Gazeti la Dira: Kashfa ya kuhongwa - Zitto, Ole Sendeka, Sarah Msafiri na Anne Kilango watajwa

ni bahati mbaya wengi humu hamfahamu kinachoendelea...na wakifanikiwa mtayumba sana.
 
hii nchi! bora kusiwe na rais wala serikali, ingewezekana tukajiongoza wenyewe! naitema puuuuuu!
wanaume wa tanzania ni wanafiki kwa kila kitu....hii nchi haitokaa iendelee hadi wanaume wote watoke madarakani....yanajivalia tu suti kichwani wizi mtupu
 
Habari kuwa kuna wabunge wa upinzani wanaohusika kuihujumu TANESCO zimepokelewa kwa masikitiko makubwa sana na imewafanya wananchi wengi kukata tamaa. Kwa ufupi wananchi tulikuwa tunawaunga mkono vyama vya upinzani tukijua wana dhamira ya kuleta mabadiliko na hatimaye kuboresha maisha ya watanzania. Kinachoonekana kutokana na taarifa za Waziri Sospether Muhongo ni kwamba hakuna tofauti kati ya CCM na vyama vya upinzani kwani lengo lao ni moja tu kutumia rasilimali za watanzania kunufaisha matumbo yao na familia zao in the expense ya maumivu na matatizo ya watanzania. Hii ni dhambi kubwa. Binafsi nimebaki njia panda kuhusu kwa nani watanzania tuweke matumaini yetu kuhusu mustakabali wa maisha bora kwa kila mtanzania. Watanzania tunasalitiwa na viongozi waroho ambao kwa wananchi wanajidai kondoo kumbe ndani ni Mbwa mwitu wabaya. Kwa viongozi wa namna hii tusitarajie tena mabadiliko hata kama CCM tutaiondoa kwani tunafanya yale yale yanayotufanye tupigane usiku na mchana kukiondoa chama dhalimu CCM madarakani. Si mambo ya kufumbia macho kwa sababu ya ushabiki wa kichama bali kutumia jicho la pili kuona upande mwingine wa shilingi na kufanya maamuzi yatakayo rudisha heshima ya vyama vinavyohusika na hatimaye kurudisha matumaini kwa waTZ. Viongozi hawa watajwe hadharani na wapewe adhabu inayostahili na wasipewe tena nafasi ya kuongoza kwani wamekosa adabu na credibility. Hii haina tofauti na kuku kula vifaranga wake.
Mtaani kwangu watu wamebaki na maswali mengi kuliko majibu na yanatakiwa yapate majibu kutoka kwa viongozi hawa hawa kwani doa lililosababishwa na wahusika ni kubwa sana.

Mkuu mvumbuzi bado hujavumbua,kwa akili yako unataka kutuaminisha kwamba tuendelee na mfumo wa kifisadi ambao hauwezi kuwajibishana badala yake ni wa kulindana?na je unadhani vyama vya upinzani ni malaika?tunachoangalia ni mfumo upi na kina nani wanausimamia,wote ni binadamu hata akiwa upinzani,ila kikubwa chama kipi kina mfumo unaopinga ufisadi kwa dahti?na ili tujue ni kwa dhati ni pale tunapoona utekelezaji wa yale makatazo,mfano ukisoma katiba ya ccm rushwa kwao wanasema ni mwiko kwa kuwa ni adui wa haki,je hili wanalikemea,je wanalisimamia,je wanachukua hatua stahiki kwa wale wanaotenda kinyume?je ni maovu mangapi makubwa na ya wazi ambayo wameshindwa kuwawajibisha waliohusika?walitangaza kujivua gamba leo iko wapi?rushwa ya rada tunaambiwa hela zimerudishwa lakini aliezichukua au kusababisha upotevu huo hajulikani?je kachukuliwa hatua gani?ninachotaka kupingana na wewe ni kutuaminisha kwamba hata tukibadili utawala na tukajielekeza kwa wapinzani mambo yatakuwa yale yale,kwa hiyo unadhani hakuna suluhu?na je tuendelee hivihivi milele yote?HAPANA MVUMBUZI,we need changes and yes we can kwa nguvu ya umma
 
January Makamba hayumo kwenye hili swaga? yeye si ndio alikua mwenyekiti wa kamati hii?
 
