Habari Mbaya kwa Watu Wote kama ilivyoandikwa na 'Raia Fulani'

Raia fulani, honestly nimependa presentation ya ujumbe. Kwa kuwa wengi wa watu wangu hawafiki hapa najiruhusu kucopy na kuwatumia watu wengi kadri iwezekanavyo. Hata wavivu wa kusoma hii hawataiacha. Na ujumbe utakuwa umewafikia wengi zaidi.
 
Raia fulani, honestly nimependa presentation ya ujumbe. Kwa kuwa wengi wa watu wangu hawafiki hapa najiruhusu kucopy na kuwatumia watu wengi kadri iwezekanavyo. Hata wavivu wa kusoma hii hawataiacha. Na ujumbe utakuwa umewafikia wengi zaidi.

Mkuu hii bila shaka ni sehemu ya M4C. Kila la heri
 
Pole dada yangu usiwe mnyonge, hili joto ni humu JF tu,
Mtaani pametulia hawajui hata kinachoendelea. Ndo maana JK akasema ni Upepo tu.

Kumbe hata nyie mnakiri kuwa jk alisema hivyo? Ila mjue kuwa kama hili joto halisikii basi muwahisheni Apollo
 
Hakuna upendo mzuri zaidi ya huu uliouonesha kwa wanajamii wenzako,japo wengine tumebaki na huzuni sana juu ya kile serikali ya ccm inafanya
 
Ikawa siku ile mbele ya Baraza la saba la kutunga haki akatokea mfuasi machachari kati ya wale wazee 323 wa Baraza akasema, “Je, hawa watajwao kati yetu hawajafanya kosa? Tazama mikono yao ilivyochafuka damu. Wamezitapanya nyara za wana wa nchi na kurarua vifua vyao na kuziteketeza roho za wapiga kura wetu. Wametapanya chakula na kujiogesha na mvinyo wa gharama. Wameivika mioyo yao uziwi na upofu hata wasisikie vilio vya wana wa nchi. Wamezini na kufanya uasherati juu ya katiba na sheria na sera na taratibu na kanuni tulizojiwekea. Je, haiwapasi watu hawa kufungwa jiwe la kusagia shingoni mwao na kutoswa baharini?”

Ndipo kiongozi wa Baraza aliposimama na kusema, “Lawezaje hili kutendeka, nasi hatuna mamlaka toka juu? Yeye aliyewakweza ndiye atakayewatweza.”

Neno likamjia tena Yule mfuasi machachari kusema. Naye akajawa na Roho wa ujasiri na kunena, “Mama yangu na mkubwa wangu, kama itapendeza mbele ya nafsi yako adhimu, nilete hoja mbele yako y
 
ni yupi kati yenu ambaye mwanawe akimuomba Yai, yeye atampa N'ge au akimuomba Samaki, yeye atampa Nyoka?

Basi imenipasa kumpa Credit, Thanx na vyeo vyoote Raia Fulani kwa madini alotema.
 
Mkuu uko juu. Unaonyesha ni jinsi gani ulivyo great-thinker maana umetoa mafichoni niliko nije nikupe tano kisha nirudi tena mafichoni. Mkuu nakala yako kama ufunuo, mkuu unatisha.
 
du naomba uwe mwandashi wa riwaya zitasaidia sana jamii mfano wa hii hasa wanajamii wagumu wa mioyo mfano ccm asante sana umerudisha furaha yangu aliyoiondoa pinda j3.
 
Asanteni wakuu kwa credits. Kwa kumjibu Fered na wengine ni kuwa tasnia ya uandishi wa riwaya bongo hailipi. Njia pekee niliyoona inafaa kupitia ni filamu. Na hili lipo kazini sasa.
 
Aksante Raia Fulani kwa waraka unaoongeza mwamko wa kisiasa na uamsho wa kiroho. Kwa namna uovu unavyolelewa na kulindwa katika kipindi hiki cha mwisho cha ile miaka mitatu kabla ya kuharibiwa kwa CCM, tutegemee mwamko mpya wa kisiasa na uamsho mpya wa kiroho kwani dola ya Tanzania sasa inadidimia.

