Gwajima: Taifa tumekosa maono, inakuwaje kujenga reli kabla ya kuchimba chuma? Waziri Mwigulu ampinga

Mimi nimejibu kama mchumi tena professsional yeye amezungumza kama layman asiyeelewa abc za uchumi



Mimi nimechangia kama,mchumi yeye amazungumza kama layman .
Ndio umuhimu wa watanzania mlioelimika kama wewe kuchukua point Kwa Hawa wanasiasa wachumia tumbo na kujenga hoja ya kukomboa taifa letu na kushauri njia sahihi
 
Upo off point na Mbunge, either hujamwelewa kabisa!! Yeye anachojaribu kusema ni kuwa shambani kwetu tayari Kuna nyanya na zinaweza kuvunwa na kuivishwa, hivyo katika kupika chakula inatakiwa ujitahidi utumie nyanya zako ulizovuna shambani!! Sasa swali lake ni iweje tukimbilie kununua nyanya Kwa jirani ilihali za kwetu zingeiva na kutumika kupunguza hasara hii kubwa ya manunuzi!? Tena Kwa Dola kutoka nje!!
Sidhani kama nyanya zimevunwa na zipo tayari ni kwamba eneo la kulima tunalo na maji ya kuwagilizia yapo...., cha kujiuliza tukienda kununua kwa jirani je ni gharama nafuu / ndogo kuliko tukilima sisi na kumwagilizia (ingekuwa bora kama tungelima na sisi tukamuuzia jirani ila kwa utunzaji wetu na gharama za bili za maji je tukishavuna tutaweza kuuza kwa bei anayouza yeye)?

Hayo ni maswali muhimu sana katika kungalia opportunity costs
 
Mbunge wa Kawe akiwa bungeni, Joseph Gwajima amesema kwa miaka mitano Taifa limelipa fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni 2.2, Gwajima amesema kwa mtu yoyote mwenye akili na anajua kuzitumia jambo hili hawezi kuruhusu kufanyika.

Gwajima amesema nchi imeanza na reli ambayo hayupo kinyume nayo lakini ameshangaa kuanza na reli ambayo 'component' kubwa ni chuma kwa kukiagiza nje ya nchi badala ya kuchimba chuma kisha kujenga reli.

Gwajima amesema kinachosumbua ni kukosa maono ya Taifa, mipango ya Taifa na dira.

Gwajima amesema Taifa linahitaji maono ya pamoja na hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa miaka mitano au kumi.

Kingu-Taarifa
Kingu akichangia kupitia taarifa, amesema hadi tume ya kutengeneza mipango ya muda mrefu imefutwa. Amesema Taifa halina tume ya mipango kuanzia miaka 50.

Mwigulu akanusha
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amekanusha na kusema Taifa lina mipango ya muda mrefu na tangu uhuru limeongozwa na viongozi wenye maono na ndio maana kuna dira ya 2025 kutoka kwa Mkapa.

Mwigulu amesema nchi imeongozwa kwa maono ndio maana ipo ilipo. Mwigulu amemaliza kwa kusema Rais ameshaweka utekelezaji wa miradi mikubwa, yote inaenda kutekelezwa ya Liganga, LNG.
Hiyo Gwajima hajui anachoongea hicho chuma kina Siasa zake za kitaalam ambazo ukisubiri hautakuja kujenga hiyo Reli, mbona hashangai tunachimba gas lakini bei ya kuinunua ikojuu?
 
Sasa pale nishati kalemani alikua na cheni ya upigaji wake wa mabilioni anzia kwenye nguzo hadi kwenye mafuta sasa january alivoingia kwanza kasafisha wandani wa kalemani wizarani na vitenda uchwara vya sub company zao so issue ikawa kalemani anampa mpina michongo ya pale then mpina anamlipua january hadi leo wakipata upenyo ni kumsagia kunguni january hata majadiliano ya wizara tofauti na nishati wao wako na january tu
Na.hii ndio sababu wanamchukia January.
 
