Gwajima: Taifa tumekosa maono, inakuwaje kujenga reli kabla ya kuchimba chuma? Waziri Mwigulu ampinga

Majuzi wametuambia mradi wa reli utachelewa kuanza kwa sababu bwawa alijakamilika lililotarajiwa kupeleka umeme; umeme uliopo sio wa uhakika.

Hivi tunafahamu umeme unaohitajika kwenye kiwanda cha heavy metal, investment capital na supporting infrastructure zake.

Kuna watu watakwambia kwanini tushindwe, utashindwa kwa sababu ni sawa na mtu anaengoa story za kuagiza Benz ujerumani wakati mapato yake ya mwezi laki mbili kabla ya kulipa kodi la pango, kutenga nauli na matumizi mengine.

Ndio wabunge wetu vitu wanavyoongea mara nyingi they don’t think through, plan tu ya kuweka vibao vya mtaa nchi nzima inatusumbua kila siku seminar; halafu tunawaza mambo makubwa makubwa.

Hivi wanafahamu ata break even ya kiwanda cha heavy metal, ili kiwe na sustainable operation.

Hapo bila ya diaspora hakuna shughuli miaka 800 tutazunguka na siasa za miaka ya sabini ubunifu wetu ulipoishia.
Kiwanda cha chuma ni muundo mbinu kama barabara, bandari nk. Huwezi kukiwekea mambo ya break even kirahisi.
 
ni lini ccm wakawa na maono ndio maana wakamuua mpaka Nyerere ili waweze kumuingiza mtu wao 2005
 
Kwa hivyo Gwajima anakubali Magufuli alikosa maono?

CCM unadhanj kuna watu inategemea wameamkaje siku hiyo hata kuwaamini tu ni kosa angekuepo jiwe asingetoa hiyo hoja, halafu hiyo hoja alishaisema zitto zamani sana
 
Mawazo ya Gwajima ni potofu na ya unafiki. Kiuchumi sio lazima nchi iwe na chuma ndio ijenge reli wala hata kama ina chuma sio lazima kwanza kuchimba chuma ndipo nchi ijenge reli. Kila ntu sasa anajifanya mchumi!.
Ziko nchi nyingi tu zimejenga reli na hazina hicho chuma.

Unapotaka kujenga reli unatangaza tenda baada ya kuwa umefanya tathmini reli itajengwa vipi na costs ni kiasi gani. Mkandarasi akishapatikana ndiye anajua vyuma atanunua wapi na kwa bei gani; sisi tunachotaka tukabidhiwe reli iliyojengwa kwa viwango na kwa wakati.

Hicho chuma ikitokea kimechimbwa siku moja kitauzwa kwa wateja wanaohitaji wa nje na ndani ya nchi na kitaingiza mapato ya fexha za kigeni na pia shilingi.

Hakuna nchi inazalisha kila kitu yenyewe na sio lazima kiuchumi tuzalishe kila kitu, vingine tutaagiza tupende tusipende; ndio maana kuna kitu kinaitwa comparative advantage katika biashara ya kimataifa sio suala la kuzalisha tu
Kama chuma kinapatikana, uzalishaji unaanza halafu kwenye tenda kunawekwa kipengele cha kutumia chuma kutoka ndani ya nchi.
Kwa maneno mengine gharama inapungua, pia biashara na ajira vinaongezeka.
 
Gwajima yupo sahihi. Ni kazi sana kwa nchi kuendelea bila chuma. Ukiwa na chuma utajenga reli kwa bei rahisi, utajenga nyingi, utajenga mabehewa. Na itakuwa rahisi kwako kurekebisha. Hao wakina Mwigulu wamekalia porojo za LNG utafikiri ni mtambo wetu!!
I hope you are just being sarcastic. I really do.

Amandla...
 
Kama chuma kinapatikana, uzalishaji unaanza halafu kwenye tenda kunawekwa kipengele cha kutumia chuma kutoka ndani ya nchi.
Kwa maneno mengine gharama inapungua, pia biashara na ajira vinaongezeka.
Naona kama kuna watu wanaamini kuwa chuma kinapochimbwa kinakuwa tayari kupelekwa site ili kitumike tunavyopenda.

