Bilioni 11.6 Kujenga Chuo cha TIA Mkoa wa Kigoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

MBUNGE ASSA MAKANIKA AMESEMA SERIKALI IMEPELEKA SHILINGI BILIONI 11.6 KUJENGA CHUO CHA TIA MKOA WA KIGOMA

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Assa Makanika ameendelea na ziara yake katika maeneo ya Kidahwe, Mungonya na Ziwani kufuatilia shughuli za maendeleo, kuonana na Makundi na kuzungumza na wananchi.

"Katika mchanganuo wa maendeleo ya haraka haraka nimewaambia fedha nyingi zimeingia. Nimezungumza na Mwenyekiti, DMO, nilileta fedha Shule ya Sekondari Msimba Day Shilingi Milioni 4,100,000 ili kuona namna gani kuiwezesha Shule lakini wananchi hawakufahamishwa" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Mheshimiwa Mbunge sisi wajumbe wa Serikali ya Kijiji tunaishi kwaajili ya uzoefu wetu kama ni kukata tamaa tungekuwa tumeshaachia Kijiji kulingana na changamoto tulizonazo. Shilingi Milioni 140 zilivyoingia Wananchi hawajui na Shule ilivyojengwa ikajengwa chini ya kiwango. Tunakuomba siku moja uje tukaikague hiyo Shule" - Mjumbe wa Serikali ya Kijiji Kata ya Mungonya.

"Mimi nimekwenda Dodoma nimeomba fedha kwa Mheshimiwa Rais kupitia Mawaziri wake nimeleta huku jimboni, mara nyingi nipo Dodoma kung'ang'ania tugawake ile keki na kuwaletea ninyi watekelezaji inabidi mtekeleze kwa usahihi, msipotekeleza kwa usahihi mkanidanganya ipo siku nitakuja kuwauliza, leo nimekuja hapa wananiambia mmjenga Shule chini ya kiwango" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Kaimu Mkurugenzi, mwambie Mkurugenzi amchukue Mhandisi akae na Serikali ya Kijiji na Vyombo vya TAKUKURU waangalie uthabiti wa miradi hii ili kama kuna ubadhirifu ambao wananchi mmeuona Vyombo hivi vitazame. Mwandiga hapa Mungonya inahitaji uwepo wangu wa Mara kwa mara, nitapanga muda nije kuangalia miradi inaendeleaje" - Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Watu wa Mungonya mimi nimesomeshwa na wazazi ninyi wenyewe, nimeingia kuwa Mbunge na nimejiwekea utaratibu nikasema nataka nianzishe Sekondari Nane (08) katika muda wangu wa miaka mitano (05), nilisema Msimba Day lazima niipiganie badala ya mtoto kwenda kusomea Ruiche aweze kusomea hapa" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Nilimuomba Makamu wa Rais kwamba mimi kule nitafanya nini nisipofanya mabadiliko! Akanipa Shule mbili za kisasa, moja imekamilika ipo Kata ya Ziwani Shule ya Shilingi Milioni 470 imekamilika na kuwekewa Kompyuta. Tunataka watoto wasiwe wanaenda Nyarubanda tu, wengine waende Shule ya Sekondari Ziwani" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Tarehe 03 Julai, 2023 tumesaini Shilingi Milioni 470 zinaenda kujenga Shule ya Sekondari Kata ya Nkungwe. Chuo cha Uhasibu kinajengwa hapa Kigoma, Chuo cha TIA na Shilingi Bilioni 11.6 zimeshaletwa. Tumeshawaambia Wataalam wanaojenga fedha inayoletwa ibaki kwa watu wa Mungonya, vijana waajiriwe wa hapa Mungonya" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini.


WhatsApp Image 2023-07-08 at 11.02.05(1).jpeg
 
Kuanzia sasa tuchague viongozi ambao kwao ni duni ili nao waendeleza nyumbani
Yaani mpaka uwe na cheo ndio kwenu kutajengwa

Africa shida sana
 
Back
Top Bottom