CCM kutoka madarakani haimaanishi nchi itabadilika

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,026
12,332
Ni muda sasa wakuambiana ukweli.

Na ukweli ni kwamba sikweli kuwa changamoto na matatizo ya Watanzania yatatamatika pale CCM itakapo toka madarakani.

Mtanzania ana matatizo na changamoto za aina mbili zinazo mkabili

Moja changamoto ya yeye kuwa Mtanzania pale tu utakapo kuwa Mtanzania kuna changamoto za kurithi unapata kutoka vizazi vilivyo pita na hizi ni changamoto zaidi za kitamaduni na mtindo wa maisha.

Pili kuna changamoto za kuwa mwafrika mweusi hizi ni changamoto ambazo utazikuta ukienda Malawi, ukienda Zambia, ukienda Ghana na sehemu yoyote ilipo jamii kubwa ya watu weusi.

Hivyo kutoka CCM madarakani haimaanishi chama kitakacho ingia kitakuwa hakina changamoto hizo.

Changamoto hizo mbili zipo kwa Watanzania waliopo CCM na Watanzania waliopo vyama vingine na hata wasio na vyama.

Mfano suala la kutawaliwa na chama kimoja halijaweza kuwa tatizo kwa China kuwa superpower duniani, halijaweza kuwa tatizo kwa Singapore kuwa na uchumi mkubwa, halijaweza kuwa tatizo kwa Vietnam uchumi wake kukua kwa kasi, halijaweza kuwa tatizo kwa Korea kujiimarisha kiulinzi, kiteknolojia na kiviwanda, halikuweza kuwa tatizo kwa Japan kukua na uchumi mkubwa, halikuwa kizuizi kwa Taiwan kupata maendeleo makubwa.

Lakini suala la chama kimoja kukaa muda mrefu kwetu lina onekana ni tatizo kwa nini ? Sababu hizo mbili zina athiri.

Kingine mabadiliko ya kivyama Afrika hayajaleta maendeleo ya kasi ya maendeleo ukilinganisha na hizo nchi nilizo tolea mfano ambazo zimeweza kuwa chini ya utawala wa chama kimoja kwa muda mrefu.

Malawi wamefanya mabadiliko, Kenya wamefanya mabadiliko, Zambia wamefanya mabadiliko lakini hizi nchi zote zipo katika cycle ile ile tuliyo nayo waafrika wengine.

Mnapaswa kufahamu sipingi mabadiliko ya kuitawala ila nipende kuwa kumbusha Tanzania, Watanzania, Africa na Mwafrika tuna changamoto na matatizo ya kiasili yanayo athiri mabadiliko na maendeleo yetu.

Muafrika aliyepo marekani ( black Americans) hana tofauti na mwafrika aliyepo Durban Afrika kusini.

Muhindi, muarab, mchina, mjapan, mzungu,mkorea aliyepo nje ya nchi yake hana tofauti na aliye ndani ya nchi yake kitamaduni, kufikiri na kutenda.

Waafrika na Watanzania tuna matatizo ya asili pale tu unapo zaliwa mwafrika na Mtanzania unazaliwa na matatizo ya kurithi.
 
Mie naamini itabadilika sana kwa sababu;
Rushwa inaweza kukoma kabisa hivyo kuboresha huduma za Jamii
Ufisadi uliokithiri utaisha hivyo fedha kwenda ktk matumizi sahihi
Wizi ktk mifuko ya jamii ie NSSSF na PSSSF itakoma hivyo kuboresha mafao ya wastaafu.
Wizi katika mifuko mingine ie NHIF kukoma hivyo kumudu matibabu kwa wote na HAKI
 
Mie naamini itabadilika sana kwa sababu;
Rushwa naweza kukoma kabisa
Ufisadi uliokithiri utaisha hivyo fedha kwenda ktk matumizi sahihi
Wizi ktk mifuko ya jamii ie NSSSF na PSSSF itakoma hivyo kuboresha mafao ya wastaafu.
Wizi katika mifuko mingine ie NHIF kukoma hivyo kumudu matibabu kwa wote na HAKI
Hayo hayawezi kukoma ni matatizo ya kurithi ya kitamaduni ambayo ukienda chama chochote utayakuta.
 
Ndio maana Huwa sioni haja ya kutoka madarakani ccm au hicho mnaita Katiba Mpya.

Si Zambia Wala Kenya ambako Kuna kitu Cha maana watu wamepata Baada ya kufanya Mabadiliko sana sana ni kuvuruga na kuongeza ugumu wa Maisha tuu.
Sisi waafrika tuna matatizo ya kiasili zaidi kuliko ya kisiasa mfumo wetu wa kimaisha na kitamaduni una athiri mpaka siasa zetu.
 
Tatizo sio ccm
Tatizo sio Katiba
Tatizo lipo kwa Watu Wenyewe.

