Hakuna nchi iliyoendelea kwa kubadilisha Chama!

Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!

Bora turud nyuma kimaendeleo kuliko kuendelea na liccm
 
Hv south africa kabla ya mandela ...enzi botha na de clark walikuwa chini ya mwamvuli wa ANC au vip naomba kujulishwa

Afrika Kusini kabla ya Mandela ilikuwa ikongozwa na Chama kimoja tu kilichoitwa ,,National Party" kuanzia mwaka 1948-1994 mwisho wa Apartheid na ndicho kilichojenga AK kuwa jinsi ilivyo na wala hawakubadilisha vyama!
 
Rudi shule bandugu.Inaonekana ni mwana CCM maslahi.Usijari Ukawa ikichukua nchi utaendelea kupumua,ondoa ofu we kiliaza uliokithiri.
 
hivi una habari kenya kwa sasa ni nchi ya uchumi wakati?

Usiwe mshabiki wa kijinga ccm haiwezi imesha shindwa,

Mkuu pole kwa kubishana na mtu alievia akili! Achana nae, endelea kutoa elimu kwa watz wengine. Huyo nyang'au ataendelea kukuchosha akili!
 
Barbosa, mbona hujazitaja India, Brazil, Canada, Australia, Canada, Uingereza, Ujerumani, na Ufaransa? Angalau tuelezee kuhusu hizo super power tatu za mwisho.

Vv
 
Kijana hauna uelewa wa kutosha toka mwaka 1999 hadi mwaka 2014 nilikuwa india kwa masomo wenzetu wameweza kutawaliwa na viongozi wakuu wawili yaani waziri mkuu alikuwa anaitwa Atari bihari Vajpayee waziri
1998–2004, huyu alijuikana sana kama mkombozi wa
sayansi na mataalam wa electronics, uchumi wa india ulikuwa kiasi new technology wakaweza kutengezeza dege ya abiria 10 then Atari then akajisahau kwa watu wa ali ya chini yaani masikini waliyo wengi wakamkataa katika uchaguzi wa mwaka 2004 chama cha BJP amacho alikuwa anaongoza kikaanguka na ktk uchaguzi mkuu na chama cha indian national congress kunachoongoza na Sonia Gandhi kilishika hatamu huku waziri mkuu akiwa ni
Manmohan Singh
kutoka 2004 to 2014 sera ya national congress kuwa uchumi wa kati yaani masikini wa india aweze kupata vitu vya msingi yaani,, chakula , malazi na matibabu bure kwa india yote hii inawezekana kama inchi yetu yen wa million max 50, matibabu shida, vyakula bei juu , usafiri bei juu , mafuta ya taa bei moja na betrol hii hatuitaji miujiza tena tunahitaji kubadili chama na si mtu.
ili maisha ya watanzania yabadilike lazima ccm iyondoke kwa sababu yoyote atakayekuja bado wataendelea kulindana tu hakuna jipya.
 
Unazidi kunikera wewe!umekariri India ni maskini sababu 1996 uliambiwa India kuna maskini kuliko bongo?
Unajua nchi zinazoitwa BRICS?hiyo I hapo ni India na BRICS wote wako vizuri kwenye swala la industrialization. India sahiv ana export magari na mashine nyingine heavy duty kama hana akili nzuri.Na hakuna nchi maskini yenye uwezo wa kufanya industrialization kama walivofanya India.
India ina wataalam mbalimbali waliosambaa kila kona dunia hii kuanzia madaktari bingwa(mpaka ccm wenzako wanaenda kutibiwa huko kwa maskini),makandarasi,astronauts, teachers yani kila sekta humkosi mhindi.
weeeeeee,india na pakistan mpaka wana makombora ya ile 'kitu' hatari, wako mbeleeeeee
 
Kenya ni nchi masikini na bado inaendelea hapa nimezungumzia nchi zilizoendelea (Kuna tofauti kati ya nchi inayoendelea na zilizoendelea)!

Ulaya yote ilijengwa na Wafalme na walikuwa hawabadilishwi mambo ya kubadilsha vyama yemakuja baada ya nchi kuendelea tayari! Na isitoshe historia ya Ulaya na wazungu iko complex sana nakuendela kwao kuweza kutaka kuwaiga watu ambao tunafanana kwenye mambo mengi ni waasia kwa maana wote tulitawaliwa wemeendelea hivi majuzi, hawajakuwa na makoloni n.k na wote hawajawahi kubadilsha vyama na wale wanaobadilsha kila siku ni masikini kama India , Bangladeshi, Pakistani n.k

Marekani ilijengwa na mfalme gani? halafu hauwez kutoka kuwa nchi maskin na kuruka kwenda kuwa nchi iliyoendelea.... wakenya nchi yao ni ya uchumi wa kati sasa wanapoelekea ni mbele zaidi... sisi tutazidi kuwa maskin tena umaskin uliokithiri..
 
Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!

Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!

Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!

Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!

Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!
Pole yako mkuu, MUTAISOMA NO.
 
Hujui history..twambie USA(1933) RUSIA (1917).U KNOW NOTHING

Unajua ni nani amejenga Urusi unayoijua wewe? Ni Ufalme wa Urusi (Russian Empire) ndiyo waliojenga Urusi hao makomunisti akina Lenin wamekuja nchi tayari imeshasimama kuna mamiji ya ukweli kama St. Petereburg, Moscow wanasayansi wote wa Soviet walisoma wakati wa Russian empire na isitoshe Soviet Union iliyofwata haikubadilshwa kwa kupiga kura mpaka leo hii!
 
Kenya ni nchi masikini na bado inaendelea hapa nimezungumzia nchi zilizoendelea (Kuna tofauti kati ya nchi inayoendelea na zilizoendelea)!

Ulaya yote ilijengwa na Wafalme na walikuwa hawabadilishwi mambo ya kubadilsha vyama yemakuja baada ya nchi kuendelea tayari! Na isitoshe historia ya Ulaya na wazungu iko complex sana nakuendela kwao kuweza kutaka kuwaiga watu ambao tunafanana kwenye mambo mengi ni waasia kwa maana wote tulitawaliwa wemeendelea hivi majuzi, hawajakuwa na makoloni n.k na wote hawajawahi kubadilsha vyama na wale wanaobadilsha kila siku ni masikini kama India , Bangladeshi, Pakistani n.k
Mbona unajichanganya!!? Kenya kweli bado ni nchi inayoendelea lkn si masikini. Lkn imefikia kiwango cha uchumi wa kati baada ya kukiondoa chama cha kanu. Kabla ya hapo imeongozwa na chama kimoja na kwa muda wote huo ilikuwa masikini. Kwa nini hutaki kuizungumzia hiyo tofauti iliyopatikana kenya kwa muda mfupi baada ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi!!??
 
Unataka utafiti gani? Nimekwambia hakuna nchi iliyoendelea ambayo ilibadilisha Chama wakati wa kuendelea kwake na mifano nimekupa sasa kama unapinga unaweza pia kuweka mifano badlaya tu kusema wacha kuongea sijui nini...
Kwa namna tu unavyojibu hoja za wachangiaji wa "hoja yako mfu" inaonesha hukujiandaa bali ulichokileta ni propaganda zilezile za jamaa wezi wa kijani wanaotukata kwa jembe lao na kutugonga kwa nyundo kutukandamiza ktk umaskini wa kufa MTU!!

Usilazimishe watu wakubaliane na utumbo wako!!

By the way, ni ili iweje basi? Sisi ni Watanganyika na wazanzibar and we have our own way of doing and seeing things

Tatizo letu sisi ni Chama cha mapinduzi na mfumo wake wa utawala wa ovyo uliojaa ufisadi na rushwa kilichoujenga kwa karibu nusu karne sasa. Hicho ndicho kikwazo cha mafanikio yetu ktk nyanja zote

So, what we need now is to evict CCM and its subsidiaries, since, that's our problem.!!
 
]Marekani ilijengwa na mfalme gani[/COLOR]? halafu hauwez kutoka kuwa nchi maskin na kuruka kwenda kuwa nchi iliyoendelea.... wakenya nchi yao ni ya uchumi wa kati sasa wanapoelekea ni mbele zaidi... sisi tutazidi kuwa maskin tena umaskin uliokithiri..

Soma vizuri Historia ya Marekani, isitoshe usitake kufananisha nchi za Kizungu na zetu za Kiafrika nchi za wazungu wana Historia ndefu sana usifikiri wameanzia juzi unajua Marekani ilianzishwa kwenye mwaka 1770 huko? Na unajua ni nani alianzisha Marekani? Usiwaone akina Obama ukafikiri Marekani ni ya mwaka 1970!
Ila nimetoa mfano nchi ambazo tunafanana kwamba wote tulitawaliwa, tukanyonywa n.k na zinaongozwa na chama kimoja mpaka leo hii na zimeendelea!
 
unajua ni nani amejenga urusi unayoijua wewe? ni ufalme wa urusi (russian empire) ndiyo waliojenga urusi hao makomunisti akina lenin wamekuja nchi tayari imeshasimama kuna mamiji ya ukweli kama st. Petereburg, moscow wanasayansi wote wa soviet walisoma wakati wa russian empire na isitoshe soviet union iliyofwata haikubadilshwa kwa kupiga kura mpaka leo hii!
urusi ya yuri andropov,contantine chernako,nikita,brezhnev,lenin na mkali stalin walikuwa wafalme! Weeeeee
 
Maendeleo yanapatikana kama viongozi wana nia ya dhati. Nia ya ccm ni kuiba na kufilisi watanzania. Hawataki kutoka kwasababu miradi yao yakifedhuli itafika kikomo. Kama unabenefit moja kwa moja kwa ccm kuwa madarakani jua watanzania wamechoka kuibiwa
 
Back
Top Bottom