Gen. Mboma ajaribu kugombea, aangushwa!

Wakuu Mlekwa & Ngongo
Nakubaliana na hoja zenu za umoja ni nguvu.Lakini katika umoja huo, tukubaliane kuwa wakati mwingine tupanue wigo wa uchaguzi wa sera badala ya personalities au itikadi za vyama.Najua watz wengi wapenda demokrasia mna hamu sana ya kuona opposition inaongeza idadi ya viti bungeni.Mimi kwa upande wangu napenda tuwafundishe na kuwazoesha wapiga kura kuchagua ubora wa sera na mgombea.Naunga mkono CHADEMA wagombee, ili sera zao zitambulike kwa wapiga kura wa Tanzania hiyo ndio nafasi pekee ya kujitangaza.Ninachotaka kushauri hapa si vizuri,incase mgombea wao hauziki waanze kumkandia mgombea wa chama kingine cha upinzani.
Tofauti ya uchaguzi wa Tarime vyama vingine vya upinzani vilikuwa vinaonyesha kukipiga vita vya wazi CHADEMA.Hali hiyo isirudiwe,chama kishiriki kueleza sera na mikakati yake ya kuboresha na kutetea walipa kodi wa Taifa letu.
Mkuu Gembe, si kweli kuwa sisi watu wa Mbeya tuna ukabila.Nitakupa mfano wa madiwani wawili wa kyela na nitaonyesha mabano ya kata wanazowakilisha.Kuna Visky Mahenge ambaye ni mkinga(Kyela) na Mh.Chrissy ambaye ni mkulya(Ipinda).Vilevile kule mbozi wenyeji wa wilaya ni Wanyiha na Wanyamwanga, lakini Mwenyekiti wa Council ni mnyakyusa.Huyu marehemu Nyaulawa,alikuwa mkinga ambao kule Mbeya vijijini ni wachache na walio wengi ni Wasafwa na Wamalila(kabila la Mboma).Huu mkoa wa Mbeya sasa hivi una wahamiaji wengi kutoka sehemu mbalimbali ya nchi yetu na nchi jirani na wanaishi vizuri na kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali za uongozi.Nakumbuka hata uchaguzi mkuu wa 2005,NCCR-Mageuzi walimsimamisha Temigunga Kisonga(mhehe) na alivutia wapiga kura wengi licha ya kwamba matokeo yalitoka kinyume na ilivyotegemewa.Mimi kama mchunguzi kilichowaangusha wapinzani ni kukosa network ya mawakala wa dhati kama wale wa Tarime.Kipindi kile mchuano ulikuwa mkali kati ya Mwakagenda(CHADEMA) na Kisonga(NCCR-Mageuzi),lakini matokeo yakawa landslide victory kwa mgombea wa CCM akisaidiwa na nguvu ya EPA.
Ninachokijua mimi ni kwamba wananchi wa Mbeya wana permanent interest,wanataka miundo-mbinu kama vile International Airport,Tarmac road mbeya-chunya-itigi,Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia n.k.Mbeya hawana chuki na mtu yeyote anayejali maslahi yao na wala hawawezi kulambishwa pipi ya kupewa vyeo kwa sababu vyeo hivyo vinakuwa kwa waliopewa sio mkoa wote.Hawapendi kuzugwa!
 
Wana JF na wapenda mageuzi wote, kujitokeza kwa Mboma ni ishara ya kuwewewseka kwa mafisadi, wamekuwa corrupted na pesa walizotuibia na madarakla wanayoyang'ang'ania. Badaa ya kujitokeza hivi sasa yanaibuliwa mengi kama vile shamba lake kule Mbozi jirani na fisadi mwenzie apson, maeneo mbali mbali yenye madini aliyomiliki kila kona ya nchi hii ni mambo yanayozungumzwa wzi wazi vijiweni hapa mbeya.

Hebi niwape dokezo, leo wamepiga kura na hivi sasa tunasubiri matokeo, lakini kuna kila dalili ya gen huyo kuandaa wajumbe kwani ndiye pekee aliyeulizwa maswali yale ya kumjenga.

