Mbunge Ngassa Akichangia Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2024 - 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Mbunge Ngassa Akichangia Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2024 - 2025

"Mwaka 2000 wakati tunaweka Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2000 - 2025 kama Taifa tuliweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha tunapambana na umasikini na kukuza uchumi. Tulianza na mkakati wa kupunguza umasikini (Nation Poverty Reduction Strategy Paper), tukaja MKUKUTA I & II na sasa tupo Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa 2021 - 2026" - Mhe. Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga

"Malengo Makuu 5 ya Dira ya Maendeleo ya Taifa; Kuboresha hali ya maisha ya watanzania; Kuwepo Mazingira ya Amani, Usalama na Umoja; Kujenga Utawala Bora; Kuwepo kwa Jamii Iliyoelimika na Kujifunza; na Kujenga uchumi imara unaoweza kukabiliana na ushindani kutokana na nchi nyingine" - Mhe. Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga

"Mambo ambayo yamekuwa yakituvuta miguu katika kuhakikisha Taifa letu linakimbia katika kufikia malengo ya mpango wa Maendeleo ya Taifa na Mipango ambayo tumekuwa tunajiwekea na leo tupo katika mpango wa tatu wa Taifa" - Mhe. Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga

"Jambo linalotushika miguu kama Taifa ni Urasimu kwenye sekta ya Umma. Serikalini kuna urasimu mkubwa sana Jambo ambalo limekuwa linatukwamisha sana katika kukimbia. Ofisi ya Umma, Jambo la kufanyiwa maamuzi siku mbili au tatu linakaa zaidi ya wiki 2 mezani" - Mhe. Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga

"Miundombinu ya kiuchumi, hii ni mishipa ya damu katika uchumi wa Taifa letu. Suala la Umeme, Barabara, Reli, Mawasiliano na huduma za kifedha. Kwenye mpango wa Taifa wa Maendeleo, Serikali mwende mkasimamie mradi wa Mwalimu Nyerere Hydro Power Project likamilike tuanze kuzalisha Umeme wa uhakika" - Mhe. Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga

"Uzalishaji wa Umeme kwa njia ya Mafuta umekuwa na hasara kubwa sana kwa wawekezaji ndani ya nchi hii na katika ukuzaji wa uchumi ni jambo ambalo limekuwa likitutia hasara na gharama ya uzalishaji imeongezeka matokeo yake tunawatia hasara wawekezaji wetu na wazalishaji na pia tunaathiri uchumi wa Taifa letu" - Mhe. Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom