Hasira hazijatosha, haiwezekani JK adharau na sisi tukae kimya..!

Inaumiza na kukera unapoona watu wachache wanapo lindana na kufisadi mali zetu nakujigamba hawezi wajibika!nimechoshwa na uhairishwaji wa bunge uliofanywa kisanii kamavile hakuna jipya lilo zungumzwa juu ya mafisadi wanaotufanya tuishi maisha haya,sasa niwakati mwafaka wakuamua sisi kama walalahoi na wafujajasho nini cha kufanya juu ya serikali dharim kama hii,tuungane na wenzetu wachache walioamua kuweka maisha yao rehani kwaajili yetu,nawasilisha.

Kwa kweli mi binafsi nimeumia sana sana. Hapa nilipo natamani kulia...siamini kilichotokea. Yaani kweli serikali hii imeamua kwa makusudi kutufanya wajinga kiasi hiki??? Tuhuma zote zile za ubadhilifu na ufujaji wa pesa za umma dhidi ya mawaziri wameamua kukaa kimya?

Ehee Mungu tusaidie. Nasubiri tu nisikie tahrir square yetu iko wapi niende, kweli nimechoka.
 
Serikali ya Tanzania ni dhahiri sasa ni namba moja duniani kwa wizi wa mali za umma.Umaskini wetu tulio nao watanzania ni kwa sababu ya Rais dhaifu na ambaye hana huruma na umaskini wa wananchi wake. Mungu ametupa utajiri wa asili lakini kinachopatikana kinaliwa na mchwa wa serikali ya ccm.

Rais, MP, Mawaziri hadi mtendaji wa kijiji wa ccm ni wezi na hawawezi kukamatana kwakuwa wizi ndiyo jadi ya chama ccm. Lakini wakumbuke kwamba CHAKULA KIPATIKANACHO KWA UDANGANYIFU NI KITAMU LAKINI MWISHO WAKE HUWA KAMA MCHANGA KINYWANI.

SIKU IKIFIKA KILA MTU ATATOA HESABU YA KAZI HAKUNA KUKWEPA.
Enyi watawala wa Tanzania ni nani aliyewaroga?Muone aibu na mchukue hatua
 
unauliza majibu, hatua za kuchukua ni walizofanya warabu wa Tunisia na Misri
 
kuna mambo mengi yanayoendelea duniani na Tanzania yanayoashiria mahitaji ya mabadiliko.kamwe hatuwezi kuzima msisimko huu kwa propaganda au ujanjaujanja,ni hatari.hivyo kuendelea kutumia njia za hadaa wakati huu wa mahitaji ya mabadiliko duniani ni hatari,tena ni hatari kubwa kwa nchi ambayo haijapitia mchakato unaofanana na huu unaoendelea duniani.
 
Huwezi amini leo lecture zilisimama mida ya jioni wanachuo wakingoja maamuzi magumu ya mtoto wa mkulima,huwezi amini ni chuo kizima lakini mwee kilamtu ameanza kutukana,juu ya serikali na wafuasi wake.dah kifo hakina break!
 
Kwa kweli mi binafsi nimeumia sana sana. Hapa nilipo natamani kulia...siamini kilichotokea. Yaani kweli serikali hii imeamua kwa makusudi kutufanya wajinga kiasi hiki??? Tuhuma zote zile za ubadhilifu na ufujaji wa pesa za umma dhidi ya mawaziri wameamua kukaa kimya?

Ehee Mungu tusaidie. Nasubiri tu nisikie tahrir square yetu iko wapi niende, kweli nimechoka.

Maisha ni yako, chaguo ni lako.
Chakua kuonyesha Ghadhabu dhidi ya CCM na Serikali yake kwa vitendo, ili ulinde mali na rasilimali za nchi hii
 
Hii ya leo kali.nshasema tuliingia mkenge na hawa jk na ccm.nyerere alitwambia kuwa jamaa hajakomaa kiakili tukapuuza.ndugu zangu watz,tusipochukua maamuz magumu kama ya wamisir, nchi yetu iko hatarini.jk hana nia njema hata kidogo na nchi hii.ameamua kuitelekeza.nasis kama tuna muunga mkono kuitelekeza tz,bas tuamue moja.mnasemaje wazalendo
 
Chamsingi niviongozi wetu kuwashitakia wananchi,sijawahi kuona wabunge wanafki kama wabunge wa ccm!GAMBA limewakamata kweli
 
Ni kweli! waondoke sasa yatosha! kwa njia yoyote waende! sina hamu ya kusikia tena kikao cha wazee wa Dsm wala utoto wa ukulima....wote kuanzia JK, PM, Mawaziri waondoke maana sasa wanatuchezea waziwazi
 
Nadhani wananchi wote mliokuwa makini kufwatilia mwenendo wa kikao cha bunge leo mmeshuhudia jinsi Waziri mkuu alivyoulaghai umma wa watanzania kwa kuongelea masuala yasiyokuwa na msingi kwa Taifa letu na kuruka yale ambayo watanzania wote tulitega masikio kuyasikia kwa hamu kubwa. Tulitegemea angetoa uamuzi/kauli ya serikali juu ya mawaziri wote ambao wamefanya ubadhirifu katika ofisi za Umma. katika hali kama hii, waziri mkuu hata kugusia hajagusia. Naimani huyu katudharau sana sisi tunaojiita wenye nchi. Hatuwezi kuendelea kuiacha serikali yetu mikononi mwa viongoz wezi na wabadhirifu na wanaotetea mfumo dokozi.

