Hatimaye Hamad Rashid, Shoka Hamis na wenzao wawili wafukuzwa CUF!

seif sharifu ataki kupunguziwa madaraka uku katibu mkuu uku waziri kiongozi,anatumia muda mwingi serikalini atumikii chama sasa wadau wanaona bora wampe HR ukatibu mkuu afanye kazi za chama, Seif akaona ulaji unaondoka kwaiyo njia saihi ni kumpiga chini HR kusudi aendelee kula neema.
 
ata hivyo awa jamaa CUF awajawai kuchagua tena viongozi,kwani wakina seif wanamdaa mrefu madarakani.
 
Mimi nalia na MSAJILI wa vyama vya SIASA Mh saana Tendwa. Hawezi kuwa pale kusajili tu kwa kutumia idadi ya WANACHAMA ambao baadae wakifukuzwa hana la kufanya hata kama makosa yenyewe ni ya kugusa sharubu za mkubwa mmoja tu.
 
Unakijua kweli unachokisema au unabahatisha tu? CUF kama chanma cha kisiasa kiliandikishwa chini ya sheria gani -- ya Zenj au ya Bara (yaanu ya Muungano)?

Suala la Hamadi kuwepo katika kikao hicho hakina tija hapa, suala kuu ni jee -- amri ya kusitisha kikao ilitolewa au haikutolewa na Mahakama?

Kama mahakama kuu ya TZ haina mamlaka huko Zenj, basi ni sharti Seif na genge lake waende mahakamani kuipinga amri hiyo.

Labda kuna wanaJF wanaweza kuchanguia suala hili kiukamilifu, sio kiushabiki.

Mkuu pamoja sana! Hapo kwenye red; hebu atueleze Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa ambayo hasa ndiyo iliyoisajili CUF ni ya (nchi ya) Zanzibar au ya JMT? Kwa ufupi CUF ilisajiliwa kwa sheria ipi?

Pili, hiyo sheria na Ofisi ya Msajili iliyosajili CUF imetokana na Katiba ipi? Ya (nchi ya) Zanzibar au JMT?

Tatu, hivi Katiba ya JMT na ile ya (nchi ya) Zanzibar ni ipi iko superior?

Nne, kwa muono wa maswali yaliyotangulia, ni Mahakama ipi yenye mamlaka juu ya masuala yahusuyo vyama vya siasa? Ya Zanzibar au ya JMT?

Mimi nadhani kwa mwendo na mkanganyiko huu hata kwa masuala mazito kama ya Katiba na Mahakama kuna haja ya kuvunjilia mbali muundo wa muungano tulio nao. Tundu Lissu is hero.
 
Sizitaki mbichi hizi, sungura anagumia.
naona nafanya kazi, bila faida kujua.
yakamtoka machozi, sungura anagumia

maneno ya mkosaji.

Baada ya kukosa ubunge kule micheweni, na sasa kufukuzwa Chama, ndio anaamua kusema.

Pole sana ammi Shoka
Bila shaka unawafahamu vizuri Maalim na Jusa. Bila shaka pia unafahamu hii safishasafisha ni ya nini hasa na kwa nini sasa na sio tangu wakati ule. Wewe sio mchoyo. Tumegee kidogo maana wenye CUF yao sio hawa wanaokimbizana hapa.
 
Mkuu pamoja sana! Hapo kwenye red; hebu atueleze Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa ambayo hasa ndiyo iliyoisajili CUF ni ya (nchi ya) Zanzibar au ya JMT? Kwa ufupi CUF ilisajiliwa kwa sheria ipi?

Pili, hiyo sheria na Ofisi ya Msajili iliyosajili CUF imetokana na Katiba ipi? Ya (nchi ya) Zanzibar au JMT?

Tatu, hivi Katiba ya JMT na ile ya (nchi ya) Zanzibar ni ipi iko superior?

Nne, kwa muono wa maswali yaliyotangulia, ni Mahakama ipi yenye mamlaka juu ya masuala yahusuyo vyama vya siasa? Ya Zanzibar au ya JMT?

Mimi nadhani kwa mwendo na mkanganyiko huu hata kwa masuala mazito kama ya Katiba na Mahakama kuna haja ya kuvunjilia mbali muundo wa muungano tulio nao.
Tundu Lissu is hero.

Kwa mikanganyiko kama hii Tundu Lissu alishayaona yote...........!
 
