Uchaguzi 2020 Hasna Mwilima hafai kupeperusha Bendera ya CCM Kigoma Kusini

Last Seen

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
223
549
Habari wana Jukwaa.

Nimefurahi kuona kwa kiasi kikubwa wajumbe wa baadhi ya maeneo kuwachinjia mbali vigogo na watia nia wenye majina na ushawishi mkubwa, Kwa Kigoma Kusini hali imekuwa tofauti Sana kwani mtia Nia asiyekubalika na asilimia kubwa ya wananchi jimboni ndio kapitishwa na wajumbe.

Mtia Nia huyu asiyelikumbuka Jimbo Mara baada ya kuchaguliwa, amekosa mvuto na Ushawishi kwa wananchi wa Jimbo la Kigoma Kusini ,Mwaka 2019 alishawahi kuzomewa mbele ya PM.

Kwanini amechokwa?

1/Tangu achaguliwe 2015-2020 amefika jimboni sio zaidi ya Mara 4.
Mara ya Mwisho alifika waziri mkuu alipokuwa na ziara jimboni.

2/ Amekuwa Hana kauli nzuri kwa Wananchi, akiombwa kuja kusikiliza kero za wananchi.

3/Kutokamilisha Miradi ya Maendeleo.

4/ Kauli za majigambo na kejeli kwa Wananchi wake.

5/ Hasikiki akitoa kero za Jimbo, Jimbo Lina kero na changamoto nyingi.

Akipitishwa Hasna Mwilima Wana Kigoma Kusini watakuwa na maumivu mengine ya miaka mitano. Chonde Chonde member wa Kamati kuu yoyote Alieko JF alifikishe hili.
 
Ndio maana huko Umasikini umejaa Barabara mbovu ... Watu wa huko kasulu , kibondo na kakonko sijui vichwa vyenu vina Nin ... Hivi Hakuna watu wenye uwezo huko CCM mpaka muendelee kuwapa nafasi hao watu wenye uwezo mdogo.
Mkuu wapi ndani ya nchi hii waliwapa uongozi watu wenye uwezo mkubwa?. Kama mtu kama Kimei anapigwa chini Kura za maoni unategemea wapi watakapochagua mtu bora hasa ndani ya CCM.
 
Akuna mgombea yeyote aliepita watu wote wakaridhika. Hii ndio siasa. Hasna angepigwa chini kuna watu pia wangelalama.
 
HATA BONA KALUA/KAMORI SEGEREA HAFAIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
Mkuu wapi ndani ya nchi hii waliwapa uongozi watu wenye uwezo mkubwa?. Kama mtu kama Kimei anapigwa chini Kura za maoni unategemea wapi watakapochagua mtu bora hasa ndani ya CCM.
Vigezo vipi umetumia kusema kimei Ni Kiongozi mzuri ?

Huyo kimei taja Mambo aliyosaidia huko kwao kipndi ana nafasi crdb !! ... Naomba uyataje hapa maana nimefika wilaya zote za mkoa wa kilimajaro. Au bado unadhani uongozi Ni elimu kubwa kama Mwakyembe wakati kwao kyela Hakuna alichofanya.

Uongozi Bora ni kufanikisha mahitaji ya wananchi wako serikalin bila kujali elimu yako. Kwa ujinga wa watu wa huko kigoma kusini angegombea kimei wangemchangua. Hujiulizi kwa nini Mwakyembe amekatwa huko kwao kyela ?
 
Nimekuuliza niwapi hapa Tz walichagua mbunge anaejielewa hasa kutoka ndani ya CCM?. Jimbo la Kigoma kusini nimefika mara nyingi na napafaham vizuri nimoja ya jimbo linalojitahidi kubadilisha wabunge kadri wa wezavyo na hakuna mbunge alielitumikia hilo jimbo vipindi viwili vinavyofuatana.

1995-2000(Msambia)
2000-2005(Kifu)
2005-2010(Msambia)
2010-2015 (Kafulila)
2015-2020 (Husna)

Kwa mlolongo huo unasemaje hawajitambui kama wananchi wanabadili mbunge kila baada ya miaka mitano?. Nahapo kuna wabunge wawili kutoka NCCR MAGEUZI ingawa wote kwa sasa walishahamia ccm ,kama uchaguzi ukiwa huru na haki nakama huyo Husna hakufanya Jambo la maana basi watampiga chini. Hilo jimbo nalifahamu vizuri maana ndio kwao ni bimkubwa.
 
Kwanini mteseke wakati wapo vijana wazaliwa wa Kigoma Kusini wanaogombea kupitia vyama vya upinzani?
Ndio faida ya kuwa na vyama mbadala,Chama chenye mgombea bora ndicho kipewe kura,na chama chenye mgombea wa hovyo kiadhibiwe ili ikawe fundisho.
 
Back
Top Bottom