Gen. Mboma ajaribu kugombea, aangushwa!

Rejea Mradi mzima wa Meremeta (vielelezo vyote vimo humu JF), then ukimaliza angalia tenda nzima ya Radar ya Jeshi, kisha angalia tenda ya Helikpta za Jeshi, ukimaliza kama una swali lingine karibu.

I love JF . . . . . Nakupata Mkuu, tuko pamoja!
 
Next time, msishangae kusikia Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samata naye amejitosa kwenye ubunge kupitia CCM. Then, mwenyekiti mstaafu wa tume ya uchaguzi, former msajili wa vyama vya kisiasa, the list goes on and on and on........This recycling is too much.

Hata Tibaigana alishawahi kugusia hilo
 
Tibaigana alishatangaza ataingia kwenye siasa 4 now naona anasubiri jimbo
 
Na nafikir iagenda ya chama tawala kupata makada 'wenye nguvu' hasa hawa waliowahi kushika nafasi nzito nzito inatimia!
 
Bungeni ndiko Mafisadi wanakojificha.Lowassa,Rostam, chenge, Karamagi ,Mungai,Mramba na wengine wengi ndio maana BWM hana wasiwasi wa kuondolewa kinga kwani mafisadi bungeni wamewazidi wabunge waadilifu. Sasa Mboma anataka kujiunga nao ili iwe vigumu zaidi kumkabili kuhusu Meremeta na kama mnavyojua Apson yeye ameona amtumie mwanae ambae baada ya kushindwa, akateuliwa na Muungwana kuwa mbunge!! Bunge ni kichaka cha ufisadi na ndio maana Makamba alikuwa anataka kumuingiza Manji huko ili timu yao itimie.
 
hehehe hii ngoma kusema kweli naona ndio kwanzaaa inachanganyia....so ngoja wengine tujivute kwenye screen..

dats why i like JF yaani mkubwa yeyote maovu yake yapo nje nje!

na bado kutakua na watu wa kuwatetea no matter wat!i like their spirit kwa kweli!

haya endeleeni kutuhabarisha juu ya huyu mkulu n associates wake!
 
Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana ki akili na na vilevle ana busara si za kawaida, nafikiri kwa kupata ubunge atasaidia watu wengi sana, huko Mbeya, Bungeni, serikalini hata Nchi nzima , lazima tukumbuke bila wazee wenye vipaji na busara nzito kama za huu mzee tunaweza kupoteza mengi.
 
Ubarikiwe, milele amina.
 
Busara my ass.
 
Inabidi ueleze busara hizo ni zipi. Eleza au onesha lolote unaloweza kuliita la busara alilofanya mpaka ukamuita ana busara. Data zipo zitaanza kumwagawa soon, ujue ukweli kama kwako hizo ndio busara.
 
Hivi Mtikila nani alikwambia ukachukue pesa kwa RA????

Ingekuwa zamani, tayari tungeshapata askari wa kumdhibiti huyu afande mstaafu!!!!!!!!!!!
 
Mkuu, watu wa Mbeya wanajua yote: wanajua kuwa MBOMA NI FISADI, tena siyo fisadi tu, bali FISADI NAMBARI MOJA, ambaye jina lake jeshini linanuka kwa rushwa na ubadhirifu.

Mali anazomiliki ni nyingi sana ikiwemo Petrol Station ya Mbeya aliyojengewa na Balhabou wa Morogoro kama asante kwa kuwapa tenda zote za jeshi kuanzia mafuta hata kusupply buti za jeshi! Habari za ukakika ni kuwa anaungwa mkono na mlinzi wa mafisadi ndani ya CCM, MAKAMBA!

Hii ni bahati kubwa kuwa anagombea ili tumwanike hadharani kisawasawa. Hata yule rafiki yake fisadi APSON MWANG'ONDA wa usalama wa Taifa, naye anataka kuwania kiti cha Mbozi Mashariki. Tunamsubiri kwa hamu kumwonesha kuwa yeye ndiye KAGODA nambari wani ambaye kwa sasa anastahili kuwa jela!

