Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Mi wala sioni mantiki ya kubishana kuamini/kutoamini watu wangapi wamekufa...afe mmoja, wawili watatu, 17, 20, 32, 200 au 300..ukweli unabaki pale pale, kuna waTanzania wamekufa 'bila hatia' kwa uzembe wa viongozi pamoja na majeshi yetu!
 
Habari zilizopo ni kwamba, mchana huu mabomu mengi zaidi yanatarajiwa kulipuka na bado kumekua na milipuko ya hapa na pale... wakazi wa gongo la mboto wameamuriwa kuondoka mchana huu kabla ya muda huo.
Source: Private source
 
Hivi na leo tena hakuna atakayewajibika au kuwajibishwa, kwa wanaokumbuka mwaka 2002 milipuko ile hakuna hatua zilichukuliwa, ikaja tena mwaka juzi, hakuna lolote, leo tena!!!
 
Ni aibu kwa serikali magari yetu yaliyonunuliwa kwa kodi zetu tena yenye namba za SU, STJ, STK n.k yanapita watu bila kuwasaidia! Ni AIBU sana kwani hawa nao si wana roho kama za wengine??
 
Asidanganye mtu, hali bado ni tete na majeruhi na vifo ni vingi, je hapa kuna mkono wa CDM pia???
 
Ningeomba private owned organizations ndo zifanye uchunguzi na sio kuundwa kwa kamati, zenye kula tena pesa kidogo iliopo, Makamba asijifanye tena kupeleka msaada wake huko, asije peleka mchele wake uliooza kama kipindi kile...
 
Hapa sijaelewa mkuu. I reside in Tabata ila sasa nipo ofisini, Hebu nieleweshe vizuri angalau nifanye kazi
Ni kwamba mzee, karibu na shule ya Tusimee kuna bomu limeanguka usiku na inasemekana bado halijalipuka na watalilipua saa tisa, pia majumba sita inasemekana kuna kitu kama hicho.
 
Maskini nchi yangu, sijui viongozi wake waliingia kwa njia isiyo halali mwaya hata sijui!!! yaani matukio mabaya tu, nadhani JK amepata kichaka cha kijifichia ili asitimize ahadi zake zenye thamani ya trillions!!!
 
Tumetaka serikali inayo dumisha UMOJA na AMANI by any means necessary ..TUMEIPATA
 
Ni kwamba mzee, karibu na shule ya Tusimee kuna bomu limeanguka usiku na inasemekana bado halijalipuka na watalilipua saa tisa, pia majumba sita inasemekana kuna kitu kama hicho.

Hebu jamani tupeane taarifa sahihi ili kutowachanganya zaidi wahanga. Generali Shimbo ametoa maelezo muda si mrefu kuwa ni uvumi kuhusu Mabomu yatakayolipuliwa mchana huu. Hawatalipua mabomu yanayookotwa na ameomba watu wasiyaguse hayo yaliyopo katika maeneo yao ila watoe taarifa. Hayawezi kulipuka yenyewe mpaka mtu ayachezee au kujaribu kuyategua na si kazi rahisi. Kasi ya kuyaondoa inaendena na yale wanayoyaona yana hatari zaidi ndiyo wanaanza kuondoa. Ni vyema tusaidiane kutoa taarifa sahihi ili kuepuka watu wengi zaidi hasa watoto kutotulia, wengi zaidi wanaweza kukimbia, kupotea au kukutwa na hatari
 
Kwa maelezo yaliyotolewa na mkazi wa gongolambota karibu na Camp (Mahojiano na Wapo Radio), alisema baada ya kama milipuko minne ya mwazo zilifika gari za Jeshi tatu zikiwa na takribani askari 50, alisema alimsikia kiongozi wa ule msafara akiongea kwa Radio call akimjulisha mkubwa wake kuwa pale camp hali ni mbaya sana sana ...lakini yule mkubwa akawa anasistiza wale askari waingie kule ndani ya Camp!!! Kijana anasema wale wote walikuja na yale magari hajatoka hata mmoja hao ni askari kutoka nje ya Camp....akaongeza kuwa milipuko ilipoaanza wapo watu walikimbilia kwenda kushangaa nini kimetokea nao hao pia hakuna aliye rudi sasa hiii ni mbali na wale askari waliokuwa wanaishi ndani ya camp......Idadi ya watanzania walikufa kwenye tukio hili itakuwa ni kubwa sana....wataficha tuu...haya mabomu yamefanya mafaa hata mbali kabisa na eneo hilo mpaka Pugu, chanika huko.....hali ni mbaya sana sana wasiundangaye Umma wa Watanzania!!!!

haya ni mazoea yetu so sishangau sana,ila nadhani hizi shule za kata japo zitaendelea kutusaidia japo elimu ya kufikiria mambo marahisi
 
Mi wala sioni mantiki ya kubishana kuamini/kutoamini watu wangapi wamekufa...afe mmoja, wawili watatu, 17, 20, 32, 200 au 300..ukweli unabaki pale pale, kuna waTanzania wamekufa 'bila hatia' kwa uzembe wa viongozi pamoja na majeshi yetu!

kweli kabisa.....huitaji kuweka number ya marehemu ili watu wachukue hatua na kufanya maamuzi magumu...
 
Kweli afadhali yawe sehemu zo mwenyewe wanajeshi kuliko maskini wa Taifa hili maana wengine wakisema wanasema kuwa ni siasa
 
Kuna tangazo hapa Channel ten, wazaz waliopoteza watoto waende vituo vifuatavyo vya police; buguruni, ukonga, msimbazi, tazara , uwanja wa taifa na saba saba.
 
Back
Top Bottom