Muafrika hata aje aongozwe na malaika atabaki kuwa maskini tuu kwa sababu muafrika hataki kuwajibika kwenye wajibu wake. Anataka wajibu wake ufanywe na mwingine.
Changamoto kubwa inakuwa hapo
 
Wafia vyama hawawezi kukuelewa ila huo ndo ukweli. Matatizo yetu yanatokana na utamaduni na mifumo ya maisha tuliyoichagua. Kwa mfano.

1. Ubinafsi - kila mtu anajiangalia mwenyewe kwanza na si masilahi ya Taifa. Akipewa kusimamia mradi anaona ndo sehemu ya kujinufaisha.

2. Rushwa - kwa sababu ya ubinafsi watu hawapendi kuishi kwa mujibu wa sheria. Atatoa rushwa ili sheria au utaratibu uipindishwe ajinufaishe yeye.

3. Uvivu - Tunataka pesa bila kufanya kazi. Yaani mtu hata umlipe shs ngapi anafanya kazi kwa kuruka ruka bora liende.

4. Kutopenda ubora - yaani kila mtu anajifanyia mambo bila kuangalia ubora. Ndo maana tunajenga hovyo hovyo bila hata kuacha njia. Huyu anajenga hivi huyu anajenga vile. Huyu kapanga vitu barabarani huyu kafanya kile yaani staili yetu ni ya hovyo hovyo. Hata kazini watu wanafanya kazi hovyo hovyo tu hakuna ubora.

5. Kutokupenda kusoma na kujua mambo kiundani. Yaani tunasomaga videsa na vitini vya hapa na pale ili mradi tufaulu tupate vyeti. Ndo maana 90% ya watanzania waliomaliza vyuo vikuu hawajui wamesoma nini. Wanazurula mtaani kwa sababu wana vyeti lakini hawana elimu. Walioko makazini wanafanya kazi hovyo hovyo maana hawana elimu bali wana vyeti.

6. Kufanya mambo kwa kujuana. Yaani hatuangalii nani anaweza, sisi tuna mpaka kazi au zababu mtu tunaye mjua au atakaye tupa kitu fulani.

7. Uongo - report mbalimbali zinaandikwa zimejaa uongo..kila mtu kuanzia wa chini hadi boss ni waongo.

8. Utapeli - kila mti anatafuta mtu wa kumtapeli ampige hela. Iwe kwenye siasa, uchumi, mapenzi..yani kila sehemu ni utapeli tapeli tu.

9. Ushirikina - watu wanaamini ushirikina kwenye kila jambo.

10. Ulimbukeni wa Dini - Tunajidai tuna dini kila makanisa na misikiti ina jaa lakini nyuma ya pazia tunafanya mambi mengine ya hovyo hovyo.

11. Unafiki - a.k.a uchawa. Kila mtu ni mnafiki atajidai anaongea hadi anatokwa na povu kumbe unafiki tu.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanatufanya kuendelea kuwa chini.

Je ni chama cha siasa kitakacho weza kubadilisha hizi tabia na tamaduni zetu ?
 
Upo sahihi. ni ngumu sana kubadili tabia za watu ni sawa na kufanya wachina wasivute sigara au wasinywe chai au kufanya wahindi wasiwe wachafu au wasiwe na madaraja katika jamii.

Tamaduni na mfumo wa maisha ni moja ya kitu kina athari sana katika jamii au taifa.

Hata leo yakifanyika mabadilishano ya watu wazungu waje Afrika na waafrika waje, wajapan waje Tanzania na Watanzania waende Japan bado wazungu na wajapan watatuacha tena mbali kabisa.
 
Ndio maana Huwa sioni haja ya kutoka madarakani ccm au hicho mnaita Katiba Mpya.

Si Zambia Wala Kenya ambako Kuna kitu Cha maana watu wamepata Baada ya kufanya Mabadiliko sana sana ni kuvuruga na kuongeza ugumu wa Maisha tuu.
Uchumi wa Kenya ni mkubwa sawa na wa Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi kwa pamoja huku ikiwa ina rasilimali chache sana kulinganisha na Tanzania.

Ni ujuha kujilinganisha na Malawi ambayo ni kama mkoa mmoja tu huku ikiwa haina bandari, nchi ambayo ni landlocked bila rasilimali zozote muhimu.

Zambia ilikuwa ikitawaliwa na chama kimoja kwa muda mrefu sana na pia tatizo kubwa lingine iliingia katika mfumo wa vyama vingi bila kufanya mabadiliko makubwa ya katiba hali iliyopelekea utawala mwingine wa chama kimoja kwa miaka 20 tangu mwaka 1991. Hata hapa Tanzania CHADEMA au chama kingine wakiingia madarakani kwa katiba hii bila mabadiliko makubwa wanaweza wasiwe tofauti sana na CCM.
 
Wafia vyama hawawezi kukuelewa ila huo ndo ukweli. Matatizo yetu yanatokana na utamaduni na mifumo ya maisha tuliyoichagua. Kwa mfano.

1. Ubinafsi - kila mtu anajiangalia mwenyewe kwanza na si masilahi ya Taifa. Akipewa kusimamia mradi anaona ndo sehemu ya kujinufaisha.

2. Rushwa - kwa sababu ya ubinafsi watu hawapendi kuishi kwa mujibu wa sheria. Atatoa rushwa ili sheria au utaratibu uipindishwe ajinufaishe yeye.

3. Uvivu - Tunataka pesa bila kufanya kazi. Yaani mtu hata umlipe shs ngapi anafanya kazi kwa kuruka ruka bora liende.

4. Kutopenda ubora - yaani kila mtu anajifanyia mambo bila kuangalia ubora. Ndo maana tunajenga hovyo hovyo bila hata kuacha njia. Huyu anajenga hivi huyu anajenga vile. Huyu kapanga vitu barabarani huyu kafanya kile yaani staili yetu ni ya hovyo hovyo. Hata kazini watu wanafanya kazi hovyo hovyo tu hakuna ubora.

5. Kutokupenda kusoma na kujua mambo kiundani. Yaani tunasomaga videsa na vitini vya hapa na pale ili mradi tufaulu tupate vyeti. Ndo maana 90% ya watanzania waliomaliza vyuo vikuu hawajui wamesoma nini. Wanazurula mtaani kwa sababu wana vyeti lakini hawana elimu. Walioko makazini wanafanya kazi hovyo hovyo maana hawana elimu bali wana vyeti.

6. Kufanya mambo kwa kujuana. Yaani hatuangalii nani anaweza, sisi tuna mpaka kazi au zababu mtu tunaye mjua au atakaye tupa kitu fulani.

7. Uongo - report mbalimbali zinaandikwa zimejaa uongo..kila mtu kuanzia wa chini hadi boss ni waongo.

8. Utapeli - kila mti anatafuta mtu wa kumtapeli ampige hela. Iwe kwenye siasa, uchumi, mapenzi..yani kila sehemu ni utapeli tapeli tu.

9. Ushirikina - watu wanaamini ushirikina kwenye kila jambo.

10. Ulimbukeni wa Dini - Tunajidai tuna dini kila makanisa na misikiti ina jaa lakini nyuma ya pazia tunafanya mambi mengine ya hovyo hovyo.

11. Unafiki - a.k.a uchawa. Kila mtu ni mnafiki atajidai anaongea hadi anatokwa na povu kumbe unafiki tu.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanatufanya kuendelea kuwa chini.

Je ni chama cha siasa kitakacho weza kubadilisha hizi tabia na tamaduni zetu ?
Haya yote ni matatizo yanayotokana na uongozi wa kisiasa.
 
Kadri tutakovyobadiri ndivyo tutapata matokeo mazuri huko mbele, watawala hawezi kujirekebusha iwapo watakuwa na uhakika wa kuwepo madarakani miaka yate, na kadri wanavyoendelea kuwepo madarakani mwananchi wa kawaida anazidi kuumia.
 
Acha unafiki wewe. Maneno mengi ili kuhalalalisha CCM kuendelea kuwa madarakani. Watu sijui mpoje. Kama huna la maana Kaa kimya. Eti CCM ilitoka madarakani haimanishi maendeleo yatapatikana.

Kaangalie hapo Rwanda baada ya Kagame kuingia au Kenya baada ya KANU kutoka, uone maendeleo yaliyopatikana. Tatizo mnaiabudu CCM na kutulazimisha ujinga wenu kuwa haiwezi kutoka madarakani. Punguza unafiki.
 
Reluxy acha jazba.
Kenya wananchi wanaandamana kama yale maandamano ya CDM kwenye majiji Dar,Mwanza,n,k.
wakenya wanalalama maisha magumu vitu bei juu.

Rwanda Kagame anauwa wapinzani wake pia hali ya maisha ni ngumu.
sijaona cha maana Kenya na Rwanda kuizidi Tanzania.
 
Acha unafiki wewe. Maneno mengi ili kuhalalalisha CCM kuendelea kuwa madarakani. Watu sijui mpoje. Kama huna la maana Kaa kimya. Eti CCM ilitoka madarakani haimanishi maendeleo yatapatikana.

Kaangalie hapo Rwanda baada ya Kagame kuingia au Kenya baada ya KANU kutoka, uone maendeleo yaliyopatikana. Tatizo mnaiabudu CCM na kutulazimisha ujinga wenu kuwa haiwezi kutoka madarakani. Punguza unafiki.
Umesoma vyema nilicho andika ?
 
Ni muda sasa wakuambiana ukweli.

Na ukweli ni kwamba sikweli kuwa changamoto na matatizo ya Watanzania yatatamatika pale CCM itakapo toka madarakani.

Hivyo kutoka CCM madarakani haimaanishi chama kitakacho ingia kitakuwa hakina changamoto hizo.
Suppose ni kweli CCM itatoka madarakani, ndio aje nani nafasi ya CCM?!.
Kinachofanya CCM inaendelea kutawala milele Tanzania ni kwasababu bado hatuna chama mbadala, hivyo CCM ikiondoka kati ya hawa waliopo, ndio aje nani?.

P
 
Back
Top Bottom