Mkuu Fataki,

Umemwaga habari mpya hapo, Apson anataka kuwania Mbozi Mashariki? Tuhabarishe mkuu. Mwaka 2010 tutasikia na kuona mengi sana.

Japo Mboma ana haki ya kugombea kama raia mwingine yeyote, lakini hivi kweli kwa mazingira ya Tanzania, ambapo mkuu wa zamani wa jeshi bado anaendelea kulipwa na kupewa huduma kibao na jeshi, itakuwa sawa kuwa Mbunge?

Kama ni kuisaidia Mbeya vijijini, kwa Mboma kupitia cheo chake cha zamani na NGO yake atakuwa na uwezo mkubwa wa kusukuma maendeleo ya Mbeya vijijini kuliko hata akiwa Mbunge wao.

Huko mbele inaelekea wastaafu wote watataka kuishia bungeni. Walianza wakurugenzi waliofilisi mashirika ya umma, sasa wamekuja madiplomasia, wanajeshi, mapolisi, muda sio mrefu hata jaji mkuu ataamua kugombea ubunge.
 
Mkuu, watu wa Mbeya wanajua yote: wanajua kuwa MBOMA NI FISADI, tena siyo fisadi tu, bali FISADI NAMBARI MOJA, ambaye jina lake jeshini linanuka kwa rushwa na ubadhirifu.

Mali anazomiliki ni nyingi sana ikiwemo Petrol Station ya Mbeya aliyojengewa na Balhabou wa Morogoro kama asante kwa kuwapa tenda zote za jeshi kuanzia mafuta hata kusupply buti za jeshi! Habari za ukakika ni kuwa anaungwa mkono na mlinzi wa mafisadi ndani ya CCM, MAKAMBA!

Hii ni bahati kubwa kuwa anagombea ili tumwanike hadharani kisawasawa. Hata yule rafiki yake fisadi APSON MWANG'ONDA wa usalama wa Taifa, naye anataka kuwania kiti cha Mbozi Mashariki. Tunamsubiri kwa hamu kumwonesha kuwa yeye ndiye KAGODA nambari wani ambaye kwa sasa anastahili kuwa jela!

Kaaaazi kwelikweli.
Kumbe kituo kile cha Mafuta alikijenga Balhabou wa Moro? Unajua niliambiwa na jamaa zangu kwamba jenerali huyu mstaafu anamiliki kituo cha mafuta pale jijini Mbeya, kipo eneo la forest mpya, katika kituo cha Daladala cha Kadege, ukitoka mafiat kama unaenda Meta kipo upande wa kushoto.
I like JF!

Rejea Mradi mzima wa Meremeta (vielelezo vyote vimo humu JF), then ukimaliza angalia tenda nzima ya Radar ya Jeshi, kisha angalia tenda ya Helikpta za Jeshi, ukimaliza kama una swali lingine karibu.

Kwa faida ya wengine, ufafanuzi wa mradi mzima wa MEREMETA uko hapa "https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/21200-cheche-ya-mboma-meremeta-na-apson.html" na hapa bofya ili upate kujua tunaongelea nini.

Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana ki akili.....

.....sawa, unaweza kutusaidia kutuonesha. Hapa hatufichi kitu

.....na vilevle ana busara si za kawaida,

....sikatai, ila busara hizi zingemtuma kupumzika kuongoza umma, kwani jamii bado inahitaji busara zake akiwa ametulia kwake na kulea wanae, sio kukurupushana na kampeni za majitaka za anazozikimbilia sana katika chama chake.....

.... nafikiri
kwa kupata ubunge atasaidia watu wengi sana.....

...kwa sababu unafikiri, hapa sina hoja kubwa ila sidhani kama uko sahihi, ukichukulia historia ya nyuma ya Jenerali huyu.

...... lazima tukumbuke bila wazee wenye vipaji na busara nzito kama za huu mzee tunaweza kupoteza mengi.

....sawa, lakini nitaendelea kuhoji kwamba, kwani bila yeye kuwa madarakani hatuwezi kuzipata busara zake? Hatuna ruhusa ya kumfuata kwake na kuchota 'Busara' zake?

By the way, ule mradi wake wa utafiti wa makaa ya mawe kule Mbozi unaendeleaje?
 
Back
Top Bottom