Nchi za kikomunisti ni nchi zilizo chini ya amri na utawala wa chama kimoja. Nawakumbusha tu msisahu hilo

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,013
12,281
Nawafunza somo jepesi.

Mfumo wa kikomunisti una toa mamlaka ya kuitawala kwa nchi kwa chama kimoja pekee.

Hata kama nchi ina mfumo wa vyama vingi kama China ila mamlaka ya kutawala China yapo chini ya wakomunisti pekee kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya watu wa China.

Nawakumbusha kuna Jamhuri fulani kutoka mashariki mwa Afrika ilikuwa na mfumo mfanano wa kikomunisti chini ya chama kimoja na ikahamia vyama vingi kimaneno sio kimatendo tena bila mabadiliko makubwa kuthibitisha hilo na mpaka leo katiba yake inasema nchi hiyo ni ya "ukomunisti wa kiafrika".

Nchi hiyo inatambua mamlaka ya utawala yapo chini ya hicho chama kimoja pekee cha ukomunisti wa kiafrika.

Nawakumbusha tena nchi za kikomunisti chama ni kikubwa kuliko serikali na chochote kile katika nchi hii siri hii alinipa rafiki yangu mmoja hivi mchina anakuambia the party leads all hapa akimaanisha chama cha kwao cha kikomunisti kumbuka mashariki mwa Afrika kuna chama cha ukomunisti wa kiafrika.

Vyama rafiki vya hicho chama cha ukomunisti wa kiafrika kutoka mashariki mwa Afrika ni vyama vya kikomunisti vya China na Vietnam.

Mfumo wa kikomunisti hau ruhusu utawala wa vyama vingi ni muda wa kukumbushana na kuambizana ukweli.
 
Ila hicho chama cha ukomunisti wa kiafrika hakifuati misingi yote ya ukomunisti kama inavyo paswa kwa sasa.
 
Then by your definition, hakuna hata nchi moja ya kikomunisti duniani.

Huwezi ukasema kwamba nchi fulani ni ya kikomunisti eti kwa sababu serikali yake iko chini ya chama kimoja.

One party rule is not a sufficient or necessary condition for communism

Itoshe, Tanzania au hiyo nchi unayoidai, haijakuwa Nchi ya kikomunisti.Sio kwa sera, sio kwa utamaduni na hata kwa kuigiza. Usipotoshe.

Na kwa Taarifa yako, uwongo huo(propaganda hiyo) ungeweza kuisambaza na labda, labda, ikachukuliwa kikasuku na wapuuzi na wajinga huko miaka ya nyuma, sio leo.

Vilevile, hiyo.misamiati, ikumbukwe ni ya wale Mafashisti na mabeberu wenye fikra finyu za siasa za Dunia, Uchumi wa Dunia n.k Ni siasa za Hadaa tu. Huku Afrika hazifanyi kazi hata kwa Uchawi.

Unajipotosha.
 
Hueleweki ni kipi unacho zungumza haswa
 
Back
Top Bottom