Gazeti la Dira: Kashfa ya kuhongwa - Zitto, Ole Sendeka, Sarah Msafiri na Anne Kilango watajwa

wanaume wa tanzania ni wanafiki kwa kila kitu....hii nchi haitokaa iendelee hadi wanaume wote watoke madarakani....yanajivalia tu suti kichwani wizi mtupu

Mbona hapo 'Gender' imebalance....Zitto na Ole Sendeka vs Sara Msafiri na Anne Kilango! Hili si tatizo la jinsia fulani, waume kwa wake...waTanzania wengi wezi! We angalia mtu akichaguliwa/teuliwa kushika nafasi ya uongozi...magazeti yaandika ' Fulani Kaula'...Kaula nini rtumemkabidhi majukumu mazito? Lakini kwa sababu mentality yetu ni 'wizi mtupu' tunaona mtu sasa 'kaula' kwani kapata nafasi ya kuiba aka 'kula'!
 
Zitto hakuhusika isipokuwa kuna shinikizo la kumuweka kwenye list ili kukidhi matakwa ya kisiasa.

Hummer,Vogue,Ghorofa kayatoa wapi? Kwa mshaara upi? Kwa mkopo upi? Hummer ni kama mil300 hv,Vogue nayo 150 mpaka 200 bado V8 mil80,ghorofa 400m piga total hapo karibia 1bil,sasa katoa wapi fedha hizo,huyu nyepesi lisemwalo lipo bwana!!
 
Kwaupande mwingine Katibu mkuu wa CDM Dr. Slaa amesema ikiwa itabaunika wabunge wake watakutwa na hatia watachukuliwa hatua kali za kichama.

Huu ni unafiki wa Slaa tuliouzoea,kwa nini siku zote hizo hatua kali za kichama zisichukuliwe against wabunge wa Chadema wanaopokea posho bungeni ilhali waliwadanganya watanzania msimamo wa chama ni kukataa posho! Au hawajui kwa majina wabunge wanaopokea posho? Acheni unafiki,shame on you!
 
Kwa bahati mbaya tuna Spika dhaifu kushinda maelezo. Lazima ata-mismanage hii kitu. Hata jinsi alivyo-handle hoja ya Vita Kawawa na kuvunja kamati ya Nishati ameacha maswali mengi sana. Ndio shida ya kupeana kazi mezani. Yeye mwenyewe Spika hana intergrity ya kukalia hicho kiti.

ninamsubiri a-mismanage!..na kuna kila dalili ya ku-mismanage!..
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mbona hapo 'Gender' imebalance....Zitto na Ole Sendeka vs Sara Msafiri na Anne Kilango! Hili si tatizo la jinsia fulani, waume kwa wake...waTanzania wengi wezi! We angalia mtu akichaguliwa/teuliwa kushika nafasi ya uongozi...magazeti yaandika ' Fulani Kaula'...Kaula nini rtumemkabidhi majukumu mazito? Lakini kwa sababu mentality yetu ni 'wizi mtupu' tunaona mtu sasa 'kaula' kwani kapata nafasi ya kuiba aka 'kula'!
huyo anne malecela na mwenzake wamerubuniwa na waume zao kupokea hizo hela...
 
Hummer,Vogue,Ghorofa kayatoa wapi? Kwa mshaara upi? Kwa mkopo upi? Hummer ni kama mil300 hv,Vogue nayo 150 mpaka 200 bado V8 mil80,ghorofa 400m piga total hapo karibia 1bil,sasa katoa wapi fedha hizo,huyu nyepesi lisemwalo lipo bwana!!

Toa ushahidi wa Zitto kumiliki hivyo ulivyotaja. Tabia ya Mtu mzima kusubiri watu wengine wafikiri kwa niaba yako haifai. Hizi siasa majitaka zitawafikisha wapi? Na utafaidika na nini kwa hizi siasa majitaka!
 
Huu ni unafiki wa Slaa tuliouzoea,kwa nini siku zote hizo hatua kali za kichama zisichukuliwe against wabunge wa Chadema wanaopokea posho bungeni ilhali waliwadanganya watanzania msimamo wa chama ni kukataa posho! Au hawajui kwa majina wabunge wanaopokea posho? Acheni unafiki,shame on you!

Hivi posho ya kikao ni shilingi ngapi hasa?
150,000,200,000,300,000 au ngapi mwenye kujua atufahamishe.
 