Mawazo ya Gwajima ni potofu na ya unafiki. Kiuchumi sio lazima nchi iwe na chuma ndio ijenge reli wala hata kama ina chuma sio lazima kwanza kuchimba chuma ndipo nchi ijenge reli. Kila ntu sasa anajifanya mchumi!.
Ziko nchi nyingi tu zimejenga reli na hazina hicho chuma.

Unapotaka kujenga reli unatangaza tenda baada ya kuwa umefanya tathmini reli itajengwa vipi na costs ni kiasi gani. Mkandarasi akishapatikana ndiye anajua vyuma atanunua wapi na kwa bei gani; sisi tunachotaka tukabidhiwe reli iliyojengwa kwa viwango na kwa wakati.

Hicho chuma ikitokea kimechimbwa siku moja kitauzwa kwa wateja wanaohitaji wa nje na ndani ya nchi na kitaingiza mapato ya fexha za kigeni na pia shilingi.

Hakuna nchi inazalisha kila kitu yenyewe na sio lazima kiuchumi tuzalishe kila kitu, vingine tutaagiza tupende tusipende; ndio maana kuna kitu kinaitwa comparative advantage katika biashara ya kimataifa sio suala la kuzalisha tu
Wewe unadharaulisha sana ubongo wako,chuma kipo,hutaki kuchimba,unaagiza nje,ni akili hiyo?
 
Mawazo ya Gwajima ni potofu na ya unafiki. Kiuchumi sio lazima nchi iwe na chuma ndio ijenge reli wala hata kama ina chuma sio lazima kwanza kuchimba chuma ndipo nchi ijenge reli. Kila ntu sasa anajifanya mchumi!.
Ziko nchi nyingi tu zimejenga reli na hazina hicho chuma.

Unapotaka kujenga reli unatangaza tenda baada ya kuwa umefanya tathmini reli itajengwa vipi na costs ni kiasi gani. Mkandarasi akishapatikana ndiye anajua vyuma atanunua wapi na kwa bei gani; sisi tunachotaka tukabidhiwe reli iliyojengwa kwa viwango na kwa wakati.

Hicho chuma ikitokea kimechimbwa siku moja kitauzwa kwa wateja wanaohitaji wa nje na ndani ya nchi na kitaingiza mapato ya fexha za kigeni na pia shilingi.

Hakuna nchi inazalisha kila kitu yenyewe na sio lazima kiuchumi tuzalishe kila kitu, vingine tutaagiza tupende tusipende; ndio maana kuna kitu kinaitwa comparative advantage katika biashara ya kimataifa sio suala la kuzalisha tu
Bila shaka wewe ni mwanaccm.Suala alilosema Mch.Gwajima ni sahihi.Tungeokoa US$2.2 billion=Tshs ngapi?Hicho chuma cha Mchuchuma/Liganga pekee kingechimbwa kikamilifu ingefanya Tanzania ijenge reli hadi vijijini na wilayani badala ya kuhangaika na lami.Tungeweza kuwa na Network ya reli kuunganisha nchi yetu lakini kwa kukosa Dira/Maono ya Taifa tunaagiza chuma.
Tunazo raslimali za gesi asilia lakini tunaagiza gesi,mbolea na mafuta.Tanzania kuna uwezekano wa kuzalisha umeme wa jua,upepo,joto ardhi au biogas,lakini serikali inawaza tozo na kuongeza kodi.
Hakuna Dira/maono ya kitaifa na Mch.yupo sahihi,at least kwa hoja hiyo.
 