Gazeti la Dira la leo limewataja wabunge wanasadikiwa kulamba mlungula ambapo kwa mujibu wa gazeti hilo wamo Zitto kabwe ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wakutisha ikiwapo nyumba kadhaa na magari ya kifahari, wengine waliotajwa ni Ole Sendeka na Mama Kilango Malecela ambao ndiyo wapiga kekele wakubwa wa ufisadi kumbe usanii tu.

Kwaupande mwingine Katibu mkuu wa CDM Dr. Slaa amesema ikiwa itabaunika wabunge wake watakutwa na hatia watachukuliwa hatua kali za kichama.

zito kabwe, rushwa ni moja ya sababu ya uadilifu iliyokufanya utangaze bungeni kuwa unautaka urais. hivi tu mbunge unatisha kwa rushwa je ukiwa magogoni c utakuwa mobutu seseseko kuku ngbendu wa zabanga!
 
Kaaaazi kweli kweli, ndo maana siku ile kamati inavunjwa Zitto alionekana mpoleee na pia zile kashfa wakati zatajwa kaonekana kuloa kinoma, mwenendo wa Zitto cdm na mihela yake zilikuwa zatia shaka, nasikia anamiliki Hummer na magari kibao ya kifahari daaaah, kweli njaa kitu kibaya.Mi nashauri cdm wamfukuze uanachama maana ni tatizo muda mwingi.
 
Kwanini slaa ndio akurupuke kutoa matamko na sio mnyika mwenye wadifa huo kichama? kuelekea 2015 tutaona mengi

sikiliza we uamsho, hizi tuhuma ni nzito lazima zitolewe ufafanuzi na kiongozi mkuu wa chama. mbona huko magamba kwenu kaziongelea pius msekwa? acha hisia mbaya.
 
Gazeti la Dira leo limekuwa lulu kwa Pro-Chadema ha haa haaa tutasikia mengi kuelekea uchaguzi.
 
ni bahati mbaya wengi humu hamfahamu kinachoendelea...na wakifanikiwa mtayumba sana.

Nahisi hiki kitanzi cha sasa kinaweza kuwa the most difficult one kuvuka - kwa pande zote. Tuombe mungu aingilie kati.
 
Gazeti la Dira la leo limewataja wabunge wanasadikiwa kulamba mlungula ambapo kwa mujibu wa gazeti hilo wamo Zitto kabwe ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wakutisha ikiwapo nyumba kadhaa na magari ya kifahari, wengine waliotajwa ni Ole Sendeka na Mama Kilango Malecela ambao ndiyo wapiga kekele wakubwa wa ufisadi kumbe usanii tu.

Kwaupande mwingine Katibu mkuu wa CDM Dr. Slaa amesema ikiwa itabaunika wabunge wake watakutwa na hatia watachukuliwa hatua kali za kichama.

Ndiyo maana alikuwa anaulilia urais kila wakati ili aweze kuchota fedha za walalahoi.Ni wachache sana nchi hii wenye uchungu na nchi hii na siyo kama akina Zitto.Hao ni wapiga debe tu ili wapate mwanya wa kuwadanganya wananchi ili wajichotee pesa kiulaini.
Wananchi amkeni.
 
Zitto!? Sikubaliani na msimamo wake sometimes lakini hili la kula mlungula ngumu kuamini!

Hata mimi kuhu zitto siamini hii hadi pale ushahidi wa wazi utakapo tolewa.

Sent from my Z3 using Tapatalk 2
 
hivi ni nani aliyenunua kiwanda cha chai lupembe pale iringa?
kwa sababu kulikuwa na makala itv ikionyesha malori yake yakipakia nguzo ktoka shambani na kudai ni kuni za kukaushia chai.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom