Hakuna mbunge jasiri anaweza kuuliza swala hili bungeni?

sisi kwa sisi

Senior Member
Feb 1, 2012
119
2
Kuna kauli mbili tofauti zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa elimu na Mafunzo ya ufundi kuhusu kutaifishwa shule zote za madhebu ya dini nchini.
Kauli ya Mkuu wa Mkoa alidai kwamba Shule za madhehebu ya kikirsto zimetaifishwa majengo tu na sio ardhi.
Lakini waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi alidai kwamba serekali imetafisha ardhi,majengo na kila resource na inamilki asilimia 100.
Lakini bado kauli za viongozi wengine hasa kama afisa wa elimu wanadai waziri Kapotoka kutoa kauli hiyo.na tayari jambo hili limeanza kuchukua sura mpya zaidi ya kidini jambo ambalo ni mustkabli mbaya kwa taifa letu changa
kwa ufupi kila mpenda amani na maendeleo ya nchi anashindwa kujua nini hasa ukweli wa jambo .Hata humu Jf kila mmoja navutia upande wake
Hakuna mbunge jasiri bila ya kuangalia dini yake anaweza kuhoji Bungeni swali hili japo swali la papo kwa papo kwa mustkbali wa taifa letu?
Maana swali hili linahitaji wabunge jasiri na sio kila mbunge anaweza kuhoji hasa ukizingatia unyeti wa jambo lenyewe hasa anaweza kuandamwa na vyombo vya habari vilivyoegemea udini zaidi badala ya mustkabli wa taifa letu
hapa nawakusudia sana akina Mnyika, Zitto, lissu,Hamad ,Lema Rashid, ambao kwa kipindi kirefu ndio wanaonekana wanania ya dhati kwa ukombozi wa taifa letu
. lkn pia ndio wabunge wasiopenda machafuko nchini

nchini
ili Kauli ya Serekali ijulikane na kuondoa msugaono huu?
 
mimi nakusaida-wametaifisha majengo na ardhi iliyoshikiliwa hayo majengo,
eneo la ardhi lolote pembeni na madarasa,mabweni na dining ni mali ya kanisa.
nishasoma shule ambapo madarasa,dining,na mabweni ni mali ya serikli,ila maeneo ya pembeni kanisa walikuwa na bado hadi leo wanayatumia hayo maeneo kwa matumizi yao binafsi.
 
Mimi siamini hivyo, ndio maana nahitaji wabunge kama Lissu. Mnyika wahoji swala hili bungeni ili tupate kauli ya serekali bungeni
 
mimi nakusaida-wametaifisha majengo na ardhi iliyoshikiliwa hayo majengo,
eneo la ardhi lolote pembeni na madarasa,mabweni na dining ni mali ya kanisa.
nishasoma shule ambapo madarasa,dining,na mabweni ni mali ya serikli,ila maeneo ya pembeni kanisa walikuwa na bado hadi leo wanayatumia hayo maeneo kwa matumizi yao binafsi.
kwa hivyo unakusudia mabanda tu. maana waislam wao wametaifishiwa hadi hayo mabweni na kila kitu. sasa ukweli wa jambo hili ni kwamba shule za kikirsito na zikiislam wametaifishiwa tofauti kwa sheria 2 tofauti?
 
Mimi sichangii lolote katika hili kwa sababu umeniudhi katika post yako hapo juu umesema "......taifa letu changa". Miaka 50 ya uhuru bado unaliona taifa changa, unategemea litakua na kukomaa baada ya miaka mingapi??
 
...nimefurahishwa na comment ya Jsaudi. Mtoa thread hapo kwenye thread yako unasema taifa changa. Wapi na wapi kwa nchi iliyoadhimisha miaka-50 ya Uhuru halafu hiyohiyo uiite taifa changa? Mtoa mada hapo ushaharibu muktadha mzima wa mada yako. Tanzania siyo taifa changa,tumeadhimisha juzi miaka 50 ya UHURU
 
kwa hivyo unakusudia mabanda tu. maana waislam wao wametaifishiwa hadi hayo mabweni na kila kitu. sasa ukweli wa jambo hili ni kwamba shule za kikirsito na zikiislam wametaifishiwa tofauti kwa sheria 2 tofauti?

Hata ingekuwa hivyo si mbaya(japo najua sivyo_)kwani shule za kiislam zilizotaifishwa ni chache sana ukilinganisha na za Kikristo.
 
Kuna msemo kwenye sheria unasema quid quid solo cedit. Every thing attached to the land is part of the said land. So hapo majengo na ardhi pia ni mali ya waliotaifisha. May be kama hayo maeneo ya pembeni wana hati tofauti na yale maeneo ya shule ila na yenyewe kama yako kwenye title moja huo msemo hapo juu unarudi kuapply
 
Mimi sichangii lolote katika hili kwa sababu umeniudhi katika post yako hapo juu umesema "......taifa letu changa". Miaka 50 ya uhuru bado unaliona taifa changa, unategemea litakua na kukomaa baada ya miaka mingapi??
Unafananisha umri wa nchi na umri wa kibinadamu? Kwamba Binadamu akifika miaka 50 anelekea uzeeni, kwa hivyo na nchi ni vivyo hivyo?
 
Mimi sichangii lolote katika hili kwa sababu umeniudhi katika post yako hapo juu umesema "......taifa letu changa". Miaka 50 ya uhuru bado unaliona taifa changa, unategemea litakua na kukomaa baada ya miaka mingapi??
Kwa taarifa yako taaifa hili sio changa ni kilui lui
 
mimi nakusaida-wametaifisha majengo na ardhi iliyoshikiliwa hayo majengo,eneo la ardhi lolote pembeni na madarasa,mabweni na dining ni mali ya kanisa.nishasoma shule ambapo madarasa,dining,na mabweni ni mali ya serikli,ila maeneo ya pembeni kanisa walikuwa na bado hadi leo wanayatumia hayo maeneo kwa matumizi yao binafsi.
Yafaa serikali izirejeshe kwa wenyewe shule zilizokuwa zimeaifishwa kwani sababu za kutaifishwa sasa hazipo. Shule za serikali sasa ni nyingi na ziko katika kila kata. Hatua hii itamaliza mivutano ya kiimani iliyoko sasa ambapo baadhi ya wanafunzi kwa kuchochewa na wasiolitakia mema taifa letu wanautumia mwanya huu kupenyeza ghasia. Kila dhehebu na asasi warejeshewe shule zao ili ziendeshwe kwa malengo wanayotaka mradi wanazingatia sheria.
 
Hata ingekuwa hivyo si mbaya(japo najua sivyo_)kwani shule za kiislam zilizotaifishwa ni chache sana ukilinganisha na za Kikristo.

Swala siyo wingi au uchache wa shule zilizotaifishwa,hoja ni kwamba zilitumika Sheria mbili tofauti katika kuzitaifisha? Usijibu hoja usizozielewa, waachie wanaojua wajibu.
 
Back
Top Bottom