Eti Kisukuma kina wazungumzaji wengi kuliko Kiswahili

Kuhani I guess here you owe some of us an apology...sayansi ya utabiri wa hali ya hewa ...kusema hauna kipimo ni kuwadhalilisha wataalamu waliokula buku - kuanzia meteorological assistants, meteorological officers hadi meteorologists - humo humo ndani wapo weather forecasters na weather analysts. Duh, umeniangusha Mkuu Kuhani lol.

Aaaaaa, hujanielewa Mkuu, nimesikitika na mimi pia.

Sikusema utabiri wa hali ya hewa ndio hauna vipimo, ila yule mchangiaji ndio niliona "anarusha rusha namba hewani kama utabiri wa hali ya hewa usio na vipimo," nikimaanisha kwamba yeye huyu ndio hatumii vipimo, kama Sheikh Yahya anaposema mwaka huu kutakuwa na ukame, au unaangalia juu unaona kiwingu kinene unasema mvua yaja, kiasi gani hujui, saa ngapi hujui, gueswork, you know. Ndio huo utabiri usio vipimo niliomaanisha.

Lakini kwa vile hukunielewa na hukufurahi, samahani Mag3.
 
Ni taasisi/mamlaka gani ambayo imefanya utafiti na kuthibitisha hilo?Au ni suala la kuhisi tu ili upate uhakika kama unachokisema ni sahihi/si sahihi?!
Binafsi,si kweli ila Kiswahili ndiyo kinawazungumzaji wengi kuliko Kisukuma na hili halihitaji mjadala-save as provided herein.
 
Si kweli kwamba Kisukuma ndio lugha yenye waongeaji wazawa wengi nchini. Ingawa hawajaweka assumption za utafiti wao na njia walizotumia kuwaainisha hao wazungumzaji wa lugha mbalimbali, bado matokeo ya utafiti huu hayana ukweli na hayalingani na hali halisi.

Ukichukulia kwamba mtafiti alilenga wazungumzaji wazawa. Haiwezekani kabisa kuwa katika Tanzania watu milioni 2 na ushee wakawa ndio wazungumzaji wazawa wa kiswahili. Maeneo ya mijini tu ya baadhi miji ya Tanzania kwa ujumla (Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Unguja, Pemba, Arusha, Moshi, Dodoma, Iringa, Mbeya, Kigoma, Mwanza), unapata wazungumzaji wazawa wa Kiswahili ambao ukiwajumlisha wanazidi milioni 10, ambayo ni zaidi ya wazungumzaji kiswahili waliotajwa na ripoti kuwa milioni 2.

Hata hivyo idadi ya Wasukuma Tanzania iko kati ya milioni 3 -4. Sasa hii idadi ya milioni 5 ya wazungumzaji Kisukuma inatoka wapi?

Wakuuu,

Kwa maoni yangu ni kwamba huu mjadala hautakuwa na tija kama hatutapata ripoti kamili ya huo utafiti. Naamini kabisa mwandishi hakuwa makini kusikiliza kile kilichosemwa, au kama alisoma ile riport naamini vilevile kwamba hakuelewa kile alichokisoma kuhusu hiyo riport. This is how perception is all about!

Mama,

Jamii ya Wasukuma na Wanyamwezi kwa pamoja wako zaidi ya asilimia 30 ya watanzania wote. So if the total population of tanzanians is 40 million, then 30% of this 40 million is 12 million. So the Sukuma people in their totality, which includes their brothers and sisters Nyamwezi, are more than what you claimed to be their population, i.e 3-4 million, which is completely wrong! Their estimated population is 12 millions!

Anyway, let us wait and see the actual riport from UDSM professors!
 
Asante sana Kuhani kwa rejea hiyo. Hapo hawajaongelea wazawa kama ambavyo wewe unaaza. Hivyo let it out of the window.

Hata hivyo zaidi ya asilimia 60 ya hao waongea Kiswahili barani Afrika wako Tz. Hivyo, basi ukweli unabaki kuwa zaidi ya Watanzania milioni 5 wanaongea Kiswahili.

Kwa mfano, kwa hesabu za haraka haraka ukichukua watu milioni 2 wanaotoka Unguja, Pemba na Dar es Salaam, wawe ni waongeaji wazawa na Kiswahili. Ukiongeza Tanga, Morogoro, Lindi, Mtwara, Arusha na Mwanza, unapata wazungumzaji Kiswahili wazawa wanaozidi milioni 3 na ushee. Hivyo basi watu wanaoongea Kiswahili Tanzania wanazidi milioni 3.


Okay, okay, hebu tuangalie wazungumzaji wazawa wa Kisukuma ili tuweze kuhusisha na hiyo idadi ya waongea Kiswahili nchini.

Tanzania kuna Wasukuma kati ya milioni 3-4, iweje leo mtafiti au hata kama ni mwandishi atueleze kuwa wanaoongea Kisukuma ni milioni 5? Wamepika taarifa, au takwimu zao ni za uongo. Kifupi ni kwamba wameudanganya umma kwa kusema kuwa kuna idadi waongea Kisukuma ni kubwa kuliko idadi halisi ya Wasukuma wenyewe! Au kuna Wasukuma hewa?

Mama,

Sukumas are more than your claimed figure! Please refer my previous post against yours!

Your statistics about Sukuma population is totally and completely wrong! They are estimated to be about 12 millions!
 
Last edited:
wapendwa hao ndo watafiti wetu,maana kwa mtu mwenye akili hamwiingii kabisa hebu angalia tu watanzania tupo wangapi? na hao wasukuma wako wangapi ndani ya watanania hao hao? na ni wangapi wanaongea kiswahili? mi sijui! may be alitoka kwenye mkesha akaamkia ofisini nakusema alikuwa kwenye utafiti,ila inasikitisha na inaonyesha hali halisi ya nchi jinsi tusivyo makini na mambo tunayo yafanya.
 
What? ulimaanisha Mara?

Pamoja na hilo....ukerewe haipo mkoa wa Mara.....ipo Mwanza....kusikilizana lugha sio tija kwamba iko mkoa mmoja....

....mfano Wilaya ya Biharamulo ina wakazi wanaongea lugha za Kisukuma sehemu za Ichwankima,Chato,nyankahanga,Busere sele,kibehe,changugu na Buzilayombo.....kiha sehemu za nyakahura,lusahunga......kisubi sehemu zote za biharamulo mjini na nje kidogo.....

Just kuweka record vizuri,

Maeneo tajwa hapo juu yapo wilaya ya Chato na si Biharamulo.
 
Max na wewe ni chapa ya ng'ombe nini?

Basukuma tunatesa sana JF aisee....that's sak pase!


Nipo ndani ya kumi bora.

Mikoa mitatu lugha moja, sio mchezo mkuu. Tunaweza kuwa nchi.

Watu milioni kumi na mbili ni taifa kamili. Ni kuweka Rais na Mawaziri na kuanza mbele.
 
Kama Tanzania ina population ya millioni 40 ni zaidi ya asilimia 90 (kwa makisio yangu) wanazungumza kiswahili acha mbali kuwa lugha yao ya kwanza.

Which is which, tuamini utafiti au individual makisio? come on man, live up a little!!
 

Nipo ndani ya kumi bora.

Mikoa mitatu lugha moja, sio mchezo mkuu. Tunaweza kuwa nchi.

Watu milioni kumi na mbili ni taifa kamili. Ni kuweka Rais na Mawaziri na kuanza mbele.

....Taraatibu ndugu zangu, naona mnataka kuanzisha movement hapa, tubaki kwenye mada!!
 
Mle ngh'olo hangi mle balele sana

kilipoondolewa kipengele cha kabila kwenye sensa za taifa lengo lilikuwa ni kuepuka hivi vi mawazo kama tupo wengi kuliko wao wachache, sasa tafiti kama hii inarudisha nyuma juhudi hizi za wajenzi wa taifa letu lenye mshikamano umoja na amani. Hebu angalia athari za tafiti hii humu ndani hata mzee wa miafrika ndivyo tulivyo amejisahau na kuanza kujitambulisha kama msukuma. Tunataka uafrika wetu kwani miafrika ndivyo tulivyo kiafrika...lofl
 
Utafiti unasema kuwa lugha ya kisukuma ndio inazungumzwa na watu wengi kuliko kiswahili.

Na Abeid Poyo

MRADI wa Lugha za Tanzania (LoT) umezindua atlasi ya lugha na kuitaja lugha ya Kisukuma kuwa na wazungumzaji wengi nchini.

Katika uzinduzi huo uliofanyika jana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lugha ya Kisukuma ilitangazwa kuwa na wazungumzaji wapatao 5, 195, 504 ikifutiwa kwa mbali na lugha ya Kiswahili yenye wazungumzaji 2,379,294

Akizungumza katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa lugha kutoka ndani na nje ya nchi, Mratibu wa mradi huo, Prof Josephat Rugemalira alisema atlasi hiyo ya aina yake inatoa picha halisi ya idadi ya lugha zilizopo nchini, wazungumzaji, maandiko, usambaaji wake na maelewano ya karibu ya lugha.

“Atlasi ya lugha za Tanzania ni kiungo muhimu katika mkakati wa wa kuzitambua na kuzitathmini rasilimali zetu za utamaduni”, alisema Prof Rugemalira na kuongeza kuwa, uzinduzi wa atlasi hiyo unatoa picha halisi ya maendeleo ya sekta ya lugha nchini.

Kwa mujibu wa Rugemalira, atlasi hiyo ni matokeo ya utafiti wa miaka kadhaa wa mradi huo ulio chini ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alibainisha kuwa utafiti huo pia ulibaini kuwepo kwa lugha 150 hapa nchini huku baadhi yake, kama vile lugha za Wanda, Kiga, Kikuyu na Bwali zikiwa hatarini kufa kwa kukosa matumizi.

Alifahamisha kuwa lugha hizo zimekumbwa na hali hiyo kutukana na mambo mbambali ikiwemo lugha hizo kumezwa na lugha kuu.

Katika hafla hiyo, machapisho 20 zikiwemo kamusi 18 za lugha za asili zilizinduliwa na Balozi wa Sweden nchini Staffan Herrstrom aliyekuwa mgeni. Hafla hiyo ilikwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Lugha Mama duniani.


Source: Gazeti la Mwananchi

Wazo langu:
Utafiti huu bila shaka haukuangalia overlap ya hizi lugha, kama kuna watu wanaozungumza kiswahili na lugha zingine ikiwemo kisukuma chenyewe au ulilenga kwa wale wanaozungumza kiswahili tu bila lugha nyingine, na kisukuma tu bila kiswahili? Ina maana wasukuma wengi hawajui kiswahili?
Wapo bado wasukuma wasiojua kiswahili? Hata kama wapo wanatakiwa wawe wengi kuliko wanaoweza kuzungumza kiswahili ili hiyo hypothesis iwe kweli...
 
Back
Top Bottom