mbogo31
JF-Expert Member
- Nov 28, 2008
- 711
- 173
Mkuu Mbogo31 kwa taarifa tu ni kwamba hata Polisi wetu sasa wamechoka na kiukweli hawaishi kwa kutegemea mishahara ila wanaishi kwa kuchukua rushwa kila siku. Nani asiyejua sasa kwamba Polisi hawawezi tena kumudu maisha bial rushwa? Hawafanyi hivyo kwasababu wanapenda, wanazidiwa. Siwatetei lakini ninachojaribu kuonyesha ni kwamba tukifanya jambo hapa na ikakolea sawasawa Polisi wetu kuhamia upande wa wananchi ni rahisi sana. Kwanza wengi husema ninyi fanyeni, sisi tunavua uniform tunawaunga mkono. Wako na sisi tufanye kazi inayotakiwa, la msingi ni mpango kamili.
Nakubaliana na wewe kabisa, mimi pia nimesha wahi kuongea na wanajeshi hawa JWTZ wao wanasema wanatii madaraka yaliyowekwa na wananchi na watatii maamuzi ya wananchi ya kuwaondoa madarakani hao walio waweka na sio wao kupindua, sasa kinachosubiriwa ni sisi wanachi kuikataa serikali na wao wakiona kweli tunadhamira ya kweli watatulinda, sasa swali tuanaza vipi? maana kwa kweli mtu unaefikiri sawasawa huwezi kuvumilia huu uoza unaoendelea ndani ya serikali labda uwe kichaa. nihatari sana na ni janga kubwa sana kwa kizazi chetu, yaani fikiria huduma za kijamii zote hovyo halafu mawaziri wanatafuna pesa ya umma, ma rc, ma dc wakurugenzi, makatibu, wahasibu wa ngazi zote serikalini? ni pesa ngapi inafujwa ambayo ingeboresha maisha ya mtanzania?