Amandla...
 
Mbunge wa Kawe akiwa bungeni, Joseph Gwajima amesema kwa miaka mitano Taifa limelipa fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni 2.2, Gwajima amesema kwa mtu yoyote mwenye akili na anajua kuzitumia jambo hili hawezi kuruhusu kufanyika.

Gwajima amesema nchi imeanza na reli ambayo hayupo kinyume nayo lakini ameshangaa kuanza na reli ambayo 'component' kubwa ni chuma kwa kukiagiza nje ya nchi badala ya kuchimba chuma kisha kujenga reli.

Gwajima amesema kinachosumbua ni kukosa maono ya Taifa, mipango ya Taifa na dira.

Gwajima amesema Taifa linahitaji maono ya pamoja na hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa miaka mitano au kumi.

Kingu-Taarifa
Kingu akichangia kupitia taarifa, amesema hadi tume ya kutengeneza mipango ya muda mrefu imefutwa. Amesema Taifa halina tume ya mipango kuanzia miaka 50.

Mwigulu akanusha
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amekanusha na kusema Taifa lina mipango ya muda mrefu na tangu uhuru limeongozwa na viongozi wenye maono na ndio maana kuna dira ya 2025 kutoka kwa Mkapa.

Mwigulu amesema nchi imeongozwa kwa maono ndio maana ipo ilipo. Mwigulu amemaliza kwa kusema Rais ameshaweka utekelezaji wa miradi mikubwa, yote inaenda kutekelezwa ya Liganga, LNG.
Kipindi siku za nyuma Bw Zitto alizungumzia kuchimba Chuma kabla ya kuanza ujenzi wa reli!
 
Kama chuma kinapatikana, uzalishaji unaanza halafu kwenye tenda kunawekwa kipengele cha kutumia chuma kutoka ndani ya nchi.
Kwa maneno mengine gharama inapungua, pia biashara na ajira vinaongezeka.
Haya mawazo aliyatoa Ayatolla Zitto ila màgufool alimpuuza
 
Mbunge wa Kawe akiwa bungeni, Joseph Gwajima amesema kwa miaka mitano Taifa limelipa fedha za kigeni dola za kimarekani bilioni 2.2, Gwajima amesema kwa mtu yoyote mwenye akili na anajua kuzitumia jambo hili hawezi kuruhusu kufanyika.

Gwajima amesema nchi imeanza na reli ambayo hayupo kinyume nayo lakini ameshangaa kuanza na reli ambayo 'component' kubwa ni chuma kwa kukiagiza nje ya nchi badala ya kuchimba chuma kisha kujenga reli.

Gwajima amesema kinachosumbua ni kukosa maono ya Taifa, mipango ya Taifa na dira.

Gwajima amesema Taifa linahitaji maono ya pamoja na hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa miaka mitano au kumi.

Kingu-Taarifa
Kingu akichangia kupitia taarifa, amesema hadi tume ya kutengeneza mipango ya muda mrefu imefutwa. Amesema Taifa halina tume ya mipango kuanzia miaka 50.

Mwigulu akanusha
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba amekanusha na kusema Taifa lina mipango ya muda mrefu na tangu uhuru limeongozwa na viongozi wenye maono na ndio maana kuna dira ya 2025 kutoka kwa Mkapa.

Mwigulu amesema nchi imeongozwa kwa maono ndio maana ipo ilipo. Mwigulu amemaliza kwa kusema Rais ameshaweka utekelezaji wa miradi mikubwa, yote inaenda kutekelezwa ya Liganga, LNG.
Hii issue zito aliliongea sana tu sema ila ilikuwa ngumu sana kusurvive
 
Aliwaambia wananchi wake kuwa atajenga treni na pesa anayo😂😂
 
Mawazo ya Gwajima ni potofu na ya unafiki. Kiuchumi sio lazima nchi iwe na chuma ndio ijenge reli wala hata kama ina chuma sio lazima kwanza kuchimba chuma ndipo nchi ijenge reli. Kila ntu sasa anajifanya mchumi!.
Ziko nchi nyingi tu zimejenga reli na hazina hicho chuma.

