Naona wengi wenu mnaendeshwa na hisia na kuhusu suala la sauti Godwin Gondwe amekuwa na sauti hiyo hiyo tokea alipokuwa anafanya kazi RFA then TIMES FM and now ITV/RADIO ONE sasa sijui kipi cha ajabu na watangazaji wazuri katika kizazi hiki Godwin Gondwe ni mmoja wapo apart from that pia ni lecturer pale Tumaini University upande wa tasnia ya habari..
We ni far kabisa, huna uwezo wa kupima hoja na ukaamua, mbona mi naona ni mtangazaji mwenye mvuto? We una matatizo binafsi
Hakuna mtu amekataa hizo facts, wengi wameshasema humu ndani, hakuna mtu anayesema hajasoma, haya ni matatizo yetu hatutaki kuambiwa chochote zaidi ya kusifiwa. Humu tupo wasomi wengi ninachosema ni kwamba kuna umuhimu wa kuwa na specialization, ninamuona strong kwenye news, si uwongo hana uwezo wa ku interview, na sisi kama wasikilizaji ndio clients wake si vizuri watu kuingiza swala la chuki binafsi, si tu kwa wana habari, ni kwa fani nyingi sana watanzania tunapoteza na tumeshindwa kupenyeza kwa kung'ang'ania ujima. mambo ya kusema eti muambie mwenyewe sasa nini maana ya social media, pia kama supervisor wake anafaa na anastahili kumpa mshahara entry yangu ni ipi? social media ni entry nzuri ya kujengana. Pia tukumbuke hapa Tanzania hakuna independent evaluation ya media wala indicators za performance ambazo ni objective na zinamhusisha msikilizaji kwenye kitu kama survey, labda ma thinkers humu ndani mchukue hiyo kama business idea, na kuweza kuangalia kwa upana. Pia tukumbuke kwa bahati mbaya kwenye hii tasnia ya habari kuna changamoto hata ya vyuo vinavyofundisha. Nadhani kwa wale wenye vyombo vya habari wanalijua hilo, mwisho kabisa sioni kama ni dharau mtu kuviita vyuo vyetu vya kama maana tafsiri kamili ni pale ambapo level hiyo ya elimu imewekwa kuwa universal kwa almost kila mtu, kitu ambacho ni kweli kwa vyuo vikuu vya Tz tumeamua kwamba kila mtanzania asome mpaka huko ndio maana tunapewa hata mikopo kulazimisha hilo, jambo ambalo labda sio baya na hivyo si sawa kulinganisha na walio soma harvard maana kama ilivyokua kwa statement ya Ehud juu ya Tanzania, vyuo vyetu na matunda yake haviwezi kupambanishwa na hivyo. Muda umefika kwa sisi kuvumiliana na kukubali constructive criticisms ili tuweze kusonga mbele kama individuals, groups na hata taifa. Bado nafikiri kwamba GG ni mtanganzaji mzuri wa factuals, anaweza pia akasoma makala, si mzuri kabisa kwenye interview based journalism, japo anaweza kujifunza akafanya vizuri, regardless of his masters degree. Ni muhimu pia kama watanzania tukafahamu kwamba academic qualification haina uhusiano wowote na performance ya mtu labda kama ni research ama kufundisha. Bado ITV inawatangazaji wengi tu wazuri kwenye interview, mtu kama Salum Mkambara, Reinford Masako, Steven Chuwa ambaye kwa sasa nafikiri ni too senior kufanya interviews, Isack Gamba, Abdallah (yule jamaa mfupi )....., na kuna kaka mwingine anasauti nzito, hawa wametulia katika macho na masikio ya wasikilizaji. Unapowasikiliza unaweza kuwafuata maana wanauwezo wa ku flow na ku build discussion kwa kupitia maswali yao, unaweza kuona wazi kuwa brain zao ziko organized. Napenda kumalizia kwa kusema kwamba thread hii haina kusudio la kumtukana mtu wala kumdharau, tafadhali sana kabla hujajibu isome kwa mtazajo chanya.
hahahahaaaaaHakuna mwenye chuki binafsi hii ni cheap strategy ya watanzania msiopenda kuambiwa ukweli, sisi ndio watazamaji wa TV kwa nini utanakataa tunachokisema, ni bahati tu kwamba bado hatujaingia kwenye pay TV tusingelipia hizi TV ambazo watu wengine mnaziona ndio deal, tunachosema ni kwamba hana kipaji sasa chuki binafsi inatoka wapi wakati sisi hatuko ITV wala kuwania kazi yake, tunamwambia kumsaidia yeye na kituo chake kuangalia upya namna ya kuboresha delivery ya vipindi vyao, ebo!
Watu wengi wanapenda sauti za kubembelezwa, GG sauti ya kiume .. sasa itatumika kutoa amri akiwa Mwenyekiti wa Kamati yaUlinzi na Usalama wilaya..... ONGERA SANA MTU WANGU WA MWANZA, NYAKATO BUZURUGA.Kashaula haya mmesema analazimisha fan! sasa kaenda kwenye fan yake