Niliwahi kuandika Makala yangu katika gazeti la Tanzania Daima la tarehe 21 november 2010 toleo namba 2179 juu ya ndugu yetu Maalim Seif Sharifu Hamad yaliyokuwa na kichwa cha Habari Maalim Seif mbona Umesahau??

Kwa wale waliosoma makala hayo japo sio mtaalamu sana wa kuandika katika magazeti lakini watu wenye busara walielewa nilichokuwa namaanisha wapo walionipongeza wengine wakanitumia SMS kupitia Simu yangu ya mkononi yenye namba 0787974883 wakiungana na mawazo yangu ambayo moja kwa moja nilitumia haki yangu ya kikatiba kutoa mawazo yangu kupitia chombo cha wananchi yaani gazeti la Tanzania Daima.

Lakini pia wapo walioniona mimi sielewi kitu juu ya Maalim Seif sasa napenda niwakumbushe tena kile nilichokuwa ninamaanisha juu ya huyo Kiongozi Mkuu wa chama cha wananchi CUF kujisahau na yale yaliyotokea kule visiwani ndugu zetu walipoteza maisha wakipinga vitendo vibaya walivyokuwa wakifanyiwa na watawala ambao hadi leo wapo madarakani nadhani hawapendi kamwe kuona wakiongozwa na chama kingine zaidi ya chama cha Mapinduzi kwa nukuu ya rais mstaafu B.Mkapa wakati wa kampein pale Jangwani mwaka 2010 nanukuu chama ambacho kinapaswa kuongoza si kingine bali CCM tu.

Leo hii Sharif Hamad anawaonngoza viongozi wenzake Kuwafukuza viongozi wenzake aliopata nao taabu hadi kuundwa serikali ya Umoja wa kitaifa kwa vile yeye yupo Ikulu na Kiyoyozi kinampepea mwenzetu kasahau hayo niliyatabiri mwaka mmoja na nusu uliopita, amesahau walivyopata taabu wote kwa kupigwa mabomu ya machozi na mapolisi na baadhi ya ndugu zetu kupoteza maisha wengine kuwa wakimbizi katika nchi yao.

Huku sio lazima utumwe na wanaokuongoza isipokuwa ni kutumia busara mambo mengine ukayapinga. Ukweli unabaki palepale Maalim Seif Sharifu Hamad ameisha jisahau alikotoka ndiyo maana akatoa baraka za kufukuzwa uanachama kwa wenzake akina Hamad Rashid Mohamed Mb,wa jimbo la Wawi.

Anatory Mujwahuzia.
 
Unakijua kweli unachokisema au unabahatisha tu? CUF kama chanma cha kisiasa kiliandikishwa chini ya sheria gani -- ya Zenj au ya Bara (yaanu ya Muungano)?

Suala la Hamadi kuwepo katika kikao hicho hakina tija hapa, suala kuu ni jee -- amri ya kusitisha kikao ilitolewa au haikutolewa na Mahakama?

Kama mahakama kuu ya TZ haina mamlaka huko Zenj, basi ni sharti Seif na genge lake waende mahakamani kuipinga amri hiyo.

Labda kuna wanaJF wanaweza kuchanguia suala hili kiukamilifu, sio kiushabiki.

Counterpunch,

Ni vizuri kwanza nikujuze sheria za nchi yako kidogo.

Kama nilivyobainisha hapo awali kuwa Zanzibar ni nchi na ina mamlaka kamili katika eneo lake. Ndanimwe kuna mahakama na baraza la kutunga sheria (baraza la wawakilishi)

Kumbuka kuwa sheria yoyote kipitishwa na Bunge la Muungano haiwezi kuweza kufanya kazi Zanzibar mpaka iridhiwe na baraza la wawakilishi la Zanzibar ndio itaweza kutumika kwenye maeneo na viunga vya Zanzibar. Kinyume cha hapo itakuwa batili.

Kuhusu sheria za kuanzishwa kwa Afisi ya msajili wa vyama vya siasa tanzania imeridhiwa na baraza la wawakilishi na hivyo vyama hivyo kuweza kuvuka mipaka mpaka Zanzibar. na nafikiri hata mfumo wake unauona. Ni lazima msajili akitoka upande mmoja na makamo wake lazima atoke upande wa pili wa muungano wenu.

Kwa mantiki hiyo vyama hivyo vinatumia sheria za pale zilipo ima Znz au Tanganyika. Kwa Mfano CUF wamefanya mkutano wao Znz basi huko watatumia sheria za Zanzibar na sio za Muungano yaani za Bara.

