Wasanii wa Tanzania mnakwama wapi kwenda kimataifa? Jifunzeni kwa Diamond Platinum

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
313
872
Mwaka 2010, jina la la Diamond Platinum lilichomoza kwenye vyombo vingi vya burudani kwa wimbo wake uliokuwa mkali kipindi hicho "Kamwambie".
Ilimuchukua Diamond miaka 4 kupambana kwa kuimba sana nyimbo nzuri mpaka 2014 alipopata collabo kubwa ya kimataifa na Davido kwa wimbo wake "number one remix"
Baada ya hapo ilikuwa ni story za mafanikio tu katika safari yake ya mziki kwa kushirikiana na wasanii wakubwa wa Nigeria wakiwamo akina Kcee, Tiwa Sawage, Blanketi, Psquare, Mr Flavour, Patoranking, na wengine kibao kutoka nchi mbalimbali Afrika na duniani.

Sasa wasanii wengine wa kitanzania mnakwama wapi kutoboa kimataifa huku mfano ulio hai (Diamondi Platnumz) angali mpo nae hapo Dar es salaam?

Msanii unakuta umekaa zaidi ya miaka 5 hadi 10 za kuwa peak ila huna connection (collabo) za kimataifa, na hata kama umefanya collabo moja ya kimataifa, project inayofuata, wimbo unakuwa local kweli kiasi kwamba kuvuka boda inakuwa ngumu kweli.

Leo hii, Diamond Platinum akisema anasitafu mziki, Tanzania music inarudi local kama zamani huku mziki wa Kenya na Uganda utatawala hapa Afrika mashariki kama enzi za akina Jose Chamilione, Zig D, Craftmaniaz, Longombaz n.k walivyo kuwa wanasikika hapa Tanzania kuliko wasanii wa kitanzania.

Nini kifanyike!!
Wadau watatoa maoni, ila kwa upande wangu ningepata nafasi ya kuwashauri wasanii wetu ningewambia yafuatayo;
1. Wasanii wa kitanzania wawekeze sana Nigeria. Nigeria ni giant wa mziki wa Afrika hivyo plan zao zote ziwe kufika na kufanya kazi nyingi na wasanii wa Nigeria (hapa ndipo siri ya Diamond Platinum ilipo na ukubwa wake Afrika)

2. Wasanii fanyeni media tour hasa kwenye nchi ya Nigeria. Hapa ni pamoja na msanii kuandaa angalau bajeti ya wiki 2 hadi mwezi mmoja kukaa Nigeria ukipita kwenye kila redio na Tv kama utaweza na kutangaza nyimbo zako.
Baadhi ya wasanii wa Tz tayari mna connection na wasanii wa Nigeria mfano -Nandy ulishawahi kufanya kazi na Joeboy na Oxlade hawa wote hawashindwi kukaribisha Nigeria kufanya media tour na kukupa connection ya collabo kwa wasanii wengine.
-Ali kiba ulishawahi kufanya kazi na Patoranking sioni ukishindwa kwenda kupiga kambi Nigeria.
-Rayvany na Harmonize hawa wana connection ya wasanii wengi tu Nigeria kama Ruger, Kizz Daniel najua mkitenga bujeti ya mwezi mzima Nigeria kupiga kambi sioni mkishindwa.
- Jux, Mario, Mbosso, Zuchu, Jay Melody, Mavokali, Young Lunya, Aslay na wengine naamini mkiomba connection kwa Chibu Dangote awaunganishe na marafiki zake (wasanii) wa Nigeria kwa ajili ya kukuza mziki wa Tanzania kimataifa naamini atawapa connection hizo maana yeye mwenyewe anapenda kuona kwenye soko la kimataifa wasanii wa kitanzania wanakuwa wengi.

2. Kimbieni mkimbiavyo lakini huwezi kuondoa lugha ya kiingereza kwenye soko la kimataifa. Hivyo katika nyimbo zenu hakikisheni lugha ya kiingereza kinatumika hasa kwenye chorus ambayo itaimbwa mara kwa mara na watu wa mataifa mbalimbali. Ukimshirikisha msanii wa nje hakikisha yeye unampa verse ya kwanza kwa sababu yeye atatumia lugha ya kiingereza katika verse hiyo ya kwanza na hivyo wengi wa watu wa mataifa mbalimbali watafatilia nyimbo hiyo hata kama wewe msanii wa bongo ukitiririka verse zinazofuata kwa kiswahili haitakuwa na shida kwa sababu kwa wakati huo huo una promote lugha yetu adhimu ya kiswahili.
 
Siri ipo kwenye kingreza sasa hata kumwandikia ujumbe huwezi itakuwaje kwa mfano.
 
Ye daimond kumpata davido aliunganishwa na Nani? kwa unavyojua mkanda na alimlipa au alifanya ngoma bure tu?
 
Naomba nikuulize swali mtoa mada,ww kwenye fani yako unayoifanya hupo kimataifa? kama haupo ni kwanini na kama hupo ulifanyaje ukafika hapo?
 
juulNaomba nikuulize swali mtoa mada,ww kwenye fani yako unayoifanya hupo kimataifa? kama haupo ni kwanini na kama hupo ulifanyaje ukafika hapo?
Nipo naandaa project zangu za kimataifa hivyo soon nitakuwa huko kwa uwezo wa Mungu
 
Kweli anastahili kupewa maua lakini sio leo...hadi hapo mwenyezi Mungu atakapo mchukua.
 
Back
Top Bottom