Mimi siamini kuwa Zitto kachukua chochote, isipokuwa kiherehere chake cha kujiingiza katika mgogoro kati ya wizara na tanesco ndivyo vimemponza. Lilikuwa kosa kusema Mhando arejeshwe kazini bila kujua ukweli kuwa Mhando ana ufisadi alioufanya. Ninajua kuwa laiti Zitto angejua ufisadi huo, asingekimbilia kumtetea. Sasa mdogo wangu Zitto, huna wa kumlaumu, ni wewe mwenyewe, acha kiherehere, mtu anayetaka urais huwa hasemi sana, wewe humwoni mwenzako Lowasa yuko kimya!!! ama humuoni Slaa yuko kimya!!!. Tulizana. sasa umeshanuka sana, itakugharimu sana kujijenga tena.