Kumbuka kuwa katika mfumo wenu wa Mahakama. Umeunganishwa katika mahakama ya Rufaa na sio mahakama za chini.

Hiyo ni kifupi sana kuhusu mfumo wenu wa kimahakama na vyama vya siasa.

Soma kidogo sheria zenu kabla kuandika.
 
Huu mfumo wa kikatiba wa vyama hautufai nchi hii. Vyama vya siasa vimegeuka kuwa vichaka vya madikteta ambao wanajipambanua kama wana demokrasia. Kimsingi wanapinga kitu kilekile wanachokifanya ndani ya vyama vyao. Ni wakati muafaka sasa kwa wabunge kuwa wawakilishi wa wananchi na sio wa vyama hivi vya siasa vinavyoongozwa na magenge ya madikteta wasiotaka kupingwa wala kusahihishwa.

Inapotokea mbunge akatofautiana na chama na kuvuliwa uanachama ni vyema akabaki kuwa mwakilishi huru wa wananchi asiyefungamana na chama chochote. Hatutaki huu utaratibu wa sasa ambao tunashirikishwa wote kuwachagua wawakilishi kwa kura na kodi zetu halafu kikundi kidogo tu cha watu kinakuwa na mamlaka ya kuwaondoa wawakilishi hao bila ya kutushirikisha.

Na kwa uzoefu mdogo tu nilioupata hivi vyama vinavyojipambabua kuwa vya upinzani ni madikteta wabaya dhidi ya wananchama wao kuliko hata chama tawala ambacho wanatushawishi kila siku tukiondoe madarakani kwa kuwa ni chama cha kidikteta.
 
Niliwahi kuandika Makala yangu katika gazeti la Tanzania Daima la tarehe 21 november 2010 toleo namba 2179 juu ya ndugu yetu Maalim Seif Sharifu Hamad yaliyokuwa na kichwa cha Habari Maalim Seif mbona Umesahau??

Kwa wale waliosoma makala hayo japo sio mtaalamu sana wa kuandika katika magazeti lakini watu wenye busara walielewa nilichokuwa namaanisha wapo walionipongeza wengine wakanitumia SMS kupitia Simu yangu ya mkononi yenye namba 0787974883 wakiungana na mawazo yangu ambayo moja kwa moja nilitumia haki yangu ya kikatiba kutoa mawazo yangu kupitia chombo cha wananchi yaani gazeti la Tanzania Daima.

Lakini pia wapo walioniona mimi sielewi kitu juu ya Maalim Seif sasa napenda niwakumbushe tena kile nilichokuwa ninamaanisha juu ya huyo Kiongozi Mkuu wa chama cha wananchi CUF kujisahau na yale yaliyotokea kule visiwani ndugu zetu walipoteza maisha wakipinga vitendo vibaya walivyokuwa wakifanyiwa na watawala ambao hadi leo wapo madarakani nadhani hawapendi kamwe kuona wakiongozwa na chama kingine zaidi ya chama cha Mapinduzi kwa nukuu ya rais mstaafu B.Mkapa wakati wa kampein pale Jangwani mwaka 2010 nanukuu chama ambacho kinapaswa kuongoza si kingine bali CCM tu.

Leo hii Sharif Hamad anawaonngoza viongozi wenzake Kuwafukuza viongozi wenzake aliopata nao taabu hadi kuundwa serikali ya Umoja wa kitaifa kwa vile yeye yupo Ikulu na Kiyoyozi kinampepea mwenzetu kasahau hayo niliyatabiri mwaka mmoja na nusu uliopita, amesahau walivyopata taabu wote kwa kupigwa mabomu ya machozi na mapolisi na baadhi ya ndugu zetu kupoteza maisha wengine kuwa wakimbizi katika nchi yao.

Huku sio lazima utumwe na wanaokuongoza isipokuwa ni kutumia busara mambo mengine ukayapinga. Ukweli unabaki palepale Maalim Seif Sharifu Hamad ameisha jisahau alikotoka ndiyo maana akatoa baraka za kufukuzwa uanachama kwa wenzake akina Hamad Rashid Mohamed Mb,wa jimbo la Wawi.

Mujwahuzi.

Mimi sijabahatika kuisoma article yako. Lakini kwa kile kichache ulichoandika hapa inajionyesha wazi wewe huijui Zanzibar bali umejikita na habari zinazoandikwa katika magazeti yenu.

