Mwenye ushahidi wa dhahiri juu ya ufisadi wa Lowassa aweke hapa hadharani! Tuache porojo!

TeamLowassa

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
1,495
936
Kati ya watia nia wanaoshambuliwa zaidi kwa propaganda mfu ni Lowassa. Kuna mambo mawili yanayomfanya ashambuliwe sana. Moja, ni utajiri wake na pili, ni watendaji wa 'business as usual'!

Karibu watia nia wengi (sio wote) waliojiotokeza CCM hadi sasa wamewahi kupatwa na dhoruba za kisiasa kwa namna moja ama nyingine! Lakini hili la richmond la Lowassa limekuwa ruba! Kwa maneno mengine richmond inafanywa moja kwa moja kama vile ni mradi wa Lowassa, kiasi kwamba Lowassa anapachikwa jina la fisadi japo hakuna ushahidi wowote ulio dhahiri!

Mwenye ushahidi wowote ule wa uhusika w Lowassa kwenye ufisadi wowote ule hapa nchini auweke hadharani ili tukate mizizi ya fitna!

=========
Updates
=========

Hadi page ya nne hakuna ushahidi wowote uliopatikana ni ngonjera za team watia nia tu!

Endeleeni kungonyerika nitakuja kutoa updates za pages zingine zitakazofuata!


Lakini fahamu hizi tips kwa wewe usiefahamu.

1. Lowassa asingejiuzulu kama utajiri wake ni wa mashaka. Angebaki kung'ang'ania uwaziri mkuu kwa maslahi mapana ya utajiri wake

2. Serikali ni kubwa na yenye nguvu zaidi kuliko Lowassa. Utajiri wa Lowassa ulianzia enzi za Baba wa Taifa, kama Lowassa angekuwa na utajiri wa mashaka, Baba wa Taifa angeshamtia ndani muda mrefu sana.

3. Kuna mawaziri waandamizi waliowahi kuwa na kesi mahakamani kuhusu masuala ya ufisadi mfano Mramba, Idd Simba na wengine wengi lakini Lowassa hajawahi kuwa na kesi hata ya kuzingiziwa. Usifikiri serikali inamuogopa Lowassa!

4. Lowassa alijiuzulu kwa dhana nzima ya uwajibikaji na kulinda chama chake na serikali yake. Angeweza kukomaa na uwaziri mkuu kama wengine wanavyokomaa mfano Mh Pinda (Operesheni tokomeza ilidunda kwa Pinda, Escrow ilidunda kwa Pinda, Mauaji ya albino ilidunda kwa Pinda, Kauli ya wapigwe tu maana hakuna namna ilidunda kwa Pinda, nk).

=======
updates
=======

Uzi upo page ya tano. Bado hakuna ushahidi. Bado ngonjera ni zilezile kama za from page 1 to 4.


=======
updates
=======

Hii post ni ya Mkandara nimeitoa page ya tano. Nimeileta hapa juu makusudi ili niweze kuitendea haki na jamii yote ijifunze kwa upana wake!

Swali:
------
Mkuu umeuliza swali zuri sana ambalo wewe unawataka wananchi watoe ushahidi juu ya UFISADI wa Lowassa.

Kwanza ni kuhusu Utajiri wake nadhani swali hili aliulizwa na baba wa Taifa miaka hiyo akiwa mtumishi wa Umma hakulijibu, sasa pengine wewe unayo majibu - Lowassa alipokuwa mtumishi wa umma aliweza vipi kupata utajiri wake? Halafu kama kiongozi mgombea Urais tungependa awakilishe mapato na kodi zake zote kutokana na miradi alokuwa nayo - tumpime kwa uadilifu wake.

====
Jibu
====
Kwanini iwe ni Lowassa pekee ndie anaepaswa kusema namna alivyopata utajiri wake akiwa mtumishi wa umma? Kwani kupata utajiri ni kanuni ngumu kiasi hicho kwa mtumishi wa umma? Mbona ni suala dogo tu la namna unavyotumia kipato chako bila kujali ni kidogo kiasi gani? Ama tuseme kuwa tajiri ili hali ni mtumishi wa umma ni makosa? Hata hivyo, ingekuwa ni utaratibu wa kila mtumishi wa umma kuonyesha namna alivyovuja jasho na kupata mali zake hata Lowassa nae angefanya hivyo hivyo bila kukawia!