Unapotaka kujenga reli unatangaza tenda baada ya kuwa umefanya tathmini reli itajengwa vipi na costs ni kiasi gani. Mkandarasi akishapatikana ndiye anajua vyuma atanunua wapi na kwa bei gani; sisi tunachotaka tukabidhiwe reli iliyojengwa kwa viwango na kwa wakati.

Hicho chuma ikitokea kimechimbwa siku moja kitauzwa kwa wateja wanaohitaji wa nje na ndani ya nchi na kitaingiza mapato ya fexha za kigeni na pia shilingi.

Hakuna nchi inazalisha kila kitu yenyewe na sio lazima kiuchumi tuzalishe kila kitu, vingine tutaagiza tupende tusipende; ndio maana kuna kitu kinaitwa comparative advantage katika biashara ya kimataifa sio suala la kuzalisha tu
Nadhani wewe ndio ujaelewa hoja yake. Ni hivi Gwajima anashangaa kwanini tumeanza kujenga reli kabla ya kuvuna chuma ili reli tunayojenga vyuma vyake vitoke hapa hapa nchini badala ya kuagiza nje.

Ni kweli nchi nyingi zimejenga reli na hazina madini ya chuma ila sisi tunayo. Kwanini mradi wa reli usingesubiri uvunaji wa chuma ili chuma chetu kiwe na soko la uhakika?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kiwanda cha chuma ni muundo mbinu kama barabara, bandari nk. Huwezi kukiwekea mambo ya break even kirahisi.
Kila kitu hapo ni investment inategemea unakiona ni merit good au business venture.

Muhimu nani anajenga ingekuwa barabara zinajengwa na watu binafsi kupita kungekuwa na toll charges, mchina akijenga bandari anataka return and so forth.

Tukiachana na hayo ata ukitafuta mwekezaji ajenge kiwanda cha chuma kwa hali ya umeme wa Tanzania atakwambia kwanza lazima ajenge na mitambo ya kuzalishia umeme wake.

Dangote tu ameweka umeme wake, hiyo ni saruji tu ili aweze fikisha production goals, sasa umeme unaotakiwa kwenye kiwanda cha heavy metal I ndustry tunaujua kweli au tunasikia tu.

Na break even kwenye kiwanda cha heavy metal is necessary ata kama huna lengo la kupata faida lakini uwezi kuzalisha kwa gharama zaidi kuliko unavyouza; vinginevyo utakuwa unatoa ruzuku kila mwaka ili kiwanda kiwepo tu; if you must know hizo ndio sababu asilimia kubwa viwanda vya chuma nchi nyingi vimekufa hasa za ulaya bora waagize China ambao wanatengeneza ata cheap (sasa usije jifananisha nao their economies of scale kwenye hiyo industry is at another level).

Ni hivi jengeni kama rahisi halafu muone kama mtaweza ata kuuza chuma Kenya au Rwanda kwa kushindana na bei za China.

Sisemi kwamba aiwezekani kabisa Tanzania kuwa na kiwanda cha chuma ila hatuna hizo resources, uchumi wa ku support hiko kiwanda na wala uwezo wa kushindana na China ata kuuza kwa nchi jirani tu let alone duniani.

Ni hivi hayo mambo sio rahisi kama mnavyoyaongea ukianza kukata namba zinazohitajika ili ufanikiwe ni mziki mnene.
 