H
Wewe unadharaulisha sana ubongo wako,chuma kipo,hutaki kuchimba,unaagiza nje,ni akili hiyo?
Hata Nyerere aliamua, tusichimbe kwanza madini maana,hayaozi tusubiri hadi tutakapokuwa na,uwezo ili yaweze kutunufaisha. Nadhani unaelewa kilichotokea baada ya Nyerere kutoka madarakani, mikataba ya ovyo iliingiwa na awamu zilizofuata hasa ya JK ambapo ni kama wawekezaji walisomba madini burexkwa kulipa kodi kiduchu hafi JPM aliporekebisha mikataba ya madini ndipo walau tunapata kiasi cha kuridhisha.
 
Bila shaka wewe ni mwanaccm.Suala alilosema Mch.Gwajima ni sahihi.Tungeokoa US$2.2 billion=Tshs ngapi?Hicho chuma cha Mchuchuma/Liganga pekee kingechimbwa kikamilifu ingefanya Tanzania ijenge reli hadi vijijini na wilayani badala ya kuhangaika na lami.Tungeweza kuwa na Network ya reli kuunganisha nchi yetu lakini kwa kukosa Dira/Maono ya Taifa tunaagiza chuma.
Tunazo raslimali za gesi asilia lakini tunaagiza gesi,mbolea na mafuta.Tanzania kuna uwezekano wa kuzalisha umeme wa jua,upepo,joto ardhi au biogas,lakini serikali inawaza tozo na kuongeza kodi.
Hakuna Dira/maono ya kitaifa na Mch.yupo sahihi,at least kwa hoja hiyo.
Ndugu yangu uchumi hauko hivyo.
Natamani nikupe lecture lakini muda hauruhusu.
 
Wewe unadharaulisha sana ubongo wako,chuma kipo,hutaki kuchimba,unaagiza nje,ni akili hiyo?
Hatuna uwezo wa kuchimba, kuprocess na mtaji, kama unakumbuka hata kiwanda cha karatasi cha,Mgololo, Mufindi kilitushinda kuendesha.
 
Ok tuseme ana hoja kwanini iwe chuma tu? Pamba, dhahabu, almasi, Tanzanite, korosho na mengine mengi tu kwanini tusiwe na viwanda vyetu tuuze product sio raw materials. Kwani ukiwa na chuma ndio utajenda reli. Hapa tuna mbao kibao lakini furniture tunanunua toka nje kwanini? Kuuza raw materials haikufanyi kuuza bidhaa bora hatuna uwezo huo vibiriti vyetu mpaka kiwake umemaliza njiti 30. Nakubaliana na yeye kama nchi ni lazima tuwe na vision, tunataka kuwa nini wauzaji au watengenezaji.
Swali gani la ajabu unauliza. Kwani wapi kwenye katiba wamesema kuna mtu anaitwa Gwajima ndio anatakiwa kuzungumzia matatizo yote ya nchi hii?

Yeye kaamua kuzungumzia chuma, jibu hoja yake sio kuuliza kwanini hajazungumzia viberiti sijui pamba wala utapiamlo wa watoto wenu. Kwahiyo angesemea hiyo dhahabu napo ungekuja kuuliza mbona hajasema chuma?
Cha kusikitisha hizi akili ndizo mnatumia kuendesha familia
 
Kuna mambo ni magumu kufanyia uamuzi bila ku-dig deeper..., na katika hili suala tuakiacha Siasa kuna ingredients mbili za muhimu za kufahamu...

Je Production cost ya Tani moja ya Chuma mpaka inakuwa tayari ni kiasi gani ?
Je Tani hio ikinunuliwa inaponunuliwa mpaka kuletwa hapa ni kiasi gani ?
Je uchimbaji na utayarishaji wa hicho chuma hapa mpaka kinaenda sokoni kitaleta faida ya kiasi gani kama tukiuza bei sawa na washindani wetu ?

Hapo ndio naweza kuchangia vizuri nini kifanyike nikipata hizo data....

Nadhani ni vema kumalizia na Msemo wa Adam Smith

It is the maxim of a every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy.
Kipi kinafanya uchimbaji wa iron ore ya Tanzania uwe wa gharama kubwa ila hiyo hiyo ore inasafirishwa kwenda nje inatengeneza vyuma na vinauzika soko la kimataifa?
Japan inasafirisha iron ore kutoka duniani kote inazalisha vyuma na kuuza kisha sisi tumeyalalia tu.

