SPIKA TULIA ACKSON: Tujadili vitu vya muhimu Bungeni Ila sio Kuuliza kuhusu Maswala ya vyoo

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,580
17,686
Hayo ameyasema leo wazi Ikiwa ni muendelezo wa kile kinacholalamikiwa na Wananchi kwa wabunge kuuliza maswali mepesi Bungeni huku maswali magumu na ya Kimaendeleo wakiyaacha na kuogopa kuyauliza ....

Spika Dkt Tulia ameongea Hayo baada ya waziri Dugange kujibu swali lililokuwa linauliza Upungufu wa Vyoo Kwenye zahanati..

"Wabunge hapa wameuliza kuhusu vyoo na wewe (Naibu Waziri Dugange) kwenye majibu yako ukatoa majibu, nafikiri kwa nchi yetu tulipofikia ni mahali ambapo hatutakiwi kuwa tunazungumza vyoo kwenye zahanati, choo kimoja pale vyoo viwili pale, serikali inafanya kazi sana na kuna mambo mengi sana ya kujibu na Kuyaongelea na hakuna sababu ya kujadili vyoo humu ndani," - Spika wa Bunge, Dkt @TuliaAckson

HIli jibu limefanya niendelee kuona Huenda bunge letu linaweza kurejea kwenye ajenda maalumu za kitaifa kuliko kujadili Vitu ambavyo wananchi wanaona havina msingi
Screenshot_20240215_133014_X.jpg
 
Spika amewaza Serikali imemnunulia V8 la Nusu Bilioni na huku kuna Mashule na Taasisi za Serikali hazina Vyoo, huenda nafsi imemsuta akaona azime mjadala kibabe...
 
Watu wanahitaji vyoo mashuleni, hospitalini

Waache porojo, tunauliza kulingana na mahitaji yetu.
Unasahau Bado sukari ni adimu watu wanakufa kwa njaa, Pesa mtaani haionekani..
Kuna matatizo mtaani mengi sana kuliko Hilo la choo..
Rejea Ziara ya Makonda..

Kwahyo Kuanza kuuliza swala la Chooni mahospitali wakati Kuna matatizo makubwa zaidi ya hayo sio sawa..

Kwa mpanga bajeti mzuri Ni muhimu Kuyapanga matatizo katika Vipengele vya uhitaji au umuhimh wake (Priotization)..

Hata katika familia yako Huwezi kununua Nguo Kibao wakati hakuna Chakula ndani, cha kwanza nunua chakula halafu fikiri mavazi na malazi..
 
Umuhimu si ni matokeo ya uhitaji? Watu wanakula, vyoo ni muhimu kama havipo hilo ni tatizo.

Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo.
Sasa kuna mtu anaenda kula Hospitali?
Malalamiko.Hospitali kuna Matundu mawili.au moja..
Sasa wewe unakula ili uende ukatoa haja zako.Hospitali??

Hii hoja sijaielewa
 
Unasahau Bado sukari ni adimu watu wanakufa kwa njaa, Pesa mtaani haionekani..
Kuna matatizo mtaani mengi sana kuliko Hilo la choo..
Rejea Ziara ya Makonda..

Kwahyo Kuanza kuuliza swala la Chooni mahospitali wakati Kuna matatizo makubwa zaidi ya hayo sio sawa..

Kwa mpanga bajeti mzuri Ni muhimu Kuyapanga matatizo katika Vipengele vya uhitaji au umuhimh wake (Priotization)..

Hatakatika familia yako Huwezi kununua Nguo Kibao wakati hakuna Chakula ndani, cha kwanza nunua chakula halafu fikiri mavazi na malazi..
Wakati bunge lina jadili "uongezaji wa makalio" akili bandia, vipi aliwakumbusha wabunge kuwa hivyo sio vipaumbele.

Sukari, vyoo n.k yote yapewe usawa
 
Aunganishe na Upi mkuu..
Kama upo mwingine kama huu ni sawa
 
Ooh ni sawa nilikuwa sijaona
 
Watu wanahitaji vyoo mashuleni, hospitalini

Waache porojo, tunauliza kulingana na mahitaji yetu.
Naungana na Spika, hata kama hizo changamoto zipo, bado mbunge anaweza kuziwasilisha kwenye vikao vya madiwani, sio bungeni,

Ingekuwa ushauri wangu, jukumu la ujenzi wa vyoo iwe zahanati au shule, lielekezwe kwenye halmashauri kupitia own source zake
 
Hayo ameyasema leo wazi Ikiwa ni muendelezo wa kile kinacholalamikiwa na Wananchi kwa wabunge kuuliza maswali mepesi Bungeni huku maswali magumu na ya Kimaendeleo wakiyaacha na kuogopa kuyauliza ....

Spika Dkt Tulia ameongea Hayo baada ya waziri Dugange kujibu swali lililokuwa linauliza Upungufu wa Vyoo Kwenye zahanati..

"Wabunge hapa wameuliza kuhusu vyoo na wewe (Naibu Waziri Dugange) kwenye majibu yako ukatoa majibu, nafikiri kwa nchi yetu tulipofikia ni mahali ambapo hatutakiwi kuwa tunazungumza vyoo kwenye zahanati, choo kimoja pale vyoo viwili pale, serikali inafanya kazi sana na kuna mambo mengi sana ya kujibu na Kuyaongelea na hakuna sababu ya kujadili vyoo humu ndani," - Spika wa Bunge, Dkt @TuliaAckson

HIli jibu limefanya niendelee kuona Huenda bunge letu linaweza kurejea kwenye ajenda maalumu za kitaifa kuliko kujadili Vitu ambavyo wananchi wanaona havina msingi
View attachment 2904864
Sawa mh Spika, jadilini ndege za kupeleka waheshimiwa kutibiwa vyoo watoto na wagonjwa watajisaidia porini kirahisi tuu.
 
Sasa kuna mtu anaenda kula Hospitali?
Malalamiko.Hospitali kuna Matundu mawili.au moja..
Sasa wewe unakula ili uende ukatoa haja zako.Hospitali??

Hii hoja sijaielewa
Wewe huwa unakula na kunya hapo hapo kama Nzige? Au mwenzangu wewe huwa unakula na vinatoka hapo hapo?

Hujiongezi kabisa ukajua kwamba mgonjwa anaweza kuwa alikula kwake na muda wa kwenda chooni ukafika akiwa hospitali?

Umeniuliza swali la kijinga sana!
 
Back
Top Bottom