Lakini waswahili walisema sikio la kufa halisikii dawa, Gen alishindwa kujibu kwa ufasaha, anasema "si kazi ya mwanajeshi kushiriki katika maendeleo, mkinichagua nitashiriki!"

Baadhi ya wajumbe waliguna kila alipojieleza wakieleza wazi kwamba maswahi yanayoelizwa ni ya kumjenga
 
Kuendelea kuuhusisha mkoa wa Mbeya na ukabila ni kutoutendea haki, na mara zote madai haya huibuka wakati wa chaguzi za kisiasa na wananchi wanapolalamikia wizi unaofanywa kwenye halmashauri. Iwapo Thom angepita ni wazi tusingesikia kelele za ufisadi, kina bubelwa aliyewahi kuwa city tresurer wa jiji la Mbeya walipoiba na watu kukaa kimya hapakuwepo na kelele za ukabila.

Pale Kyela walipomkatalia Vicks Mahenge kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa sababu ya kukosa elimu, zikaibuka kelele za ukabila na kusahau kuwa ni hao hao waliompa udiwani wa kata ya mjini!

Mbeya haina ukabila bali ni njaa za wanasiasa uchwara na wezi, sina haja ya kutoa mifano zaidi kwani Nsaji Mpoki amefanya hivyo.

Madai ya ukabila ni upomkubwa, wako mababila mvbali mbali mkoani humo ambao wanamiliki ardhi na uchumi mkubwa kuliko wenyeji na wala wenyeji hawalalalamiki.

Wenyeji wa Mbeya hawaendi kunywa kwenye baa kwa sababu ni mnyakyusa mwenzao, au mmalila au msafywa, au mnyamwanga au mdali kama ilivyo kwa baadhi ya makabila hapa ambapo wachaga hunywa baa za wachaga wenzao
 
Nsesi,

Asante sana kwa kutupasha za Mbeya.

Mahenge kule Kyela alikataliwa au alishindwa katika kura halali? Labda ni matumizi tu ya lugha. Nakubaliana na wewe, hao hao waliompa udiwani ndio waliomnyima kuwa Mwenyekiti wa halmashauri kwa kura halali. Hakuna ukabila hapo.

BTW: Nimelipenda jina lako la Nsesi, linanikumbusha mengi.
 
MATOKEO JIMBO LA MBEYA,

Mboma kabwagwa na na Mchungaji wa Kanisa ka Uinjilisti maarufu kama Kanisa la Leiner hapa Mbeya.

Mchungaji Manjali ameibuka mshindi kwa kura 435, Alan Mwaigaga kura 259, Andrew Saile kura 229 na Mboma kura 164

yametangazwa nusu saa iliyopita
 
wewe si uli nuna?Imekuaje?Sie tulijua wewe huwezi,ulikuwa unatingisha kibiriti tu,mbowe kakuamrisha urudi na sasa umerudi,kibaraka wa Mbowe!!!!!
 
wewe si uli nuna?Imekuaje?Sie tulijua wewe huwezi,ulikuwa unatingisha kibiriti tu,mbowe kakuamrisha urudi na sasa umerudi,kibaraka wa Mbowe!!!!!

Nakosa muunganisho wa posti yako hii Halikuniki, kama ni personal issues si ni vyema ukamtumia private messgae ( PM)?. Vinginevyo unatuchanganya wanajamvi, sorry anyway!
 
Mkuu Nsaji,
Nakubaliana na wewe kwamba kwa miaka hii Mbeya imebeba wageni wengi sana, kiasi kwamba ile dhana ya ukabila ishatokomea. Kuna madiwani kibao sana hapo Mbeya ambao si wenyeji wa mkoa huo. Umeongea mengi sana pamoja na kutoa mifano. Mbeya ni tofauti sana na mikoa iliyo mingi ambayo inakumbatia ukabila, kwamba mtu kama sio wa kabila lile basi hana nafasi. Kwa sasa, wananchi huwa wanamchagua mtu ambaye ana maono 'Vision' ya kile ambacho wananchi wanataka.
Nyaulawa hakuwa Msafwa wala Mmalila (wenyeji wa wilaya ya Mbeya), lakini aligombea jimboni humo na akapita bila kupingwa na amesaidia sana ujenzi wa shule za sekondari na uanzishwaji wa Saccos mbali mbali (mojawapo ipo kijiji cha Inyala). Alikuwa katika mpango wa kuanzisha kiwanda cha mbolea kwa mikoa hii ya nyanda za juu kusini ili kupunguza gharama za bidhaa hiyo, mpango ambao sioni wa kuuendeleza baada ya Nyaulawa kufariki.
Hata huyu Mchungaji Mwanjali aliyepata ushindi kupitia CCM si Msafwa, ilhali Wasafwa akina Mwaigaga na wenzake na Mmalila Mboma wamemwagwa! Sasa mpaka hapa ukabila uko wapi?
 