Kipi kinafanya production cost za steel ziwe kubwa kwa Tanzania hii. Kuna maajabu gani kwenye steel ukishakuwa na umeme na raw materials, yani kutengeneza matairi ni vigumu kuliko kutengeneza steel.

Uganda wako mbioni kutuzidi kwenye hii sekta. Hakuna nchi iliwahi endelea bila chuma hatutakiwi kuwa na visingizio. Kuanzia China na Uturuki walioanza na textile manufacturing, kuja Japan na South Korea kwenye shipbuilding, kuja Germany kwenye automobile au Russia wenye extensive railway systems hakuna aliyenunua chuma nje.

Tukizalisha sisi wenyewe tunachukua malighafi kwenye machimbo yetu hapo gharama inakuwaje kubwa kushindikana kuwa controlled
 
China anatoa ores Australia kwa meli. Azikifua na kusafirisha steel duniani kote kuuza. Sisi huko liganga kinachimbwa na makaa yapo hukohuko ya kufulia. Gharama za uwekezaji mwanzo zitakuwa kubwa, pengine investors wataona siyo biashara. Kama ambavyo wanaona kujenga kitu kama barabara ni biashara kichaa. Lakini kikianza kuzalisha kina faida lukuki kwenye uchumi, kama barabara tu. Si lazima wauze bei pungufu, wanaweza uza bei inayoweza endesha kiwanda. Inaweza kuwa ya soko au chini.

Na usizungumzie Ulaya na Marekani. Gharama za uzalishaji huko, hasa za wafanyakazi na mazingira ni kubwa sana, ndiyo maana wanaagiza chuma. Si kwamba hawajui umuhimu wa kukizalisha. Utajiri na maendeleo yao leo yametokana na chuma.

Na si mpaka kuuza nje, tukijitosheleza wenyewe kwa nondo, vyuma vya mashine, reli, boats nk nk inatosha.

Nchi zote zilizotaka kujitosheleza kwa chuma ziliambiwa haziwezi na nyingine kunyimwa teknolojia. Hii ipo sana.

Everything you need to know about the industry breakdown.


Average investment costs za kujenga steel mills (plant) kuvuka $4 billion sio jambo la ajabu kabisa.


Average running costs ya large steel mill ni $1 billion dollars
..........

Na kuna costs zingine luluki ata kuziongelea ni shida.

Sasa ni hivi tukirudi kwenye dunia ya ukweli:

Tanzania inanunua chuma kwa wastani wa $400 million kwa mwaka; reli ikiisha na mradi wa bwawa hiyo level itashuka. Wakati expenses tu kuendesha kiwanda kikubwa cha chuma $1 billion kwa mwaka. Kwa hali ya sasa tungekuwa na kiwanda serikali ingekuwa inatoa ruzuku $600 kuwa na kiwanda tu; can you see why nikaongelea maswala ya break even.

Pili hakuna bank wala donor itakayoipa Tanzania hela ya kuwekeza kwenye hiyo mill in the first place; na hakuna hayo mapato ya ndani ya ku fund hiyo project.

Tatu ata tukiweza kuwekeza kwenye Mills, inabidi tujenge kwanza which might take years, halafu baada ya hapo tutafute hela tena za kujenga hiyo reli sums which might amount to 10s of billions na muda mrefu sana kabla ya kuanza kuona matunda ya reli yenyewe (be it ni ndoto za mchana kwa mazingira ya sasa).

Huyo Gwajima porojo zake abaki nazo huko huko kwenye kanisa lake, sio kuichosha dunia kusikiliza upuuzi wake; hakuna lolote la maana aliloongea zaidi ya ujinga mtupu.
 