Shime wananchi wote wazalendo tunajidiliane hapa what is the way forward????hii hali hatuwezi kuendelea nayo. Maana serikali imeamua kulinda wezi kibabe.

Hakuna dili inayochezwa bila ****** kupewa chake mapema na ndiyo maana inamuwia vigumu sana kuchukua hatua. Shimbo si huyo anaendelea kupeta.
 
Mnashindwaje kumuelewa lengo lake anataka mawazili wake waendelee kuumbuka ili alahisishe kifo cha ccm bila hao mawaziri kuendelea kuhalibu CDM wataingiaje IKULU?? CDM jiandaeni 2015 ikulu yenu jk ni kama isaya nyikani anaandaa mapito ya CDM kiulaini.
 
Pm amenishangaza kwa kusema kuwa serikali itashughulikia huu wizi. Tangu lini mwizi akajishughulikia. Serikali yetu ni sawa na mzazi anaeiba vijiko na sahani watoto walie mikono
 
Ndugu wana JF nimesikiliza kwa makini hotuba ya PM Mtoto wa mkulima na kugundua kitu kimoja ambacho kimepangwa kutumika kubadili mawazo ya wananchi na wanasiasa kwa ujumla kufuatia PM na Mawaziri wengine kukataa kujiuzuru.

Hii ni Katiba mpya!!
Katika hotuba yake amesema tume itaanza kukusanya maoni kuanzia tarhe 1 May 2012, kwa mantiki hiyo kuna siku saba tu kabla ya kubadili CD hivyo kuondoa kile tulichoambiwa ni upepo wa kisiasa ukizingatia nchii hii inaendeshwa kwa matukio.

Nawasilisha.
 
Wakati wa watanzania kufanya maamuzi magumu dhidi ya Rais na serikali yake umefika. sioni kitu mbadala zaidi ya kumkataa JK, Kumzomea yeye na mawaziri wake wote akiwemo Pinda kwa kulifikisha taifa mahali hapa. Nilidhani wangeelewa kidogo maneno ya kamanda Sugu leo bungeni lakini sioni kama kuna intentionality ya aina yoyote.

Mkulu anaendaje kuzika kwenye hali tete namna hii ya nchi? haiingii akilini hata kidogo! PM atadanganyaje umma wa watz namna hii kwa kuwatangazia kuwa tafanya maamuzi magumu na kisha apige siasa?

Kama watz tumeamua ujinga basi hapa ndiyo mahali pa kunyamaza: lakini kama imetosha, basi hapa ndiyo mahali pa kuchukua hatua. Makamanda tuongozeni sasa kwenye maamuzi magumu juu ya nchi yetu inayoliwa na mafisadi.
nawasilisha
 
Wewe unasema ya CAG, Mimi nasema bunge lisiwepo mana mabunge hasa ya CCM yanakula hela zetu afu hakuna yanachofanya. Kazi yao kubwa ni kuisimamia serikali. sasa kama serikali imewashinda kuisimamia, kwann tuendelee kula hasara ya kuyalipa posho majitu mapumbafu?? inasikitisha sana. Yani nchi yetu hata siku moja huwezi sikia habari zake nzuri. Mbona mnatufanya tuwe wanyonge ninyi viongozi wadokozi na wezi???kwa kweli i am not proud by my country particularly chini ya uongozi wa viongozi wadokozi na wezi.

Ndugu zetu wakulima wanateseka sana vijijini, ila serikali haioneshi kuwajali. Wagonjwa wanateseka, no one to help them. Rasilimali zetu zinapotea kila kukicha, wamefikia hadi kuuza Tembo???Kumbe tunasaka majangili porini, kumbe majangiri ni mawaziri na viongozi wetu????Shame on you ccm govt. CDM amka mianya hii ndio ya kuitumia kuingia ikulu, kwa madudu haya wanayofanya ccm, wallah 2015 wakiitaka hii nchi, lazma tutapakatana makofi mana serikali ya ccm imetufika shingon.

Great! Kila mtu asome maneno haya na atafakari.
 
tusitegemee hata siku moja kuwa mabadiliko ya kweli nchini yanaweza kuletwa kwa ushirikiano wa ccm na upinzani.ni mazingaombwe tu!kama kweli wabunge wa ccm walidhamiria kutukomboa dhidi ya ubadhirifu serikalini basi motion ya zitto ingeungwa mkono na wabunge wengi zaidi ya 75.hili halijatokea na kamwe haliwezi kutokea.
Sasa ni wakati muafaka wa chadema kuwaeleza wananchi jinsi serikali na wabunge wa ccm wanavyotuchezea shere!
 
Back
Top Bottom