. Kuvumiliana pia ni muhimu wanabodi ni ni njia nyingine ya kudu
 
Ndugu.

Ni vizuri kwanza kujua unachokiandika kabla kukurupuka na kuweka kitu kisichojulikanaLabda nikuulize suala kidogo.

1. Je ni nani aliyeweka pingamizi hilo?
2. Kama ni Hamad Rashid, mbona na yeye mwenyewe alihudhulia mpaka maamuzi yakatokea akiwemo ndani?
3. Je unaweza kutujuza ni jaji au hakimu gani alitoa maamuzi hayo ya kuzuia kikao hicho.

lakini mwisho tumehabarishwa kuwa kikao hicho kilifanyika Zanzibar? vipi amri ya kuzuia itoke mahakama kuu ya Tz badala ya mahakama kuu ya Znz. Kumbuka kuwa mahakama kuu ya Tz hukumu zake mwisho Chumbe. hazifiki Zanzibar. Zanzibar ni nchi yenye mamlaka kamili yaani kuna Serikali, Mahakama na Bunge lake (baraza la wawakilishi.
Barubaru tupo pamoja kasoro kwenye red,

Ilikuwaje HR akahudhuria kikao alichokipinga mahakamani? kama si ujanja ni nini.
Halafu sielewi kama hakimu aliyetoa hati ana akili timamu, kikao tayari kimeshaanza na mlalamikaji yumo kikaoni tumeelezwa hati ilifika saa 8 sasa hiyo hati itahusu pia zile ajenda za asubuhi na maamuzi yake?, comfused.com.
 
Soma katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010. kifungu cha kwanza kabisa ibara ya kwanza kimeweka wazi kuwa Zanzibar ni Nchi.

Na kumbuka siku zote ili inchi iwe nchi inahitajika kuwa na mihimili mikuu mitatu.
1. Serikali (chini ya Rais na mawaziri wake). zanzibar kuna rais na mawaziri wake na vitendea kazi vyao
2. Chombo cha kutunga sheria. zanzibar kuna baraza la wawakilishi.
3. Chombo cha kutafsiri sheria. zanzibar kuna mahakama inayoongozwa na Jaji mkuu Zanzibar.

Ndugu.

Ni vizuri kwanza kujua unachokiandika kabla kukurupuka na kuweka kitu kisichojulikanaLabda nikuulize suala kidogo.

1. Je ni nani aliyeweka pingamizi hilo?
2. Kama ni Hamad Rashid, mbona na yeye mwenyewe alihudhulia mpaka maamuzi yakatokea akiwemo ndani?
3. Je unaweza kutujuza ni jaji au hakimu gani alitoa maamuzi hayo ya kuzuia kikao hicho.

lakini mwisho tumehabarishwa kuwa kikao hicho kilifanyika Zanzibar? vipi amri ya kuzuia itoke mahakama kuu ya Tz badala ya mahakama kuu ya Znz. Kumbuka kuwa mahakama kuu ya Tz hukumu zake mwisho Chumbe. hazifiki Zanzibar. Zanzibar ni nchi yenye mamlaka kamili yaani kuna Serikali, Mahakama na Bunge lake (baraza la wawakilishi.

Unakijua kweli unachokisema au unabahatisha tu? CUF kama chanma cha kisiasa kiliandikishwa chini ya sheria gani -- ya Zenj au ya Bara (yaanu ya Muungano)?

Suala la Hamadi kuwepo katika kikao hicho hakina tija hapa, suala kuu ni jee -- amri ya kusitisha kikao ilitolewa au haikutolewa na Mahakama?

Kama mahakama kuu ya TZ haina mamlaka huko Zenj, basi ni sharti Seif na genge lake waende mahakamani kuipinga amri hiyo.

Labda kuna wanaJF wanaweza kuchanguia suala hili kiukamilifu, sio kiushabiki.
 
Feedback na Barubaru mmenena -ni vema pia kuwa na details za zuio- je, ni la kikao au maamuzi kumhusu HR au yote? nina maana kama ilizuia kikao kuchukua maamuzi juu ya HR then kinaweza kuaendelea na pia HR alikuwa sahihi kuhudhuria(Mtizamo wangu ni wa akili ya kawaida tu)
 
Back
Top Bottom