Dira wametaja majina ni kwasababu hawajapewa mgawo, wakipewa 2 hawaandiki tena, mi nimekosa imani pia na haya magazeti yanayonunuliwa ili yatoe habari zao nzuri 2 kama mwananchi lilivyojithibitisha ktk kutoa hbr za Zitto
 
Huwa wanakuomba kula sio kura, sema wewe hujui tu
kweli mkuu..ila imetia doa sana, hakuna wa kumwamini tena, halafu nimegundua wale wanaojipambanua kwa makelele mbele ya jamii, wala rushwa wakubwa,,,yaani wanahongwa tena kwa kujirahisi kama makahaba..pumbavu zao
 
Nipo kwa hamu kumjua nani anapeleka nguzo za umeme za mbeya na iringa huko kenya halafu anazirudisha tena tanzania na kusema zimetoka south afrika...yaani huy akanunue risasi mwenyewe, mi nitakuja kumaliza!!
duh?huu usanii unatisha
 
Habari kuwa kuna wabunge wa upinzani wanaohusika kuihujumu TANESCO zimepokelewa kwa masikitiko makubwa sana na imewafanya wananchi wengi kukata tamaa. Kwa ufupi wananchi tulikuwa tunawaunga mkono vyama vya upinzani tukijua wana dhamira ya kuleta mabadiliko na hatimaye kuboresha maisha ya watanzania. Kinachoonekana kutokana na taarifa za Waziri Sospether Muhongo ni kwamba hakuna tofauti kati ya CCM na vyama vya upinzani kwani lengo lao ni moja tu kutumia rasilimali za watanzania kunufaisha matumbo yao na familia zao in the expense ya maumivu na matatizo ya watanzania. Hii ni dhambi kubwa. Binafsi nimebaki njia panda kuhusu kwa nani watanzania tuweke matumaini yetu kuhusu mustakabali wa maisha bora kwa kila mtanzania. Watanzania tunasalitiwa na viongozi waroho ambao kwa wananchi wanajidai kondoo kumbe ndani ni Mbwa mwitu wabaya. Kwa viongozi wa namna hii tusitarajie tena mabadiliko hata kama CCM tutaiondoa kwani tunafanya yale yale yanayotufanye tupigane usiku na mchana kukiondoa chama dhalimu CCM madarakani. Si mambo ya kufumbia macho kwa sababu ya ushabiki wa kichama bali kutumia jicho la pili kuona upande mwingine wa shilingi na kufanya maamuzi yatakayo rudisha heshima ya vyama vinavyohusika na hatimaye kurudisha matumaini kwa waTZ. Viongozi hawa watajwe hadharani na wapewe adhabu inayostahili na wasipewe tena nafasi ya kuongoza kwani wamekosa adabu na credibility. Hii haina tofauti na kuku kula vifaranga wake.
Mtaani kwangu watu wamebaki na maswali mengi kuliko majibu na yanatakiwa yapate majibu kutoka kwa viongozi hawa hawa kwani doa lililosababishwa na wahusika ni kubwa sana.

Rushwa ni mtu binafsi na sio chama. Issue ni chama kinachukua hatua gani inapoonekana mwanachama wake amechukua rushwa. Macho na masikio tuangalie chama cha upinzani kitafanya nini pindi wabunge wake wakigundulika wamechukua rushwa. Nadhani tunaweza kuwapima kwa hilo. Kwa CCM sishangai sana kwasababu karibu wote waliingia kwa kutoa rushwa kwahio kama jadi yao kupokea kwao siyo issue.
 
sasa ni kuumbuana tu,kashfa zote ni za kweli na zinafanyika kila siku ila wakubwa wamezidiana kwenye kuiba sasa wanaanikana.
 
Huu ni unafiki wa Slaa tuliouzoea,kwa nini siku zote hizo hatua kali za kichama zisichukuliwe against wabunge wa Chadema wanaopokea posho bungeni ilhali waliwadanganya watanzania msimamo wa chama ni kukataa posho! Au hawajui kwa majina wabunge wanaopokea posho? Acheni unafiki,shame on you!

Msimamo wa Chama ukikiukwa sio kosa la jinai.....Rushwa ni kosa la Jinai...Kula rushwa na kukiuka msimamo wa chama ni vitu viwili tofauti!
 
if you see someone acting cagey; they have something to hide!!!!!!!!!!
 
Wabunge wote waliotajwa yaani hamna haja ya kuuliza ukijaribu kuangalia mienendo yao kwa Bunge la sasa unaweza kupata majibu.. Tukumbuke enzi zile Zito alikuwa akisimama tu hata Sita alikuwa anapey attension..Lakini recent amekuwa mchadhaifu tu na siasa za kishabiki tena akitanguliza maslahi yake binafsi..ukija kwe Anne Kilango alikuwa naye ni mwiba mzuri kwa serikali kwa misimamo yake,,Ole Sendeka najua wote mtamkumbuka alivyodili na EL na Jairo..wote hawa siku hizi wamekuwa wakiegemea michango ya kimipasho zaidi hamna tena kuongelea ufisadi au udhaifu wa serikali. Kilango siku hizi amakuwa mti wa ndiooooo na kupiga makofi ya kishabiki. No way tunaweza kuwaamini tena tumewapa nafasi mkazichezea its time to get out of the pool waingie wengine..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom