Maoni yangu kuhusu NHIF kwa wote

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
209
236
Salaam wana JF,

Wakati ndugu zetu waislamu wakisherekea siku kuu ya eid el fitri, natamani tujadiliane kidogo kuhusu swala la Bima yq afya kwa wote.

Kiukweli, nachukua fursa hii kuipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuja na mpango wa bima ya afya kwa wote, maana watanzania wengi ambao hawana kipato kinachoweza kumudu gharama za matibabu wanapata changamoto kubwa sana za kupata matibabu bora kutokana na gharama za matibabu husika, hivyo mara nyingi watu hawa hukosa matibabu bora na wengine kupoteza kabisa maisha yao.

Nadhani serikali iendelee kuchakata kwa usahihi na kwa undani zaidi ili kuja na mpango madhubuti juu ya hili jambo na kupata ufumbuzi wa kuduma juu ya swala hili.

Sasa kwanini nimewaza kuja na uzi huu, nimeamua kuandika uzi huu kutokana na mchango wa Mmbunge shabiby katika bunge la bajeti hivi karibuni.

Na hoja yangu imejikita moja kwa moja kwenye ushauri wake kwamba serikali inaweza kutafuta chanzo cha mchango wa bima kwa wote kutoka katika laini za simu( yaani kutoka kwa watumiaji wa simu) ambapo kila mwezi itakatwa Tsh.2000 kama mchango wa bima ya afya kwa wote.

Binafsi nadhani ushauri wake haujazingatia hali halisi ya kiuchumi kutoka kwa wananchi, nasema haya kwasababu ya utafiti mdogo nilioufanya mtaani kati ya watu 10 watu 7 wanalalamika kuhusu ugumu wa maisha na wengine hata baadhi ya mahitaji muhimu hawayapati wakati woote lakini pia kumbuka wananchi hawa hawa tayr wananchi wanalipa tozo na kodi mbalimbali kwajili ya kusapoti serikali yao pasipo lawama wala manung'uniko, sasa ushauri kama huu endapo bunge likiupokea na likapitisha maana hii ni hatari sasa.
Hoja ya pili.

Je hiyo Tsh.2000 ya kila mwezi itahusisha makundi gani tukiachana na wanainchi? Kama itawahusu wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi je ushauri huo umezingatia mazingira halisi ya watumishi hao? Na ikumbukwe wafanyakazi hawa ndio wanaongoza katika kuchangia moja kwa moja kupitia mishahara yao ya kila mwezi. Hivyo kama mchango huu wa Tsh. 2000 kila mwezi utawahusu, je bunge halioni huu utakuwa ni unyonyaji wa hali ya juu?

UShauri
1.kwanini tozo zilizopitishwa na bunge kwajil ya ujenz wa miundombinu(madarasa) zilizokuwa zikikatwa katika miamala ya mitandao ya simu zisitumike kugharamia bima ili kuwapunguzia wanamchi mzigo wa kodi na tozo. Nashauri ivi kwakua kumekuwa serikali imefanikiwa kujenga madarasa mengi sana kiasi kwamba wanafunzi wanamadarasa ya kutosha kabisa.

2. kama kuna ulazima sana wa jambo hili basi serikali iangalie njia bora na sio hii ya Tsh. 2000 kila mwezi toka kwa mwananchi. Inaweza kufanya ivo kwa kufanya utafiti utakaowapa picha halisi ya namna gani swala mchango huo umepokelewa vipi na utayari wa wananchi ni upi. Pia wajue lain za watumish na ambazo sio za watumishi ili kutokukusanya michango mara mbili kutoka kwa watumish kama itakuwa imeamriwa watumishi wasichangie mchango huo. Vile vile itapaswa kujua ni wananchi wangapi ambao hawajiunga kabisa katika mfuko wowote wa bima ya afya ikiwemo wa NHIF.

MWISHO KABISA.
Haya ni mawazo yangu, sina nia ya kuleta taharuki wala uchochezi wa aina yoyote wala kumchafua yoyote, uzi huu ni kwaajili ya kuelimishana na ikiwezekana utumike kufikisha ujumbe kwa wambunge wetu kwamba wana wajibu wa kuwakilisha hoja zetu kwajili ya mustakabari wa maisha yetu na taifa letu kwa ujumla( wazingatie sana hali zetu za kimaisha na kiuchumi)

Karibuni tujengane wakuu🙏
 
Mkuu hoja ya mbunge kwa upande fulani ukiitazama unaweza kuona ina mashiko hivi maana mnufaika wa bima hiyo unakuwa wewe binafsi, maana ukiugua utatibiwa sasa kwanini usichangie

Changamoto ninayoiona ni kiwango kukata buku 2 ni nyingi sana na italeta shida kwenye makampuni ya simu kushuka mapato yao badala yake kiwe hata jero ambayo kwa mwaka wanaweza kukusanya zaidi ya bilioni 70+ nyingine sasa ndiyo waangalie kwenye maeneo mengine hasa maliasili zetu
 
Nakushukuru kwa mawazo yako Mkuu.
Kwakua hapa tunazungumzia afya zetu nitakubaliana nawewe, lakin kumbuka jukumu la msingi la serikali n kuwahudumia wanainchi, sasa ikitokea serikali ikapitisha hilo uone kama serikali itakuwa inadhihirisha kushindwa kuwahudumia wanainchi wake???

Na kumbuka hata kwenye izo hospital bado wanainchi wanapaswa kutoa michango yao ili wapate matibabu! Sasa huo mchango inamaana utaeda kufuta michango hiyo ama??
Kwa mawazo yangu nadhani serikali ingebuni njia nyingen ambayo sio kutoka kwa wanainchi moja kwa moja ili wanaichi wahudumiwe vyema pasina kutoa mchango kwakua wananchi hawa hawa kumbuka ndio wanatoa kodi zoooote.
 
Mkuu hoja ya mbunge kwa upande fulani ukiitazama unaweza kuona ina mashiko hivi maana mnufaika wa bima hiyo unakuwa wewe binafsi, maana ukiugua utatibiwa sasa kwanini usichangie

Changamoto ninayoiona ni kiwango kukata buku 2 ni nyingi sana na italeta shida kwenye makampuni ya simu kushuka mapato yao badala yake kiwe hata jero ambayo kwa mwaka wanaweza kukusanya zaidi ya bilioni 70+ nyingine sasa ndiyo waangalie kwenye maeneo mengine hasa maliasili zetu
Pia kutokana na mawzo yako hapo, vip umefikilia kuhusu hatma ya watumishi endapo ikionekana kila mmiliki wa lain ni lazima achangie iyo 2000 ?
 
Mkuu hoja ya mbunge kwa upande fulani ukiitazama unaweza kuona ina mashiko hivi maana mnufaika wa bima hiyo unakuwa wewe binafsi, maana ukiugua utatibiwa sasa kwanini usichangie

Changamoto ninayoiona ni kiwango kukata buku 2 ni nyingi sana na italeta shida kwenye makampuni ya simu kushuka mapato yao badala yake kiwe hata jero ambayo kwa mwaka wanaweza kukusanya zaidi ya bilioni 70+ nyingine sasa ndiyo waangalie kwenye maeneo mengine hasa maliasili zetu
Kutokana na serikali kushindwa kutengeneza fursa za kiuchumi zinazowafanya wananchi wake wainuke kiuchumi, kushindwa kuzuia ufisadi, rushwa na matumizi mengine mabaya ya kodi za wananchi, haina uhalali wa kuwarundikia mizigo ya tozo wananchi wake.Serikali inatakiwa kubuni vyanzo vingine vya mapato kutokana na rasilimali zilizopo ili kufadhili elimu,afya n.k.Kama hawawezi kutumia rasilimali zilizopo kupata pesa za kuendesha mambo hayo wakae pembeni.
 
Kama mtu hawez lapa 2000 hata ukiweka 100 hata lipa ikiwa ni hiyar tuachie serikali ifanye kaz yake
 
Kama mtu hawez lapa 2000 hata ukiweka 100 hata lipa ikiwa ni hiyar tuachie serikali ifanye kaz yake
Ni kweli serikali inatakiwa ifanye kazi yake, lakini si kwa kuumiza wananchi wake ambao 80% ni maskini wa kutupwa kutokana na serikali yenyewe kushindwa kufanya na kusimamia mambo ya msingi katika nchi.
 
Kote zunguka ila mimi naona ni kama hii bima ni sehemu tu ya serikali inatagta chanzo cha fedha ambazo iatenda kuzifanyia mambo mengine ikiwemo wafanyakazi wa mfuko kujikopa.
Huduma lazima zitakuwa chini na malalamiko yatakuwa mengi.
Kifurushi cha toto tu kimewashinda ije kuwa kila raia ana bima.
 
Kutokana na serikali kushindwa kutengeneza fursa za kiuchumi zinazowafanya wananchi wake wainuke kiuchumi, kushindwa kuzuia ufisadi, rushwa na matumizi mengine mabaya ya kodi za wananchi, haina uhalali wa kuwarundikia mizigo ya tozo wananchi wake.Serikali inatakiwa kubuni vyanzo vingine vya mapato kutokana na rasilimali zilizopo ili kufadhili elimu,afya n.k.Kama hawawezi kutumia rasilimali zilizopo kupata pesa za kuendesha mambo hayo wakae pembeni.
Mkuu hata hivyo vyanzo vingine bado atakayehusika ni mwananchi huyohuyo ukiweka kwenye bidhaa mfano ukiongeza kodi mfanyabiashara atapandisha bei tayari tumeathirika, weka kwenye mafuta kote huko tutaguswa tu
 
Kiongozi unadhani kipi ni sahihi sasa ?
 
Back
Top Bottom