Ameshatokea kijana mmoja ambaye aliitwa na Mungu na kuonywa juu ya uovu wa makuhani na viongozi wa Dola hii, kinachosubiriwa sasa ni ............... ili lile andiko litimie. Hakika, Uovu usiotubiwa husababisha taifa, jamii, au mtu binafsi kuangamia.

Tujiandae kama Taifa! Tusimame, nasi tuseme chochote kupinga uovu huu. Tusiwaogope wao la sivyo tutafanywa tuwaogope. Leo tumefanywa kama mji wenye ngome, nguzo za chuma na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya uongozi mbovu wa nchi hii, dhidi ya serikali dhalimu ya Tanzania, maafisa wake, makuhani wake na wafuasi wao. Watapigana nasi lakini hawatatushinda, kwa kuwa MUNGU yupo pamoja NASI
 
RF a great thinker.makala safi sana.
Wana wa nchi yenye asali na maziwa,tazama tunaangamia kwa kukosa maarifa!Mungu anatutazama kutoka mahali pa juu palipoinuka na kutuonea huruma.Ni lini tutatumia akili,uwezo,ujasiri na maarifa alotupa kunusuru taifa hili na viwavi hawa?
 
Raia flani kwakweli wewe ni mkali tena sio kidogo.....hongera sana una maono ya uchambuzi wa mambo bayana..great thinker!!!
 
Asante kwa makala isiyochosha yenye maandiko ya kutafakari, ss 2nahitaji m2 kama mussa aje a2komboe kutoka kwenye huu utawala wa farao. Nami nasema ikawa 2010, ikawa 2015 UKOMBOZI UMEFIKA.
 
Ikawa siku ile mbele ya Baraza la saba la kutunga haki akatokea mfuasi machachari kati ya wale wazee 323 wa Baraza akasema, “Je, hawa watajwao kati yetu hawajafanya kosa? Tazama mikono yao ilivyochafuka damu. Wamezitapanya nyara za wana wa nchi na kurarua vifua vyao na kuziteketeza roho za wapiga kura wetu. Wametapanya chakula na kujiogesha na mvinyo wa gharama. Wameivika mioyo yao uziwi na upofu hata wasisikie vilio vya wana wa nchi. Wamezini na kufanya uasherati juu ya katiba na sheria na sera na taratibu
na kanuni tulizojiwekea. Je, haiwapasi watu hawa kufungwa jiwe la kusagia shingoni mwao na kutoswa baharini?”

Ndipo kiongozi wa Baraza aliposimama na kusema, “Lawezaje hili kutendeka, nasi hatuna mamlaka toka juu? Yeye aliyewakweza ndiye atakayewatweza.”

Neno likamjia tena Yule mfuasi machachari kusema. Naye akajawa na Roho wa ujasiri na kunena, “Mama yangu na mkubwa wangu, kama itapendeza mbele ya nafsi yako adhimu, nilete hoja mbele yako ya kumfunga shingoni jiwe la kusagia kiongozi wa mawaziri hawa walio mbele ya Baraza lako tukufu. Huyu tuna mamlaka naye. Na huyu tukushamtosa ndani ya kina cha Nungwi, itampendeza mkuu wa nchi kuvunja Baraza lao na kutenganisha kati ya ngano safi na magugu.”

Ndipo kiongozi wa Baraza aliposimama tena huku akiwa amejawa na ghadhabu. Akasema, “Ewe mfuasi mtukutu, mawazo yako yamejaa ubatili, nayo yanaelekea kushindwa.” Akafungua juzuu lililoko mbele yake na kusoma toka huko haya yafuatayo;


  1. Mwanabaraza yoyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa kiongozi wa Baraza ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na kiongozi wa mawaziri kwa mujibu wa aya ya 53A ya juzuu hii;
  2. Hoja yoyote ya kutaka kupitisha Azimio la kumtosa kiongozi wa mawaziri kwenye kina cha Nungwi haitatolewa mbele ya Baraza endapo;
    • Haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya kiongozi wa mawaziri yaliyoainishwa katika aya ya 52 ya juzuu;
    • Hakuna madai kwamba kiongozi wa mawaziri amevunja sheria ya maadili ya utumishi wa juu, ya wana wa nchi;
    • Haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa; au
    • Haijapita miezi tisa tangu hoja kama hiyo ilipotolewa mbele ya Baraza na Baraza likakataa kuipitisha.
  3. Hoja ya kutokuwa na imani na kiongozi wa mawaziri haitajadiliwa na Baraza kama;
    • Taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na wanabaraza wasiopungua asilimia 20 ya wanabaraza wote itatolewa kwa kiongozi wa Baraza, siku zisizopungua 14 kabla ya siku iliyokusudiwa kuwasilishwa mbele ya Baraza…

Nazo siku zilizosalia zilikuwa tatu tu ili Baraza liahirishwe hadi mwezi wa sita wa mwaka.
Ikawa Yule mfuasi machachari aliposikia hayo, kwa hali ya unyenyekevu kabisa akasimama tena na kunena na kiongozi wa Baraza. Akamwambia, “Kama juzuu isemavyo, Niruhusu mimi na wenzangu 70 miongoni mwetu tukuletee majina na sahihi zetu panapo siku ya Jumatatu ili zipate Baraka na kibali mbele yako ya kutekelezwa kwa hoja yetu yenye azma ya kumtosa kiongozi wa mawaziri katika Baraza lijalo.”

Naye kiongozi wa mawaziri huku akijua anawindwa ili kutoswa kina cha Nungwi, akafanya hila na kupenya kati yao akaenda mahali panapo utulivu huku akifanikiwa kuwakutanisha wale alio na nasaba nao. Akawaambia, “Nafsi yangu imejaa ukiwa hata natamani kulia. Ama nilie?”

Nao wafuasi wale wakamsihi sana asilie, ndipo alipotulia na kuwaambia, “Chombo chetu ki katika maji ya kina kirefu cha bahari. Nayo bahari imeghadhabika. Mawimbi yanakipiga chombo, nacho kinakaribia kuzama kutokana na wingi wa shehena. Tukimwaga shehena yote baharini hatutapata chakula cha kutufikisha Pwani. Tutafia majini. Sasa basi, kwa kuwa bado chombo kimelemewa, nasi ni wengi himu chomboni, na tupige kura kwa watu nane hivi ili nao tuwatose baharini.”

Ikawa yapata majira ya saa sita hivi usiku hata zoezi la kuwapata wale nane lilipokamilika. Wale wafuasi waliobakia wakawafunga wale nane kwa kamba kuzunguka miili yao. Nao wale waliosalimika wakasimama kwa ahueni na hudhuni, Wakawa wakisubiri amri ya kuwasukumia wale nane baharini toka kwa kiongozi wa mawaziri, ambaye nae alionekana kujawa na huzuni sana moyoni.

Na tazama, sauti ikasikika toka katika kipaza sauti ndani ya kile chombo. Nao wakataharuki Wakawa wakiisikiliza ile sauti. Sauti ikasema, “Hamna mamlaka ya kutoa uhai wa wenzenu. Mimi ndiye mwenye mamlaka hayo! Tazama, kama itampendeza Yule aliye juu kabisa, dhoruba hii itapita na mambo yatakuwa shwari. Wafungueni wenzenu na muwaache huru. Rudini Barazani walipo mahasimu wenu nami nitatoa maelekezo ya nini cha kufanya.”

Ikawa usiku ikawa asubuhi siku ya Jumatatu. Ndipo Baraza lilipokusanyika tena wakiwapo wale manusuru ambao bado walionekana wangali wakiweweseka. Naye mkuu wa Baraza akaketi mahali pa juu kabisa. Mahali pa mamlaka. Naam, mahali palipotukuka. Naye akishakukaa akatoa dua, kisha agizo kwa Baraza kuanza.

Nalo Baraza likaanza kuchambua hoja moja baada ya nyingine kwa mapana na membamba na marefu na mafupi yake, na wala pasionekane lolote lililo jipya kati ya yote yaliyozungumzwa.

Ikawa asubuhi ikawa mchana siku hiyo ya Jumatatu. Naye mkuu wa Baraza akiwa na mamlaka rasmi, alisimamisha Baraza na kuwapa wanabaraza muda wa kutosha wa kwenda kuongeza uhai.

Ikawa mchana ikawa alasiri siku hiyo ya Jumatatu. Na wana wa nchi toka pande zote wakatega macho na masikio yao katika vyombo rasmi na visivyo rasmi vya taarifa, wakisubiri kwa hamasa na ari na shauku na tashwishi na kiwewe, kuona hukumu ya haki iliyotabiriwa kutokea. Nao wana wa Jamiiforums walikuwa mstari wa mbele katika kupashana habari juu ya yale yanayoendelea ndani ya Baraza lile tukufu.

Nao wanabaraza wakapewa tena muda wa kuwasulubu wale manusuru kwa hoja na takwimu na data na ushahidi, ya kwamba ni kwa nini wasifungwe

mawe ya kusagia na kutoswa baharini? Na yote haya yangetekelezwa kwa namna ambayo ingempendeza Jemedari mkuu kuyatolea maamuzi.

Na muda wao ulipokoma, ndipo mkuu wa Baraza aliposimama na kuwapa manusura muda wa kujitetea. Nao wakajitetea kwa hoja na hisia na huruma, ya kwamba ni chuki na ghiliba na vijiba vya roho na husuda na vivu wa wachache waliokosa nafasi hizo adhimu ndio sababu ya wao kupendekezwa kutoswa baharini kwa namna ambavyo ingempendeza Jemedari mkuu kuyatolea maamuzi.

Lakini wanabaraza huku wakijawa na jazba na ghadhabu walipiga kelele wakisema, “Na watoswe baharini! Watoswe baharini!”

Nao umagamba ukaufanya moyo wa mkuu wa Baraza kuwa mgumu, wala asisikilize kilio cha wanabaraza. Akasema, “Niliyosema, nimeshayasema! Ni kwa namna ambayo itampendeza Jemedari mkuu pekee kuyatolea maamuzi. Nami ndiye mwenye kauli ya Mwisho miongoni mwenu.”

Haya yote yalitokea na kutendeka ili lile neno lililoandikwa lipate kutimia.

Nalo ni hili;

Ee mkuu mfalme wa kisasi
Mfalme wa kisasi uangaze!
Mwenye kuhukumu nchi, ujitukuze
Uwape wenye kiburi stahili zao.

Mkuu hata lini wasio haki,
Hata lini wasio haki watashangilia?
Ee mkuu wanawaseta watu wako
Wanawatesa warithi wako

Nao husema, mkuu haoni
Mfalme wa wote hafikiri
Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini
Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?

Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?
Aliyelifanya jicho asione?
Awaadhibuye mataifa asikemee?
Amfundishaye mwanadamu asijue?

Lakini mkuu amekuwa ngome kwetu
Na Mfalme wetu mwamba wetu wa kukimbilia
Naye atawarudishia uovu wao
Atawaangamiza katika ubaya wao
Naam, mkuu, Mfalme wetu atawaangamiza.

Nao wana wa nchi wakiwa hawaamini kwa kile kinachotokea mbele ya macho na masikio yao, ndipo Yule mwana mpendwa wa mkulima, mkuu wa mawaziri aliposimama na kuijongelea mimbari kwa ajili ya kutoa neno la hitimisho. Nayo maneno mengi yakamtoka kinywani. Maneno yaliyoandikwa juu ya gome. Naam, maneno mengi.

Hapo ilikuwa yapata saa moja usiku, nae alikuwa Akiendelea kushukuru na kupongeza na kushauri na kukemea na kusisitiza na kusihi, wala asijue kuwa wana wa nchi walikuwa na kiu nyingine. Kiu ya kusikia jambo jipya. Kiu ya kusikia habari njema.

Hata alipofikia tamati, hapakuwako na neno lolote la kuwafariji wana wa nchi kwa maana walitamani mioyoni mwao kusikia, “Yanipasa kujivua gamba”, wala wasisikie.

Naye akiisha kusema hayo, akahitimisha kwa kuahirisha Baraza la saba hadi mwezi wa Juni wa mwaka bila kwa neno la matumaini kwa wana wa nchi. Ndipo waliposema, “Hakika mwana wa mkulima mwoga!”
Raia fulani uko vizuri...hongera kwa ustadi wako...naomba niichukue kwa matumizi yangu binafsi na kila nitakapo itumia nita ku acknowldge...! ushauri..andika kitabu kwa staili hii kuanzia kuanguka kwa nywele nyeupe mpaka hapa tulipo zaidi ya kuielimisha jamii naamini na kipato chako kitapanda...na siku nikiwa waziri wa elimu kupitia serikali ya chadema nita kirecommend kitabu hicho kutumika mashuleni katika masomo ya siasa na fasihi!
 
Kisha sauti ya Bwana ilinijilia mimi Baby mwana wa Kailama ndani ya beseni :bathbaby: katika hema la Magwepande ikinena,

"Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu, usitumie nguvu na rasilimali zako nyingi kutegemea mabadiliko toka vinywa vya wazee wa Baraza huko Mjengoni, wala usiketi muda mrefu katika jukwaa la Siasa la Mtandao wa Jamii wala kutumaini kauli ya Mh. Mwanasiasa awaye yote Mgombea, maana chemchem zao zi mikononi mwa aliyewapeleka". Liko neno moja linalokera, nalo ni kufunikwa au kusukumizwa nyuma sana mawazo ya wasio wapelekwa hapa mtandaoni, naam liko la pili ambalo ni chukizo kwa Bwana, nalo ni kupinga juhudi za kweli za Ukombozi kwa kutumia msamiati mgumu na kuanzisha mada za kukanganya kila mara Wananchi wanapotaka kuchukua hatua.


Ilitabiriwa kuwa katika mwaka wa mwisho wa kutawala kwake Mfalme, watashuka kutoka Makumbusho kuanzisha mada motomoto na kulaghai umma kuwa wanachukiana ili kufisha akili zenu. Wengi watabweteka kuwa khali sasa ni shwari bali ukweli itakuwa ni kujilisha upepo mbele ya mwendo wa mwanamke mzinzi aonekanaye shujaa ambaye hula akapangusa kinywa chake na kusema sikufanya chochote!
 
Raia Fulani umenifanya niludi nyuma na kujifikilisha kuhusu kufikilia na kupitia picha kuwa HAKI ucheleweshwa tu na wala HAIZUIWI.Hakika mtu anaposoma wakara wako anapata msisimko fulani wa kiroho ni hapo kwa walio wakristu wanapata moyo wa simulizi za DAVID v/s GOLIATH.

Hakika kaa chini utengeneze kitu [Kitabu hata cha page mia] uonyeshe awamu zote nne [BB/Julius, Mzee wa Ruksa Mwinyi, Mzee wa Ubinafsishaji zoezi la kufilisisha umma Mkapa,na sasa Mzee wa Urafikisation na kifo cha CCM JK.I hope utaacha hazina ya aina ya vitabu vya fasihi MSOLOPAGAZI-my favorite, ALFU LELA ULELA , WAGAGAGIGIKOKO.

Umetuonyesha your hidden talent,manake UShakespeare huo tunauitaji kama hautatumika mashuleni kwa kuwa utakuwa unachochotea na kuhamasisha mioyo ya wapenda haki na walinzi wa Taifa basi utakuwa Lulu kwa waelevu vizazi na vizazi [Great Thinkers].

Please RF make it happen!!
 
Thanks Guys! Mawazo yenu nitayafanyia kazi japokuwa kutengeneza simulizi kama hizi inahitaji muda, taarifa, utafiti na pesa pia. Ila kwa ajili ya wana wa nchi, haya yatawezekana
 
Back
Top Bottom