Bravo kummwaga Mboma! Ila hili wimbi la wachungaji kukimbilia bungeni nalo limekaa je? whats up?
 
Mbona hii ya kubwagwa Mboma kali sana, yeye hakuchunguza kwanza kabla ya kutumbukiza kichwa chake? Labda ni fundisho kwa hawa wakuu wengine ambao walipokuwa madarakani hawakujali kabisa japo kuhamasisha vijana kule wanakotoka ili wajiendeleze na kujitegemea. Sasa wamestaafu wanajifanya wanaweza kuleta mabadiliko?

Hongera kwa wananchi wa Mbeya vijijini.

Nyaulawa (RIP)alikuwa a truly mwana Mbeya, asiye na makuu lakini na moyo wa kusaidia wengine ambao hawakubahatika kama yeye.
 
Jamani Mboma alishabwagwa hata kabla ya kura za maoni. alishabwagwa tokana na aliyoyafanya - meremeta, kusababisha uhaba wa sukari, uingizaji wa sukari toka nje, kumrubuni Dr Omar Juma ku-sign proposal feki za kiagiza sukari!
 
.....MIMI NADHANI TUWEKE WAZI MTU YEYOTE ANAYESHIKA NAFASI YA UKUU WA MAJESHI ...AU UNADHIMU MKUU ,MKURUGENZI WA USALAMA..., MKUU WA JESHI LA POLISI ,ets WAKISHAKUWA WAMESTAAFU WASIINGIE KWENYE NAFASI ZA KUGOMBEA..KWANI HAWA INAPENDEZA WAKIENDELEA KULITUMIKIA TAIFA KATIKA NGAZI YA USHAURI...

MBOMA AMEWAAIBISHA WAKUU WA MAJESHI WASTAAFU ...SIJUWI NANI KAMDANGANYA ...HAINGEPENDEZA YEYE KWENDA BUNGENI KUKIMBIZANA NA KINA ZITO....

MKUU WA MAJESHI NA MNADHIMU NI KAMA MARAIS WASTAAFU WANALELEWA HADI WANAKUFA....LAKINI PIA KITENDO CHA MBOMA KUGOMBEA NI FUNZO KWA SERIKALI....INAWASAHAU SANA HAWA WAKUU WANAKUWA IDLE.....IWATAFUTIE ACTIVITIES.....MBALI YA ZILE WANAZOFANYA MASHAMBANI MWAO...
 
Mbona anajua kwamba akijaribu kuingia Chadema hatapata nafasi hata ya kuwa mwanachama .So sijui unasemaje ?Ameoza mno kuwa upande wa pili watu wa aina yake huishia CCM tu .
....Mambo mengine vichekesho kama mtu amestaafu ina maana hata mwajiri wake amemuona anastahili kupumzika sasa mtu kama Mbona bado anataka ubunge nina imani hata uwezo wake wa kufikiri utapungua tu sasa sijui wanakuwa hawajakusanya vijisenti vya kutosha kwa hiyo wanatafuta jinsi ya kuongezea..
 
.....MIMI NADHANI TUWEKE WAZI MTU YEYOTE ANAYESHIKA NAFASI YA UKUU WA MAJESHI ...AU UNADHIMU MKUU ,MKURUGENZI WA USALAMA..., MKUU WA JESHI LA POLISI ,ets WAKISHAKUWA WAMESTAAFU WASIINGIE KWENYE NAFASI ZA KUGOMBEA..KWANI HAWA INAPENDEZA WAKIENDELEA KULITUMIKIA TAIFA KATIKA NGAZI YA USHAURI...

MBOMA AMEWAAIBISHA WAKUU WA MAJESHI WASTAAFU ...SIJUWI NANI KAMDANGANYA ...HAINGEPENDEZA YEYE KWENDA BUNGENI KUKIMBIZANA NA KINA ZITO....

MKUU WA MAJESHI NA MNADHIMU NI KAMA MARAIS WASTAAFU WANALELEWA HADI WANAKUFA....LAKINI PIA KITENDO CHA MBOMA KUGOMBEA NI FUNZO KWA SERIKALI....INAWASAHAU SANA HAWA WAKUU WANAKUWA IDLE.....IWATAFUTIE ACTIVITIES.....MBALI YA ZILE WANAZOFANYA MASHAMBANI MWAO...

Mkuu PM,

Nakubaliana na mengi uliyoandika hapo. Ningeongezea hata Jaji mkuu kwenye hilo kundi.

Mkuu wa majeshi ana network kubwa sana, hivi kweli anaweza kukosa cha kufanya kwenye nchi maskini kama Tanzani? Kwa kushirikiana na NGO anaweza kutoa contributions nyingi sana kwenye jamii.

Hii ya kupewa majukumu mengine na serikali naona haifai. Mbona kuna mambo mengi sana ya maana ya kufanya Tanzania kwa mtu asiye na njaa?
 
Spirit za ukabila utazijua tu,unakuta mtu anasema alikua "Truly mwana Mbeya". Mawzo mengine bwana.

Btw. Mkuu wa majeshi bado anakimbilia kwenye siasa.Sijui lengo lake ni nini,hivi asingeweza kuwasaidia watu bila siasa?
 
Labda alikuwa anataka uwaziri-ulinzi; maana kwa kazi aliyoifanya kutaka ubunge ni kuji-insubordinate kwa hali ya juu kabisa! On the other hand, yote hii ni matokeo ya nchi yetu kuathirika na siasa-watu hawaoni kama wamefanya cha maana katika jamii hadi wawe wanasiasa.
 
Nakubaliana na Jibaba Bonge kwamba Mboma alianguka mapema, wananchi walikuwa wakihoji alichoifanyia Mbeya Vijijini akiwa kwenye nyadhifa za juu jeshini kwani hawaoni chochote alichowafanyia. Mwananchi mmoja alifikia hatua ya kusema hajawahi hata kupeleka kijana mmoja jeshini.

Ukweli huo aliuthibitisha mwenyewe alipoulizwa swali "Umeisaidiaje Mbeya ukiwa Mkuu wa Majeshi?" majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo, " Nisingeweza kutumia kasma ya jeshi kusaidia Mbeya Vijijini, si kazi ya mwanajeshi kushiriki katika maendeleo, lakini mkinichagua nitashiriki."

Tatizo lake kubwa ni kwamba hata huko kijijini kwake hakuwa na kawaida ya kwenda na hakuwa akivifahamu vijiji vingi kiasi cha kufika hatua ya kushangaa alipofika kijiji kilichoko mlima Loleza kwamba hata huku kuna watu!

Ni kweli kabisa ingetungwa sheria ya kuzuia baadhi ya nyadhifa kutoingia kwenye siasa wanapostaafu.
 
Mkuu PM,

Nakubaliana na mengi uliyoandika hapo. Ningeongezea hata Jaji mkuu kwenye hilo kundi.

Mkuu wa majeshi ana network kubwa sana, hivi kweli anaweza kukosa cha kufanya kwenye nchi maskini kama Tanzani? Kwa kushirikiana na NGO anaweza kutoa contributions nyingi sana kwenye jamii.

Hii ya kupewa majukumu mengine na serikali naona haifai. Mbona kuna mambo mengi sana ya maana ya kufanya Tanzania kwa mtu asiye na njaa?

Wandugu, inategemea na Elimu na upeo. Hwa viongozi wengine ukiondoa vyeo walivyo/kuwa navyo ni bure kabisa.
 
Back
Top Bottom