Hoja ya Mpina kuhusu upasuaji wa kuongeza makalio yazua mjadala Bungeni

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
MJADALA mkali umeibuka bungeni kuhusu upasuaji kurekebisha maumbile, ikiwamo kupunguza au kuongeza ukubwa wa makalio katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa (CCM), ndiye aliyeibua zogo bungeni jijini, alipotoa hoja kwamba MNH-Mloganzila imeanzisha huduma hiyo kinyume cha Sera ya Taifa ya Afya ya Mwaka 2007.

"Hakuna mahali kwenye Sera ya Afya yetu ya Mwaka 2007 imeruhusu jambo hili. Operesheni ya matibabu, operesheni kwa ajili ya kuongeza makalio; ni operesheni ya kimapambo (cosmetic surgery), si ya mtu ambaye ana changamoto yoyote ile ya afya.

Baada ya Mpina kutoa kauli hiyo, Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby, alisimama na kumpa taarifa Mpina, akisema hata kiuno kikikaa vibaya nayo ni changamoto ya kimatibabu.

"Kwahiyo, kukiweka kiuno vizuri, ni kusababisha binadamu atembee vizuri na aweze kuwa na umbo zuri," alisema Shabiby.

Hata hivyo, Mpina alikataa kupokea taarifa hiyo ya mbunge mwenzake, akisisitiza serikali imeanzisha huduma hiyo bila kibali cha Bunge wala hakuna sheria, kanuni na mwongozo wa utoaji huduma hiyo.
 
Kwa mtu anae jitambua hii ni pretty issue. Sio hoja yakulazimisha bunge liache mambo ya msingi lianze kujadili hii issue.

Na plastic surgery inaenda beyond kuongeza shape/Matrako kama mpina anavotaka kuijadili hio hoja
Suala la afya ya wananchi isn't a petty issue. Kusipokuwa na usimamizi thabiti side effects zikianza kutokea tutaanza tena kulaumu.
 
Kwa mtu anae jitambua hii ni pretty issue. Sio hoja yakulazimisha bunge liache mambo ya msingi lianze kujadili hii issue.

Na plastic surgery inaenda beyond kuongeza shape/Matrako kama mpina anavotaka kuijadili hio hoja
Hoja yake iko sawa,, lazima vitu hivi viwekewe kanuni ilinkudhibiti watu kuuawa au kuibiwa pesa hasa private hospital zikianza kufanya hivyo
 
Huyo mpina ni takataka, kuna watu wanapata ajali za moto, wanahitaji juduma hizo kuweka sura zao sawa, yeye akili yake imekaa kuwaza makalio tu
Chiembe nakupa onyo uache mara moja kukosoa serikali ya awamu ya tano na washirika wake la sihivyo tutaanika ya upande wako yote na washirika wako pale ghorofani.
 
Huyo mpina ni takataka, kuna watu wanapata ajali za moto, wanahitaji juduma hizo kuweka sura zao sawa, yeye akili yake imekaa kuwaza makalio tu
Hata hoja yake hujaisikiliza na kuielewa wewe unakurupuka tu kujibu

Huyo aliyeungua si ni mgonjwa huyo, Mpina anaongelea mtu asiye na ugonjwa ila kaona hana tako anataka kuliongeza ana nyonyo ndogo anaenda kuongeza na anasema hii surgery haipo kwenye sera ya ya taifa kiasi kwamba mtu akipata madhara hawezi kusaidika maana kitu kisichotambulika kimechomekwa tu
 
Jimboni kwake kuna mambo mengi ya kufanyia kazi, kama hilo halimuhusu, apite kule. Nchi lazima isonge mbele katika masuala ya sayansi
 
Huna akili, Huwa Nashangaa wajinga
Huyo mpina ni takataka, kuna watu wanapata ajali za moto, wanahitaji juduma hizo kuweka sura zao sawa, yeye akili yake imekaa kuwaza makalio tu
kama wewe kupingana na MPINA .

Kuna wakati ,Midomo yenu mikubwa inabidi muiunganishe na Ubongo wenu Mdogo, ndo sasa muongee.

Kwa mfano, wee ni Mwanamke , una matiti madogo, umehisi ukiwa na matiti makubwa ndio utavutia, unaamua kwenda Mloganzila kuongeza Matiti ..unaenda Mloganzila wanaofanya Augmentation Mammoplasty ,unakua na matiti makubwa ......... Hapa Ndio MPINA anasema, Hamna Sera Wala Sheria Wala Kanuni ya Afya, itakayomlinda mteja wa aina hii.

Mpina anahitaji Suala kama hili, litungiwe Sera, Sheria !!.

Mfano...

Umepata Ajali, Pua haieleweki, unafanyiwa Rhinoplasty .... Hii ni sahihi kisera hata Sasa, na sio ambayo MPINA anazungumzia.
 
Huyu mpina achana naye, mganga wake wakati anagombea 2020 hajamlipa, kwa hiyo hapo alipo anarogwa na mganga wake ili afitinike na wananchi na chama chake.

Sasa hivi mganga wa Mpina anamuhudumia yule jamaa aliyekuwa mshindani mkubwa wa Mpina. 2025 hatoboi.

Na wewe unawaonea wivu hao wamekuwa habari ya mjini kwa kuweza kufanya operesheni za aina hiyo, umeishia kuandika maneno uliyokaririshwa tu
 
Kwa mtu anae jitambua hii ni pretty issue. Sio hoja yakulazimisha bunge liache mambo ya msingi lianze kujadili hii issue.

Na plastic surgery inaenda beyond kuongeza shape/Matrako kama mpina anavotaka kuijadili hio hoja
Hoja yake ni ya msingi, vipaumbele vyetu kuhusu afya ni vipi? Ni muhimu kuipenda miili yetu tuliyopewa na Mungu au kuibadilisha kwa operesheni?

Wanawake inabidi wajiamini vile walivyo. Labda kama mnene tumia diet kidogo sio operesheni.
 
Hata hoja yake hujaisikiliza na kuielewa wewe unakurupuka tu kujibu

Huyo aliyeungua si ni mgonjwa huyo, Mpina anaongelea mtu asiye na ugonjwa ila kaona hana tako anataka kuliongeza ana nyonyo ndogo anaenda kuongeza na anasema hii surgery haipo kwenye sera ya ya taifa kiasi kwamba mtu akipata madhara hawezi kusaidika maana kitu kisichotambulika kimechomekwa tu
Akikuelewa unitag,maana wananchi wengi wana mihemko ya kibaiolojia mkuu.usije Kuta unabishana na mdada😜 hii ndo JF
 
Hoja yake iko sawa,, lazima vitu hivi viwekewe kanuni ilinkudhibiti watu kuuawa au kuibiwa pesa hasa private hospital zikianza kufanya hivyo

Pia kusaidia kulinda ushahidi. Sasa pata picha shahida anaambiwe afanye utambuzi kwa mtu aliyekuwa hana tako, ghafla anakutana na mtu mwenye minitako kama yote. Lazima kesi ziwe ngumu. Kanuni muhimu.
 
Back
Top Bottom