Eric Shigongo auita mtandao wa JamiiForums wa "KIJINGA KIJINGA"...

Status
Not open for further replies.
Nimemsikiliza Eric Shigongo kupitia Channel 5.

Ukweli upeo wake ni finyu sana maana kauli alizotoa ni tata, mtu mzima hawezi kuongea hivyo. Anasema Wakenya na Waganda wanatudharau sana Watanzania. Pia anasema watanzania wengi ni wajinga ndio maana wanamponda kupitia JF.

Hoja aliyokuwa anaongelea na kuwahusisha waTZ wote ni mtafaruku wake binafsi na Jose Chameleone. Ukweli kaongea pumba tupu, hakuna punje hata moja. Anajenga chuki baina ya mataifa mawili. Nimejua ni kwa nini yeye ni mkurugenzi wa udaku na up upu Tz.
Afrika Mashariki tunapendana, yeye atabaki na chuki zake binafsi !

Shigongo ametajirika kupitia blackmailing business, tunajua sana wala hana cha kujisifu.
 
nasikia alikuwa anacopy na kupaste....

Hahahaha, duh sikujua basi enzi izo nafuatilia ile mbaya kumbe alikuwa anatranslate tu! Duh wabongo, nimeona hata sms watu wanaforward tu hawana muda wakuandika! This is Tanzania.
 
Whats goin on between mr. Erick shigongo and dr. Josee camelion?..details please
 
Jamaa ana hasira kalizwa pesa yake na watoto wa uganda.
Gazeti lake la udaku nnaweza kuliandika lote kwa dakika 10 kwa kutumia google.
 
Whats goin on between mr. Erick shigongo and dr. Josee camelion?..details please

jamaa ameingizwa mkenge na kichaa camellion wa dollar 3500, alimpa cash manager wa cammellion ili jae afanye show bongo then jamaa achomoa kuja kwamba ajapokea pesa...
 
huyu Shigongo ni Problematically kweli halafu alivyo mnafiki anajifanya mlokole kumbe moja ya matapeli tu hapa mjini, na asije akajiona yeye ana akili nyingi kuliko wote na asitake kujifanya yeye ni mwerevu sana kumbe mnafiki tu, na kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake humu JF ili mradi havunji sheria, pumba zinazoandikwa kwenye mtandao wake zina tija gani katika maendeleo ya jamii ya kitanzania? zaidi ya kuwafirisi watu mawazo na kuwafanya wawe na dhiki ya akili..... Shigongo acha unafiki ndugu hata wakina mama rwakatare walileta chokochoko wamepoa sasa hivi na bora uendelee na mambo yako la sivyo watu watamwaga maovu yako hapa
 
Eti anaipenda Tanzania hadi kampa jila Tanzania mtoto wake wa kike...jamaa ana pumba mbaya.

Nani alimdanganya kumpa mtoto jina kama hilo ndo kupenda? Nijuavyo mimi angekuwa akiipenda angeitete hasa kwa kutumia magazeti yake kuvumbua uovu wa serikali na viongozi wake ambao ndo unaiweka serikali kwenye hali mbaya kama hivi ilivyo sasa, na siyo eti kujiunga na magamba na kuwasapoti ktk maovu yao pia nilichomgundua jamaa anatengeneza mazingira ya kuja kugombea ubunge. Alafu si miongoni mwa wale waliotapeli waTz ktk lile tamasha la tarehe 7.7 kwakuwaadaa kuna pambano la cheka na kaseba? Iweje leo aseme anaipenda Tz na siyo raia wake
 
Shigongo ni nani vile, maana nakumbuka kulisikia jina hili miaka kadhaa iliyopita
 
huyu Shigongo ni Problematically kweli halafu alivyo mnafiki anajifanya mlokole kumbe moja ya matapeli tu hapa mjini, na asije akajiona yeye ana akili nyingi kuliko wote na asitake kujifanya yeye ni mwerevu sana kumbe mnafiki tu, na kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake humu JF ili mradi havunji sheria, pumba zinazoandikwa kwenye mtandao wake zina tija gani katika maendeleo ya jamii ya kitanzania? zaidi ya kuwafirisi watu mawazo na kuwafanya wawe na dhiki ya akili..... Shigongo acha unafiki ndugu hata wakina mama rwakatare walileta chokochoko wamepoa sasa hivi na bora uendelee na mambo yako la sivyo watu watamwaga maovu yako hapa
anatatutafutia ban tuachaneni naye.
 
Kaka huyu ni mwehu,kwanza anadai eti Members wa JF eti wana account nyingi nyingi,unajua nini? Ni rahisi tu.Huyu ni Expert wa UDAKU, sasa hapa JF watu wanaongea ukweli,wanafichua uozo,wanaanika Ukweli,sijui kati yake na Chamillion yupi yupo sahihi lakini kuita mtandao huu wa kijinga jinga hapo ameingiza udaku kwenye mambo ya Msingi.Shigongo kiwa makini na Matamshi yako.kuna hawa unaowaita wajinga na wanunuaji wa Magazeti yako,au na wewe huhitaji wao wanunue mahazeti yako kama alivyoongea mkubwa wa Kaya kwa Waalimu?

Sijui mtu akishakuwa ccm kwanini anakuwa na akili mbovu namna hii, hivi ni kitu gani kinampa kiburi namna hiyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom