Nimesikitika sana taasisi yenye dhamana ya kusimamia Lugha ya Taifa (Kiswahili) kukosa jenereta pale unapokatika umeme

Irene Magoboka

New Member
Feb 8, 2024
2
1
Jana nilifika katika ofisi za BAKITA (Taasisi ambayo inabeba dhamana ya lugha ya Kiswahili inayotuunganisha sisi kama Watanzania). Nilichokiona kimenisikitisha sana.

Nilihitaji kupatiwa huduma ya Tafsiri cha ajabu niliambiwa hakuna umeme ofisi nzima (kutokana na mgawo ambao unaendelea nchini kutokana na TANESCO na baadhi ya viongozi wa Serikali kutosimama imara kuhakikisha nishati nchini ya umeme inapatikana muda wote).

Hivi inawezekanaje ofisi ya Serikali ikose chanzo mbadala cha nishati ya umeme (Jenereta)? Maana jana nilipoingia nilishangaa kuwaona watumishi wamekaa chini ya miti, nikajiuliza inakuwaje hawa wako nje saa hizi.

Nilipouliza nikaambiwa umeme umekatika ndio nikajua kuwa watu wanaopaswa kutoa huduma wameshindwa kukaa ndani ya majengo hayo kwa sababu ya joto.

Nitoe rai kwa Serikali, ni aibu kubwa sana viongozi wa chama tawala kusimama kwenye majukwaa na kuweza kufikisha ujumbe kwa wananchi (wapiga kura) na kuongea Kiswahili ambacho husikika vizuri katika ngoma za masikio ya wapiga kura wao halafu taasisi inayokisimamia hicho Kiswahili inashindwa kununua hata jenereta.

Hata majengo ya ofisi hiyo nilipodadisi nilielezwa kuwa zilikuwa nyumba za wafanyakazi wa Shirika moja la bima nchini.

Kelele za viongozi kuhusu Kiswahili ni nyingi lakini uhalisia haupo kabisa. Mimi nilipata bahati ya kuishi katika nchi za Ulaya taasisi zinazosimamia lugha zinaheshimika sana. Kwa mazingira niliyoyaona ninapata wasiwasi juu ya weledi wa watumishi wa taasisi hiyo.

Naomba kuwasilisha.
 
Sio kwamba unasikitika kwanini kuna Mgao in the First Place ?

Ukiambiwa Hakuna Kamusi za Kutosha au Wadau wa ku-update Kamusi sababu ya kukosa fedha kwa ajili ya kununua jenereta (au kwanini mpaka sasa neno la kiswahili la jenerata sio neno linalotumika zaidi) nadhani unaweza kusema ni ufujaji wa pesa...

Tupende kupeleka lawama panapohusika....
 
bora umeme....mimi nilienda kufanyiwa translation ya vyeti. yaani wino umefaint, maandishi hayaonekani kabisa....niliumia roho na wakati nimetoa 30 elfu kwa kila cheti. inaumiza kiukweli.....huduma mbovu mbovu.
 
Jana nilifika katika ofisi za BAKITA (Taasisi ambayo inabeba dhamana ya lugha ya Kiswahili inayotuunganisha sisi kama Watanzania). Nilichokiona kimenisikitisha sana.

Nilihitaji kupatiwa huduma ya Tafsiri cha ajabu niliambiwa hakuna umeme ofisi nzima (kutokana na mgawo ambao unaendelea nchini kutokana na TANESCO na baadhi ya viongozi wa Serikali kutosimama imara kuhakikisha nishati nchini ya umeme inapatikana muda wote).

Hivi inawezekanaje ofisi ya Serikali ikose chanzo mbadala cha nishati ya umeme (Jenereta)? Maana jana nilipoingia nilishangaa kuwaona watumishi wamekaa chini ya miti, nikajiuliza inakuwaje hawa wako nje saa hizi.

Nilipouliza nikaambiwa umeme umekatika ndio nikajua kuwa watu wanaopaswa kutoa huduma wameshindwa kukaa ndani ya majengo hayo kwa sababu ya joto.

Nitoe rai kwa Serikali, ni aibu kubwa sana viongozi wa chama tawala kusimama kwenye majukwaa na kuweza kufikisha ujumbe kwa wananchi (wapiga kura) na kuongea Kiswahili ambacho husikika vizuri katika ngoma za masikio ya wapiga kura wao halafu taasisi inayokisimamia hicho Kiswahili inashindwa kununua hata jenereta.

Hata majengo ya ofisi hiyo nilipodadisi nilielezwa kuwa zilikuwa nyumba za wafanyakazi wa Shirika moja la bima nchini.

Kelele za viongozi kuhusu Kiswahili ni nyingi lakini uhalisia haupo kabisa. Mimi nilipata bahati ya kuishi katika nchi za Ulaya taasisi zinazosimamia lugha zinaheshimika sana. Kwa mazingira niliyoyaona ninapata wasiwasi juu ya weledi wa watumishi wa taasisi hiyo.

Naomba

bakita ni baraza la kiswahili tu na sio taasisi

Back
Top Bottom