Usisahau kuwa kipindi hicho Baba wa Taifa alishatanabaisha kuwa umaskini ni adui wa kitaifa, hivyo Lowassa kwa kumuunga mkono rais wake akaanza kupambana mbele kwa mbele kutokomeza adui umaskini. Kuthibitisha hili ndio maana Baba wa Taifa hajawahi ku pin point na hakuna rais yeyote aliewahi kuonyesha ni wapi Lowassa alikwapua utajiri. Kwa kiasi kikubwa imebaki kama wivu na chuki binafsi.

Pia tume ya maadili ya utumishi wa umma ina list ya mali za Lowassa kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma, kama kungekuwa na mali yenye mashaka tume ingeweza kuchukua hatua za mbele zaidi.
=================================================================


Swali:
------
Katika utendaji wake na kuhusu swala la Richmond. Lowassa mwenye alishindwa kujibu alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kujiuzuru kwake, akajibu ya kwamba alifanya hivyo kukinusuru chama!. Kweli wewe leo unataka kuwa Rais wa nchi hii ulopenda kukinusuru chama kwanza kabla ya nchi yako kwa kashfa ya Kuhujumu Uchumi? Je, hizi gharama tunazolipa leo katika uwekezaji wa Richmond haoni kwamba yeye kama waziri mkuu ndiye mhusika mkuu?.

====
Jibu
====
Lowassa ana hekima sana na uzalendo mkubwa kwa Taifa lake. Ni kiongozi mwenye kifua cha kuvumilia mengi. Kusema kuwa alijiuzulu ili kunusuru chama ni kuonyesha utii kwa chama kilichompa ridhaa ya kuwa waziri mkuu. Lowassa hajajipa uwaziri mkuu. Kama asingeonyesha kuheshimu na kulinda hadhi ya chama chake ungeweza kufanisha na abiria anaetoboa ngalawa yake. Lazima aonyeshe heshima na uzalendo wa kutosha kwa chama kilichompa ridhaa. Uwaziri mkuu alipata kwa tiketi ya chama chake.

Kumbuka nchi ni chama. Chama ndio kinaongoza nchi na nchi hainongozi chama. Chama ni nchi, hakuna nchi bila chama. Ndivyo siasa za ulimwengu zilivyo. Hata huo umeme aliokuwa anapigania si kwa ajili ya chama bali kwa ajili ya Taifa. Hakuna popote ambapo amehujumu uchumi. Kuhujumu uchumi kwa sheria za nchi hii ni kosa la jinai, kama hivyo basi leo hii angekuwa rumande ama ana kesi ya kujibu mahakamani.

Swali:
------
Na zaidi ya hapo Lowassa amedanganya kwamba viongozi wa Marekani walikuja na kusema Mradi huo wa Richmond ni mzuri kabisa na kwamba mitambo yake ni state of the art! Ukweli umetuonyesha kwamba hata balozi wa Marekani amesema wazi kwamba kampuni ya Richmond ni shirika la uchapishaji vitabu tu, pia tunajua mtambo huo wa GE sio state of the art ni mtambo ulokwisha kuwa ktk soko zaidi ya miaka 10 iliyopita. Kusema uongo kwa kiongozi kama yeye ni mwanzo wa kutoamini kauli zake.

=====
Jibu
=====
Mkuu jitahidi kuongea facts walau kidogo. Kama una ushahidi wa haya unayosema tuwekee hapa hadharani. Hearsay sio ishu mkuu.

Swali:
------
Report ya Mwakyembe inaonyesha wazi waziri mkuu alihusika sana na maamuzi yote yatokanayo na shirika la Richmond kupewa tender hiyo dhidi ya maamuzi ya wataalam walipendekeza Agrekko na mashirika mengineyo mbali na kwamba bunge la kwanza la mwaka 2006 lilipendekeza Tanesco iwezeshwe katika kuzalisha umeme. Report ya Mwakyembe pekee ni ushahidi tosha akiweza kujibu maswali yote leo hii kufuta lawama hizo tutamsikiliza.

=====
Jibu
=====
Kama hivyo ni kwanini tume ya mwakyembe haikumhoji kuhusu hili? Balance ya story hii iko wapi???? Kwani Lowassa ahojiki mbona hakuohojiwa ili aeleze in and out?


Ahsante sana kwa maswali yako mazuri. Hope, hapa umefunguliwa mwanga wa mengi kuhusu Lowassa. Karibu sana!