Naomba nikujuze kitu. Kwa mtu makini huko Tanzania. napenda kukufahamisha kuwa hakuna maadili yanayofuatwa katika uandishi wa habari zenu. Wengi wa wahariri wa magazeti yenu ni wafanya biashara wanaandika habari kibiashara zaidi na kusahau miiko ya uandishi.

wengi wametanguliza mbele fedha na sio uzalendo. wamekuwa wachochezi na sio wapatanishi. mfano kama hamad rashid ametoka nje ya kikao na kuongea na waandishi wa habari suala la kwanza kwa mwandishi makini ni kumuuliza kikao kile hakikuwa na minutes au katibu au msemaji. Kwanini yeye aongee pekee yake au yeye ndio msemaji wa kikao kile. Kuchukua maneno yake pekee ni kosa na siku zote waswahili husema msema pweke ushinda. kiandishi hiyo inaitwa uchonganishi. Kwani kila chama kina taratibu zake na kanuni zake na sio kila mtu anaweza kuzungumza.

Lakini pia wanaoijua Znz na sirka na desturi za kule tunaweza kukwambia Maalim Seif ni Hero kwani siku zote amekuwa mwenye kuitakia mema Znz na waZnz. Uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni ushindi sio tu kwa Znz bali pia kwa Waznz.

Jaribu kufuatilia maendeleo ya Znz tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na maendeo yaliyopatikana kwa kipindi hichi kifupi cha Umoja wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Utaona wazi znz kwa sasa inaendelea kwa kasi sana sio tu kisiasa bali pia kiuchumi na nyanja zote za maendeleo. hata ukiongea na wengi wanazungumzia maendeleo na sio malumbano.

Kumbuka mwandishi makini anazungumzia maendeleo kiuchumi na sio kimigogoro.

nakupa pole. isome vizuri Znz utaijua.

hata useme nini hamad ana nguvu na ushawishi mkubwa sana kwa sasa ktk siasa za tanzania.
 
"MS alikuwepo Zanzibar. kama Mwandishi wa habari, akishuhudia Hamad Rashid akifurushwa"
Jana Jioni nilikuwa Jos kona Ngome kuu ya Cuf iliopo Soko Muhogo Baada Ali Salehe kuripoti kupitia BBC, washabiki wa CUF
walipiga mayoe kwa furaha, yaani ukiwahoji ni wazi wamemchoka Hamad Rashid.
Saa 1:00 jioni. Mtaa wa Mtendeni, makao makuu ya CUF. cuf haikuzaliwa Arusha. moshi, Tabora. Imezaliwa Malindi na kama kufa itafia malindi, hamad Rashid ziiiiiiiiiii

Saa 2:30 usiku nilipofika maskani ya CUF Jangombe gengeni, mazungumzo Hamad Rashid kesha, akachume karafuu Pemba. hali ni shwari.
Saa 3:00 Usiku. Ngome nyengine ya CUF Jangombe kwa maharuki anapotoka mmoja wa vijana waliofukuzwa yaani Saanani. maneno ni hayo hayo. Aende tu Chadema. acheze na Ndevu za Seif asicheze na akili ya Seif(Maalim seif)
Leo saa2:00 asubuhi. daraja bovu,Ofisi ndogo ya CUF . Hamad rashidi ni m-mboya tu, akatafute Ubunge Moshi. hapa nooo.

Magomeni ngome ya CUF:matangazo yao" Hamad rashid kavuna alichopanda. aanzishe chama Chake, yeye na familia yake"

Vituo vya Magazeti.
Yakheeeeee, kakie hamad umemsikia? eti anataka kuwa mbunge wa Mahakama. kanchoka tena.

Ahsantum kwa taarifa.

Hakika alipewa kamba ya kutosha sana ili ajimalize mwenyewe. Na sasa amejimaliza.

Kumbuka kuwa kuna wengi walitimuliwa kuanzia Mapalala, Naila Jidawi na akina Msabaha. Na wote sasa mnawaona wakoje na wanaishi vipi na hishma yao kwa jamii hususan ya kizanzibari ikoje?

Namsikitikia sana Mh Hamad rashid na kumpa pole, choyo na kiu ya madaraka imemponza.

Hivi MS ni mwandishi wa habari??
hizo habari unazoleta na kuziandika zina typing error kibao wanaosoma habari zako wana roho ya Paka...
 
Back
Top Bottom