Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 588
- 1,698
Mbunge wa Kawe akiwa bungeni, Joseph Gwajima amesema kwa miaka mitano Taifa limelipa fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni 2.2 kununua chuma, Gwajima amesema kwa mtu yoyote mwenye akili na anajua kuzitumia jambo hili hawezi kuruhusu kufanyika.
Gwajima amesema nchi imeanza na reli ambayo hayupo kinyume nayo lakini ameshangaa kuanza na reli ambayo 'component' kubwa ni chuma kwa kukiagiza nje ya nchi badala ya kuchimba chuma kisha kujenga reli.
Gwajima amesema kinachosumbua ni kukosa maono ya Taifa, mipango na dira.
Gwajima amesema Taifa linahitaji maono ya pamoja na hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa miaka mitano au kumi.
Kingu-Taarifa
Kingu akichangia kupitia taarifa, amesema hadi tume ya kutengeneza mipango ya muda mrefu imefutwa. Amesema Taifa halina tume ya mipango kuanzia miaka 50.
Mwigulu akanusha
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amekanusha na kusema Taifa lina mipango ya muda mrefu na tangu uhuru limeongozwa na viongozi wenye maono na ndio maana kuna dira ya 2025 kutoka kwa Mkapa.
Mwigulu amesema nchi imeongozwa kwa maono ndio maana ipo ilipo. Mwigulu amemaliza kwa kusema Rais ameshaweka utekelezaji wa miradi mikubwa, yote inaenda kutekelezwa ya Liganga, LNG.