Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,902
- 944
MBOWE ADHARIRIKA HAI, WANANCHI WAMKIMBIA UWANJANI
Freeman Mbowe amekosa kabisa uungwaji mkono kwa wananchi wa Hai kutokana na kukaa kwake kwenye ubunge kwa Miaka 20 bila kuwasemea wananchi wapate Maendeleo na badala yake Wananchi wamegeukia kwa Mbunge wao wa sasa, Mhe. Saashisha Mafuwe ambaye ameonekana kuwapa kipaumbele sana Wananchi.
Katika hali ya kusikitisha na kutia huruma sana, Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kuishiwa hoja, Freeman Mbowe anadai kuwa Kanda ya Kaskazini yote imetengwa kimaendeleo, Inaonekana wazi hajui chochote kuhusu Hai kama ambavyo alikuwa Mbunge na hakuwa na muda wa kuwajali wananchi wa Hai. Je, ni kweli Mbowe hana macho ya kuona na kutazama hatua nzuri za maendeleo jimboni Hai? Mbowe kuwa mkweli.
Swali la kujiuliza, Freeman Mbowe aliyekaa kwenye Ubunge kwa takribani miaka 20 na bado alishindwa kutatua changamoto zinazotatulika, Je, ridhaa ya miaka mitano anayoomba ataweza? Ni wazi, Mbowe hataweza. Changamoto zilizodumu miaka 20 ya Ubunge wake ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wa Mbunge hakuzitatua na badala yake zimetatualiwa na Mhe. Saashisha Mafuwe ndani ya miaka mitatu na miezi mitatu.
Wananchi wa Jimbo la Hai walikuwa na Changamoto ya mgogoro wa Ardhi (KIA), Miradi ya Elimu, miradi ya afya, Viwanda vya Vyuma kufufuliwa, Barabara, madaraja, wakulima na wafanyabiashara. Haya yote ni kazi ya Mbunge kuyasemea Bungeni lakini kwa Freeman Mbowe hili tu lilimshinda kwa miaka 20. Saashisha Mafuwe ameweza ndani ya Miaka mitatu tu.
Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai, Mbunge kijana ambaye ametokea kuikonga mioyo ya Wana Hai kwa kuwasemea kwa bidii Bungeni hali iliyopelekea miradi ya maendeleo lukuki kutekelezwa na Serikali na kuleta suluhisho la kutatua changamoto jimboni Hai ambaye anatumia muda wake mwingi kukaa na wananchi na siyo kumzungumzia Freeman Mbowe
Itakumbukwa kuwa, Saashisha Mafuwe ndiye Mbunge pekee mpaka sasa ameuliza maswali mengi Bungeni kuliko Mbunge yeyote katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii ni kutokana na kiu ya mafanikio anayotaka kuyaona ndani ya Jimbo la Hai kwani amedhamiria hasa kutatua changamoto za wananchi wa Hai.
Wananchi wa Jimbo la Hai wamesema wao wanataka vitu vya maendeleo kama ambavyo anafanya Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe na wananchi wanamuunga mkono kwa asilimia kubwa sana.