Wewe ni mshamba ndio maana hujaona logic ya Gwajima. Ni sawa na kutoa tenda ya kusambaza vyakula mashuleni ila kampuni hiyo ikawa inanunua mahindi Kenya wakati hapa nchini yapo tungekuwa na mashine tungesaga.

Hivyo vyuma kama sikosei wanachukua zaidi Urusi kuja kujengea reli. Kuna ugumu gani kwenye teknolojia ya steel mpaka tuagize nje kwa kutumia billions of money? Tungekuwa na uzalishaji wa kujitosheleza tungetumia chuma chetu kutoka Mchuchuma & Liganga na kuzalisha ajira, kupunguza importation, kuongeza capacity ya uzalishaji na hatimaye kuuza nje, na huo mradi wa chuma ungerahisisha ujenzi wa viwanda.

Yani vyuma tumevilalia ardhini alafu unakuja na hoja za kishamba eti "comparative advantage". Hakuna nchi inaweza endelea bila kuwa na chuma, ambao hawana iron ore kama South Korea na Japan wanazalisha ila sisi tumelala na wala sio teknolojia ya nishati wala kompyuta kusema ni ngumu
Bora umenisaidia kumjibu huyo asiyejielewa
Shida wametanguliza chuki kwa mtu binafsi mpk wanashindwa kuona logic ya anachokiongea!
 
Sasa Mwigulu hiyo vision 2025 ndio mpango wa muda mrefu? Unajua tofauti ya short na long term Plans? Miaka 25 huwezi kuita long term ni makosa! Projections za miaka angalau 50 ijayo would suffice. Inakupa maono ya jinsi mnavyotegemea nchi iwe!
Ni mpango wa mda wa Kati,haujaanza leo kutekelezwa.
 

Everything you need to know about the industry breakdown.


Average investment costs za kujenga steel mills (plant) kuvuka $4 billion sio jambo la ajabu kabisa.


Average running costs ya kiwanda mill plant ni $1 billion dollars
..........

Na kuna costs zingine luluki ata kuziongelea ni shida.

Sasa ni hivi tukirudi kwenye dunia ya ukweli:

Tanzania inanunua chuma kwa wastani wa $400 million kwa mwaka; reli ikiisha na mradi wa bwawa hiyo level itashuka. Wakati expenses tu kuendesha kiwanda kikubwa cha chuma $1 billion.

Pili hakuna bank wala doner itakayoipa Tanzania hela ya kuwekeza kwenye hiyo mill in the first place.

Tatu ata tukiweza kuwekeza kwenye Mills, inabidi tujenge kwanza which might take years, halafu baada ya hapo tutafute hela tena za kujenga hiyo reli sums which might amount to 10s of billions na muda mrefu sana kabla ya kuanza kuona matunda ya reli.

Huyo Gwajima porojo zake abaki nazo huko huko kwenye kanisa lake, sio kuichosha dunia kusikiliza upuuzi wake; hakuna lolote la maana aliloongea zaidi ya ujinga mtupu.
Hakuna benki ya kimataifa au donor atakupa pesa ujenge steel mill. hili limeandikwa sana. Dunia ipo hivyo. Na kazi ya chuma si kujenga reli tu kwamba reli ikiisha kitakosa soko. Chuma ni muundombinu ambao si rahisi kuuwekea monetary value. Ni kama vile shule au hospitali. Hakuna nchi imeendelea bila kujitosheleza kwa chuma. Leo unaagiza chuma China, halafu China anaingia mgogoro na Australia. Unafikiri utakuwa kwenye hali gani? Chuma ni muhimu kuliko umeme maana mapinduzi ya viwanda yanaweza tokea bila umeme ila hayawezi kutokea bila chuma. Lakini watu huwa hatuulizi sana bei ya power plants maana tunajua faida yake. Sasa chuma ni zaidi ya umeme.

Gwajima katika hili yupo sahihi.
 
Back
Top Bottom