Gwajima hayo maneno ungeyasema wakati ndugu yako aliyekupa ubunge yupo, ungevuliwa ubunge, angepewa Mdee
 
Ule mchongo ilikua hivi, jamaa baada ya kufumaniwa na akawa anampinga jiwe, kwa sababu jiwe mpenda sifa jamaa kuna kanisa huko korea kusini akaenda kubeba waumini wawili watatu wakapiga suti then kaomba aonane na jiwe kamletea wawekezaji basi jiwe kamwagika na shangwe na macamera wawekezaji kufika ikawa jam tu, jamaa akawa anapendwa sasa jumlisha na lugha wanaongea moja na ukumbuke zamani alikua team lowassa case ikaishia hapo, huyo hua ni msukuma mjanja mjanja wa mjini kama lugumi, kisena, dialo, masha, hao hua ni fursa mbele na ndio unaona kapewa kiwanja cha tanesco pale anajenga kanisa kabisa la kudumu wakati alikua mpangaji tu.
Duh

Ova
 
Pia, busara ungetumika kuaanzisha bwawa kabla ya kugharimu project ya SGR? its like putting a cart before the horse???
 
Kila kitu hapo ni investment inategemea unakiona ni merit good au business venture.

Muhimu nani anajenga ingekuwa barabara zinajengwa na watu binafsi kupita kungekuwa na toll charges, mchina akijenga bandari anataka return and so forth.

Tukiachana na hayo ata ukitafuta mwekezaji ajenge kiwanda cha chuma kwa hali ya umeme wa Tanzania atakwambia kwanza lazima ajenge na mitambo ya kuzalishia umeme wake.

Dangote tu ameweka umeme wake, hiyo ni saruji tu ili aweze fikisha production goals, sasa umeme unaotakiwa kwenye kiwanda cha heavy metal I ndustry tunaujua kweli au tunasikia tu.

Na break even kwenye kiwanda cha heavy metal is necessary ata kama huna lengo la kupata faida lakini uwezi kuzalisha kwa gharama zaidi kuliko unavyouza; vinginevyo utakuwa unatoa ruzuku kila mwaka ili kiwanda kiwepo tu; if you must know hizo ndio sababu asilimia kubwa viwanda vya chuma nchi nyingi vimekufa hasa za ulaya bora waagize China ambao wanatengeneza ata cheap (sasa usije jifananisha nao their economies of scale kwenye hiyo industry is at another level).

Ni hivi jengeni kama rahisi halafu muone kama mtaweza ata kuuza chuma Kenya au Rwanda kwa kushindana na bei za China.

Sisemi kwamba aiwezekani kabisa Tanzania kuwa na kiwanda cha chuma ila hatuna hizo resources, uchumi wa ku support hiko kiwanda na wala uwezo wa kushindana na China ata kuuza kwa nchi jirani tu let alone duniani.

Ni hivi hayo mambo sio rahisi kama mnavyoyaongea ukianza kukata namba zinazohitajika ili ufanikiwe ni mziki mnene.
China anatoa ores Australia kwa meli. Azikifua na kusafirisha steel duniani kote kuuza. Sisi huko liganga kinachimbwa na makaa yapo hukohuko ya kufulia. Gharama za uwekezaji mwanzo zitakuwa kubwa, pengine investors wataona siyo biashara. Kama ambavyo wanaona kujenga kitu kama barabara ni biashara kichaa. Lakini kikianza kuzalisha kina faida lukuki kwenye uchumi, kama barabara tu. Si lazima wauze bei pungufu, wanaweza uza bei inayoweza endesha kiwanda. Inaweza kuwa ya soko au chini.

Na usizungumzie Ulaya na Marekani. Gharama za uzalishaji huko, hasa za wafanyakazi na mazingira ni kubwa sana, ndiyo maana wanaagiza chuma. Si kwamba hawajui umuhimu wa kukizalisha. Utajiri na maendeleo yao leo yametokana na chuma.

Na si mpaka kuuza nje, tukijitosheleza wenyewe kwa nondo, vyuma vya mashine, reli, boats nk nk inatosha.

Nchi zote zilizotaka kujitosheleza kwa chuma ziliambiwa haziwezi na nyingine kunyimwa teknolojia. Hii ipo sana.
 
Back
Top Bottom