Nao wana wa nchi wakiwa hawaamini kwa kile kinachotokea mbele ya macho na masikio yao, ndipo Yule mwana mpendwa wa mkulima, mkuu wa mawaziri aliposimama na kuijongelea mimbari kwa ajili ya kutoa neno la hitimisho. Nayo maneno mengi yakamtoka kinywani. Maneno yaliyoandikwa juu ya gome. Naam, maneno mengi.
Hapo ilikuwa yapata saa moja usiku, nae alikuwa Akiendelea kushukuru na kupongeza na kushauri na kukemea na kusisitiza na kusihi, wala asijue kuwa wana wa nchi walikuwa na kiu nyingine. Kiu ya kusikia jambo jipya. Kiu ya kusikia habari njema.
Hata alipofikia tamati, hapakuwako na neno lolote la kuwafariji wana wa nchi kwa maana walitamani mioyoni mwao kusikia, "Yanipasa kujivua gamba", wala wasisikie.
Naye akiisha kusema hayo, akahitimisha kwa kuahirisha Baraza la saba hadi mwezi wa Juni wa mwaka bila kwa neno la matumaini kwa wana wa nchi. Ndipo waliposema, "Hakika mwana wa mkulima mwoga!"
Angalau nashukuru kwa kunikubali
Thanks for your clarification mkuu. Wanajeshi wetu nao wamekuwa corrupted na system so wanachokifanya ni ku-preserve status quo.MNYISANZU. Popote pale penye mapinduzi ya kijeshi, wanajeshi wa kawaida ndiyo wahusika wakuu. Tena wenye vyeo kama kapteni na luteni ndiyo wafanya mapinduzi,kwani wao ndiyo wenye wanajeshi,kupitia vikosi.
Hivyo wanajeshi wetu hawana ujasiri kama tulivyo sisi raia wa kawaida.
Well said. Viongozi wa majeshi ndio kikwazo cha mapinduzi nchini. Wanajeshi wa kawaida wanataka sana kuipindua serikali ila viongozi wao ndio stumbling blocks.
Raia Fulani, YOU ARE A GREAT THINKER, Congrats!!
:violin::violin::violin::violin::violin:
Ee mkuu mfalme wa kisasi
Mfalme wa kisasi uangaze!
Mwenye kuhukumu nchi, ujitukuze
Uwape wenye kiburi stahili zao.
Mkuu hata lini wasio haki,
Hata lini wasio haki watashangilia?
Ee mkuu wanawaseta watu wako
Wanawatesa warithi wako
Nao husema, mkuu haoni
Mfalme wa wote hafikiri
Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini
Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?
Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?
Aliyelifanya jicho asione?
Awaadhibuye mataifa asikemee?
Amfundishaye mwanadamu asijue?
Lakini mkuu amekuwa ngome kwetu
Na Mfalme wetu mwamba wetu wa kukimbilia
Naye atawarudishia uovu wao
Atawaangamiza katika ubaya wao
Naam, mkuu, Mfalme wetu atawaangamiza.
Raia Fulani, YOU ARE A GREAT THINKER, Congrats!!
Kwani nchi kupinduliwa nani kakuambia ni habari mbaya?
Nchi kupinduliwa ni hatua moja kuelekea kwenye ukombozi.
Duniani kote, pale jeshi linapogundua serikali imeshindwa kuwatumikia wananchi, na kuna chama ambacho kinatetea maslahi ya umma lakini inashindwa kutokana na utawala wa mabavu, linaipindua hiyo serikali kandamizi, na kuikabidhi kwa wananchi kwa njia ya haki, kwa maana ya kufanya uchaguzi wa kidemokrasia, ambapo taratibu zote za uchaguzi unaratibiwa na jeshi.
Kwa mfano jeshi letu ukiacha Shimbo na Mwamunyange wakiwemo wafuasi wachache, wanaelewa jinsi serikali yetu ilivyoshindwa kuwatumikia wananchi, wanaelewa jinsi serikali yetu inavyowakumbatia waizi.