Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Sikonge,
Nilisoma na L Nducha huku Bukoba - Ndolage Nursing School - Hivi yupo wapi siku hizi?
Baba Enock,
Mwanzo nilikuwa nafahamu kuwa Nducha ni watu wa Sikonge. Baadaye yule mama wa kupika chai akawa kimya. Nafikiri walijahamia Mpanda / Urwila kama sikosei. Ila nilipokuwa Arusha nikawafahamu hao nducha wawili mtu na nduguye. Mmoja wazazi wake wakiishi Mpanda (Mlokole wa Kisabato na Fundi mchundo ujenzi) na mwingine wazazi wake wakiishi Kibaha (yeye akisomea Umeme). Tangu miaka ya 80 mwishoni nimepotezana nao hadi leo. Mwaka 90 niliishi na huyo kijana nimeandika Mdoe na baba yake tukimwita shemeji kwa kuwa kaolea hiyo familia ya Nducha. Mtu wa mwisho kumuona alikuwa Nducha mmoja akifanya kazi Wizara ya Sayansi, tech na elimu ya juu. Huyu alikuwa ni baba yao mdogo kama sikosei. Kutoka hapo sikupata habari zao zozote hadi nilipokuja kusoma humu ndani kuwa kuna Flora Nducha mtangazaji wa BBC.
Kama wamhitaji sana huyo jamaa basi naweza kutafuta simu ya huyo A. Nducha na ninauhakika ataweza kukupa maelezo ya huyo L. Nducha kwa sasa yuko wapi na anwani yake. Huyo A. niliambiwa ni kaka yake wa kuzaliwa FLora.