=======
updates
=======

Hizi ndio baadhi ya posts za ushahidi:


Richmond, kupora ardhi na kujigawia nyumba ya serikali ikakarabatiwa na fedha za Umma akampangisha balozi wa South Africa huo sio ufisiyard?

ushahidi utaupata jina lake litakapo katwa nakukosa urahisiii anaoupigania kufanakupona,nandoutakuwa mwisho wakupata posho ktka kwa fisadi el a.k.a joka lamakengeza.shame on u unaejfanya punguhn xababu ya mtonyo wa ..

Watanzania mnaotaka mamvi awe rais ni wapumbavu nambari, huyu jamaa hastahili hata kujadiliwa mngekuwa karibu yangu ningewatembezea kerubu za hatari *****. Emu nitumieni gunia la limao nipunguze hasira mnanikera sana nyang'au shwaini nyie.

hiikitu inakuzwa ili kumchafua lowasa, ripoti ya mwakyembe nimeisoma zaidi ya mara tano, sijaona mahali ambapo barua ilitoka ofisi ya Pm ikitaka Richmond apatiwe tenda zaidi ni porojo na mipasho tu, pili EL Hakuitwa wala kuhojiwa, ripoti ililenga uwaziri mkuu ,mara tumepewa maagizo kutoka juu! yani usomi haukuwepo kabisa , ila wa tz tumeshajua ukweli na sisi fitna kwe2 mwiko, navyoijua ccm mtu mzuri hatakubalika kamwe kwani wanajua atakuja kuwa sambaratisha woote lowasa ni kama mvua kama inanyesha inanyesha

TUACHE HABARI AMBAZO HAZINA MAANA YOYOTE ILE MWENYE TAARIFA SAHIHI JUU YA UHUSIKA WA MOJA KWA MOJA WA MH LOWASSA.
TUNAKUOMBA UTUWAKEE HAPA TUJIRIDHISHE KUROPOKA KWA WATOTO WA KIUME HAKUPENDEZI/ LETS TALKS WITH DIRECT EVIDENCY/i

Niliwahi kusema kuwa chuki na ghiliba za kisiasa plus interest za nchi kubwa za Dunia hii ndo zinapelekea Lowassa kuundiwa zengwe ... bahati mbaya sana Watanzania wa leo wanaongozwa kwa hisia na si facts ... Lowassa ndo kiongozi pekee mwenye kujua deals za maharamia na kutumia Rasilimali zetu kwa manufaa ya wananchi!! Kuna watu wanakinga kiasi kikubwa sana cha fedha kutoka Egypt via USA ili kutunza maji ya Lake Victoria... Watanzania tulinyimwa kutumia maji hayo; waliokuwa wanapewa fedha za kuchimba visima virefu walikuwa wanakula... Ilipotokea Lowassa ametekeleza mradi wa KASHWASA jamaa wakaona sana deal lao limevurugwa ...!!! Watanzania kuweni Makini sana na hawa EHM mnao waona Wazalendo! Jiulize kwanini ESCROW ya akina Membe, Pinda, Nchemba et al Imepoozwa na kuonekana Fitna za Richmond ndo ya Ukweli ?.... Itoshe kusema Lowassa tunamuhitaji kuliko yeye anavyohitaji kuwa Rais wetu ...

Lowasa ni fisadi.

======
updates
======

Hapo chini ni mtanange wa page ya 7 bado ushahidi dhahiri haupo! Nitaendelea kuwapa updates zaidi!

Mkandara Nixon alisamehewa na Gerald Ford aliyekuwa Rais baada ya Nixon kujiuzulu. Msamaha aliopewa ulikuwa kwa crimes,he committed or may have committed. Nixon alifanya kosa la kisheria sio ethics mkuu Uchunguzi ulifanyika na kila kitu kikawekwa wazi. Alifanya kosa Nixon akapewa Presidental pardon.Kosa la kimaadili la Lowassa ni lipi?Adhabu ya dhana zisizo na ushahidi wa kukubalika ni kuendelea kwa uzushi. Na kwa sababu tunapenda uzushi na kukimbia haki na uhuru wa mtu ndio maana hakuna aliyeleta ushahidi mpaka sasa . Mtu hata akituhumiwa kwa kukiuka maadili si huwa anahojiwa? Kwanini hakuhojiwa?Kwanini?

Lowassa hakuvuliwa Uwaziri bali alijivua kwa kutoridhiswa na jinsi Kamati teule iliyoundwa na bunge kuchunguza suala la RICHMOND ilivyomuonea!
Angalia hii!

https://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=5Zx9d91aywI

Sasa wewe ndiye unayetaka kulazimisha. Nilichoandika ni kwamba Lowaasa alikiuka miiko na maadili ya Uongozi na ushahidi nimeuweka hapo report ya Mwakyembe ambayo imemweka waziri mkuu kama mhusika acha mbali kuwajibika kwake kama waziri mkuu. Kama angetaka kujieleza alikuwa na wakati huo Bungeni, sio lazima aitwe na kina Mwakyembe mbona kina Rostam na Yona walikataa kuhojiwa! Unajua wazi kwamba Bunge letu halina meno wala TAKUKURU kwa viongozi wa juu. Lakini yeye akachagua kujiuzuru kabla ya kujitetea akidai anakisamilisha chama. Kiongozi wa aina hii hafai kuwa rais wa Tanzania anaweza kuwa kiongozi CCM lakini sio kiongozi wa nchi hii maana ana maslahi menigne zaidi ya Taifa.

Nimekuuliza swali la Utajiri wake aloulizwa na baba wa taifa miaka ya 70 halijajibiwa. yeye kama mtumishi wa Umma na kiongozi wa chama aliwezaje kupata Utajiri wakati chama chake kikiendesha mrengo wa UJAMAA na KUJITEGEMEA ambao kiongozi hakutakiwa kuwa na mishahara miwili, kofia mbili acha mbali kuwa na hisa katika mashika binafsi?.

Mkandara kweli mkuu unataka ujibiwe swali la miaka 1970? Ndio uzushi ninaouzungumzia huo.Mwaka 1971 Lowassa alimaliza form four.Alikutana wapi na Mwalimu Nyerere na kumuuliza kuhusu utajiri wake? Alikuwa ana post gani kitaifa miaka ya 1970?Mpaka aulizwe? Mkandara mkuu huwa na admire uwezo wako wa kuchambua mada lakini na wewe umebebwa na kimbunga cha uzushi bila hata kujiuliza. Is it possible? Ni kweli ?

=====
updates
=====

Tupo page ya 8 ushahidi bado haujapatikana, nitaendelea kuwapa upadtes!

Lowassa angekuwa anahusika na Kashfa ile, angeweza "kukomaa" na uwaziri mkuu wake na bado pasingekuwa na mtu wa kumwajibisha, ila aliachia ngazi ili kuwaridhisheni nyie wachache mliodhani kuwa naye pia ni mhusika.Ili mpate faraja kwa muda tu. Pinda "amekomaa" na mangapi na mpaka leo anadunda? Sasa Lowassa anakuwa Rais wa TANZANIA, haya yote aliyashayasemehe!

======
updates
======

page ya 9 bado bila bila, tuendelee kutafuta ushahidi

We kweli mwehu, badala ya kuweka ushahidi we unaharisha hapa, shame on you! chuki nyingine hazina maana...

RICHMOND (GIRE HOUSTON TEXAS)-AMBASSADOR/ Facilitator (Mr. DARAJA)-the President (commanding unit) Dr/Prof Kikwete - Implementer (Mr. Edward Lowasa). Lowasa Kashikwa na ngozi ndiye mwizi.

=====
updates
=====

Tupo page ya 10 still no ushahidi, bado nitaendelea kufuatilia

1. Nitajie mapungufu matano ya kibinadamu alionayo lowasa kama binadamu

2.Nitajie mapungufu matano ya mheshimiwa lowasa kama kiongozi mapungufu ya kiuongozi....

Tangu 2011 tunaskia sifa zake tuu sasa naomba unijuze mapungufu au Lowasa ni malaika hana kasoro...

jambazi ulitaka ahojwe nini ...

Mie nadhan mwenye ushahidi na tuhuma hizi AMA maelezo tofauti atakuwa Lowassa mwenyewe,lakini Mbona katika mkutano wa safari ya matumaini hakuchimbua suala hili na kuweka peupe?sasa tunamtaka nani amsemee mambo ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe!!!!

Hii comment nimeitoa page ya 10 naye bado anasubiri ushahidi

nasubiri ushahidi kwa hamu

mana kelele zilizid humu

Hakuna mahali popote katika ripoti ya Mwakyembe ambapo Lowassa alitajwa kuhusika na ufisadi. Lowassa aliwajibika kutokana na makosa ya watendaji wa chini yake yaani political responsibility.

Ki uhakika na kimazingira angekuwa fisadi asingekubali kujiuzulu, angekuwa king'ang'anizi.
Tabia za mafisadi tumeziona kwenye sakata la escrow.

Lowasa ni kiongozi wa mfano, mzalendo, makini mwenye kupenda maendeleo ya mtanzania mmoja mmoja
 
Mimi kuhusu ufisadi na Richmond najua ni game inachezwa kupitia wanasiasa wenyewe,
Wasiwasi wangu kwa lowassa amekuwa mshirika mkubwa wa serikali karibu awamu zote amekuwemo, hebu tuonyeshe ambacho lowassa amekifanya ili anagalau mimi binafsi nishawishike kumpa kura yangu
 
bado kikwete ni raisi wako kumruhusu rowasa aongee ukweli ni kubomoa serikali

Wote ni wale wale tu!Kama hapendi rushwa, mzalendo na ni muadilifu, ni kwanini asingeamua kujiuzulu mapema kama aliona boss wake anamuingiza kwenye deal chafu na badala yake anajiuzulu baada ya kamati ya Bunge kumtaka afanye hivyo(ajiuzulu)?
 
ushahidi utaupata jina lake litakapo katwa nakukosa urahisiii anaoupigania kufanakupona,nandoutakuwa mwisho wakupata posho ktka kwa fisadi el a.k.a joka lamakengeza.shame on u unaejfanya punguhn xababu ya mtonyo wa ..
 
Watanzania mnaotaka mamvi awe rais ni wapumbavu nambari, huyu jamaa hastahili hata kujadiliwa mngekuwa karibu yangu ningewatembezea kerubu za hatari *****. Emu nitumieni gunia la limao nipunguze hasira mnanikera sana nyang'au shwaini nyie.
 
Watanzania mnaotaka mamvi awe rais ni wapumbavu nambari, huyu jamaa hastahili hata kujadiliwa mngekuwa karibu yangu ningewatembezea kerubu za hatari *****. Emu nitumieni gunia la limao nipunguze hasira mnanikera sana nyang'au shwaini nyie.

Utakufa bure mdogo wangu kwa kula gunia la limao kwani acid itakuwa nyingi na mwisho itaozesha nyama za mwili.

teh teh teh
 
hiikitu inakuzwa ili kumchafua lowasa, ripoti ya mwakyembe nimeisoma zaidi ya mara tano, sijaona mahali ambapo barua ilitoka ofisi ya Pm ikitaka Richmond apatiwe tenda zaidi ni porojo na mipasho tu, pili EL Hakuitwa wala kuhojiwa, ripoti ililenga uwaziri mkuu ,mara tumepewa maagizo kutoka juu! yani usomi haukuwepo kabisa , ila wa tz tumeshajua ukweli na sisi fitna kwe2 mwiko, navyoijua ccm mtu mzuri hatakubalika kamwe kwani wanajua atakuja kuwa sambaratisha woote lowasa ni kama mvua kama inanyesha inanyesha
 
Kati ya watia nia wanaoshambuliwa zaidi kwa propaganda mfu ni Lowassa. Kuna mambo mawili yanayomfanya ashambuliwe sana. Moja, ni utajiri wake na pili, ni watendaji wa 'business as usual'!

Karibu watia nia wengi (sio wote) waliojiotokeza CCM hadi sasa wamewahi kupatwa na dhoruba za kisiasa kwa namna moja ama nyingine! Lakini hili la richmond la Lowassa limekuwa ruba! Kwa maneno mengine richmond inafanywa moja kwa moja kama vile ni mradi wa Lowassa, kiasi kwamba Lowassa anapachikwa jina la fisadi japo hakuna ushahidi wowote ulio dhahiri!

Mwenye ushahidi wowote ule wa uhusika wa Lowassa kwenye ufisadi wowote ule hapa nchini auweke hadharani ili tukate mizizi ya fitna!

Katika kupima uadilifu wa mtu (hasa anayegombea nafasi inayohitaji uadilifu mkubwa) ile principle ya "WHO ALLEGES MUST PROVE' inakufa. Yeye atuambie utajiri wa kufuru alio nao aliupata wapi wakati akiwa mtumishi wa serikali na mshahara kiduchu!
 
Back
Top Bottom