Ibada ya kwanza
JF-Expert Member
- Mar 21, 2013
- 3,282
- 1,806
Watu wengi ukisikiliza maoni yao utasikia wanakwambia tunataka CCM iondoke, ukiwauliza nani aje wanakwambia yoyote tu bora tu tubadilishe ili tuendelee sasa mimi leo ninawasaidia kubadilisha Chama hakuleti maendeleo kwanza ni kinyume chake!
Hakuna nchi tajiri au iliyofanikiwa Duniani kiuchumi iliyowahi kubadilisha Chama, nchi zote zilizo tajiri leo hii zimekuwa zikiongozwa na Chama kimoja siku zote na hawajabadilisha na nitatoa Mifano, Ujapani inaongozwa na Chama kimoja kwa Miaka zaidi ya 50 na ndicho kilichoijenga Ujapani, Korea Kusini inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Korea, Uchina inaongozwa na Chama Kimoja na ndicho kilichojenga Uchina, Taiwani Chama Kimoja, hata Malaysia inaoongozwa na chama kile kile tangu Uhuru hawajawahi kubadilisha na ndicho kilicholeta maendeleo Malaysia!
Afrika Kusini iliongozwa na Chama Kimoja cha National Party kuanzia 1948 mpaka 1994 na ndicho kilichojenga AK tunayokimbilia kila siku, hata hapa Afrika nchi zilizofanikiwa kama Angola, Namibia, Botswana na sasa hivi Msumbiji wanakwenda vizuri hawajawahi kubadilisha Chama!
Sasa ukiangalia nchi zenye tabia ya kubadilisha badilisha Vyama ni masikini kama India, Pakistani, Zambia, Kenya, hata nchi za Ulaya siku zinaanza kuwa na matatizo ya Kiuchumi baada ya kuanza kubadilisha badilsha vyama kumbuka Ulaya ni tajiri kwa sababu ilijengwa na Wafalme ambao walikuwa hawabadilshwi!
Hivyo mimi bado naamini kabisa kwamba kama TanZania tunaweza kutoka hapa kimaendeleo basi ni ndani ya CCM na si kwingineko waache Upinzani watumike kama vile sasa hivi kuishtua CCM ili iamke kama ilivyofanya sasa hivi kwa kujivua gamba na sasa tuko ready for take off!
Bora turud nyuma kimaendeleo kuliko kuendelea na liccm