Mungu tu ndiye asikie kilio cha watanzania zaidi ya milioni40
Serikali ya Tanzania ni dhahiri sasa ni namba moja duniani kwa wizi wa mali za umma.Umaskini wetu tulio nao watanzania ni kwa sababu ya Rais dhaifu na ambaye hana huruma na umaskini wa wananchi wake. Mungu ametupa utajiri wa asili lakini kinachopatikana kinaliwa na mchwa wa serikali ya ccm.
Rais, MP, Mawaziri hadi mtendaji wa kijiji wa ccm ni wezi na hawawezi kukamatana kwakuwa wizi ndiyo jadi ya chama ccm. Lakini wakumbuke kwamba CHAKULA KIPATIKANACHO KWA UDANGANYIFU NI KITAMU LAKINI MWISHO WAKE HUWA KAMA MCHANGA KINYWANI.
SIKU IKIFIKA KILA MTU ATATOA HESABU YA KAZI HAKUNA KUKWEPA.
Enyi watawala wa Tanzania ni nani aliyewaroga?Muone aibu na mchukue hatua
Kweli ndugu, Mungu ndie pekee anaweza kutusaidia.
hahaha kweli ndugu yangu nchi yetu rushwa ni kila kona.Tatizo la Viongozi wanaona mifano kama ya singapore lakini hawawezi kuchukua hatua kwa sababu wapo madarakani kwa manufaa yao binafsi.....Ndugu yangu umesahau jambo moja kubwa,nalo ni RUSHWA.Ah Serikali yetu imebarikiwa kwa rushwa,mimi simjui nani aliyetoa msamiati huu usemao RUSHWA NI ADUI WA HAKI,kwa hakika amesema kweli,yaani Nchi hii sasa huwezi kufanya lolote mpaka utoe Rushwa,si Polisi,Mahakamani,Hospitali.sasa vipi watakamatana wakati wenyewe ndio hao hao wanaochukua rushwa then mwisho wake wanamalizia na WIZI?Kweli Nchi hii sio maskini lakini serikali yetu ndio inayochangia sisi wanyonge kuzidi kua maskini.Hivi hawa viongozi wetu hawachukui mfano wa Nchi ya Singapore?Wenzetu wamepiga hatua kubwa kimaendeleo kwa sababu ya kukomesha RUSHWA NA WIZI SERIKALINI.
Kwanza nampa heko Zito kwa kazi kubwa; haijalishi kitakachofuata, amediriki na hii ndio njia ya Ukombozi wa kweli mbele ya macho hali mkitazamana mnapeana ukweli.
Plan B: Kwa kuwa hatua hiyo inapotezewa na PM na wahusika wengine, ni wakati wa Wananchi kuzungumza, hapa hatuna kanuni wala sheria wala mipaka ya muda, kwetu tuna jambo moja kubwa. Ni wenye nchi, waumiaji na tunaopaswa kuchukua maamuzi mazito.
1. Napendekeza ziwepo 'forms' katika kila Wilaya, ama Kata ambazo zitakusanya sahihi za Wananchi waliokata tamaa na Serikali iliyoko madarakani.--Itahitaji kuwa na wasimamizi, hapa nahitaji ushauri. Fomu hizo zikusanye majina halisi, simu na sahihi za kutaka mabadiliko. Fomu hizi ziratibiwe na kamati hiyo hiyo iliyokwisha anza zoezi la kushughulika na Waziri Mkuu na Mawaziri wengine.
2. Fomu hizi zipelekwe Bungeni ikiwa ni Sauti ya Wananchi pasipo kujali vizuizi.
3. Bunge liruhusu ajenda ya kutokuwa na Imani si na baadhi ya mawaziri bali Serikali nzima
4. Wananchi wajipange kwa hatua ya 'Civil Disobedience' hadi pale mambo yatakapobadilika.
Mfumo wa civil disobedience ndio uliotumika na akina Martin Luther King hadi wakapata haki yao. Kwetu tuutumie kushinikiza mambo ambayo tunaona siasa zinaendelea kuyapuuza hali tunaumia na wao wakiongeza posho. Nia ya Civil Disobedience iwe ni total palalysis ya nchi, hadi haki ipatikane.
SIO WAKATI WA KULALAMA NI WAKATI WA KUTENDA, INAWEZEKANA TUSIMAME PAMOJA KUDAI HAKI ZETU.
We Shall Overcome, Deep in My heart I do believe we shall Overcome so soon
Nawakilisha.