nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,858
- 2,348
Japokuwa watu wa sensa huuliza lugha za watu, inaonekana ni moja ya takwimu ambazo huwa hawajisumbui kuzitaja.
Pengine huonekana si muhimu, ama pengine watu huwa hawaiulizii hiyo takwimu.
Ila, binafsi, naamini kingereza hadi sasa kipo kwenye tano bora ya lugha zinazoongelewa zaidi nchini, ama, basi tuseme walau zinazoeleweka zaidi na watanzania
Hadi sasa wazungumzaji wa kingereza kwa ujumla wao wanazidi idadi ya wazungumzaji wa lugha nyingi za makabila.
Siamini wazungumzaji wa Kiingereza wamepitwa kiidadi na wazungumzaji wa lugha kama Kizaramo, kihehe, Kimasai, au kichaga na kadhalika, zingatia sio wazungumzaji wa hizo lugha kwa ujumla wao, bali kama lugha moja moja na wazungumzaji wake kivyake, kisha linganisha na kingereza na wazungumzaji wake kama lugha moja pia
Hivi kwa mijini tunamoishi, unadhani wangapi kiidadi baada ya Kiswahili wanaweza kuzungumza lugha zao zile za asili kwa uzuri kabisa, haya, je, wangapi kiidadi baada ya Kiswahili wanaweza kuelewa ama kuzungumza kingereza? Unadhani wepi ni wengi, je, ni watanzania wawezao lugha zao za asili ama wale ambao kingereza ndio lugha yao ya pili?
Haya ni maoni yangu, wewe unaonaje?