Hawa ni Nguli wa masimulizi hapa JF Jukwa la Entertainment. Je, unadhani nani ni mkali?

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Leo nimeona niwatambue hawa jamaa wanaoendelea kutuburudisha na kutupunguzia misongo kule kwenye jukwaa la Entertainment kwa simulizi zao za moto kweli kweli.Hawa nitakaowaorodhesha hapa kwa upande wangu ndiyo wababe wa lile Jukwaa.

Hawa nitakao wataja hapa nimewaita wababe kwasababu wanazo simulizi kuanzia mbili na kuendelea na zote zikiwa za moto


1. SteveMollel
Huyu jamaa anazo simulizi kadhaa ambazo zimeendelea kukonga nyoyo za wasomaji,miongoni mwa simulizi hizo ni hapa

Tukibaki Hai, Tutasimulia

Anga la washenzi na Joana anaona kitu usiku

Nyuma yako

Roho yake inadai

Baradhuli mwenye mikono ya chuma

Niliweka shada za maua kwenye makaburi matano ya watu wangu wa karibu


2. Jack Daniel
Huyu jamaa nae anazo simulizi kadhaa ambazo zimefanya na zinaendelea kufanya vizuri huko kwenye Jukwa la Entertainment,zake ni hizi hapa

Milango ya mafanikio

Mimi na Boss Wangu

Nilinusurika kuchomwa moto

Pombe na ilivyosababisha nikaikosa nyumba


3. leadermoe
Huyu jamaa yeye pia amejitahidi kukonga nyoyo za hadhira yake kwa simulizi zake za kweli kali na zilizoenda shule.Baadhi ya simulizi zake ni hizi hapa

Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Nilivyookoa maisha ya Watalii toka Finland

4. Analyse
Huyu jamaa yeye pia amekuwa na simulizi kadhaa ambazo zimeendelea kujizolea umaarufu huko kwenye jukwaa la Entertainment,amekuwa akikonga nyoyo za wadau na kuzisuuza roho za wadau wenye misongo.Simulizi zake ni hizi.

Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...

Fumanizi la mama mwenye nyumba

Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee

5. JBourne59
Huyu jamaa simulizi zake zitakufanya ukae chini ushike tama kisha unyanyuke ushike kiuno,hii yote ni utamu tu wa simulizi zake ambazo hazichoshi kusoma.Baadhi ya simulizi zake ni hizi

Uhusiano wangu kimapenzi na "Hamida"

Hatimaye nipo huru

Hekaheka Uzeeni

6. UMUGHAKA
Huyu jamaa apewe maua yake,nimejaribu kupitia simulizi za huyu jamaa kiukweli anajua hadi anajua tena,yeye husema ni Bodaboda ila siamini kama kweli ndiyo kazi anayoifanya.Kitu nilichokipenda kutoka kwa huyu jamaa ni kwamba simulizi zake ni halisi na zinahusu maisha yake.Baadhi ya simulizi zake ni hizi hapa

Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

7. Jose Author
Huyu jamaa yeye kwasasa pale kwenye jukwaa la Entertainment naweza sema ndiye mwenye mji wake,ameendelea kujizolea kijiji chake na anaendelea kukimbia nacho,hakika jamaa anajua hadi kapitiliza,baadhi ya simulizi zake ni hizi

Wakati najiuza niliwafanyisha watu mapenzi na fisi bila ya wao kujua

Duduke

Mwenzi wa Maisha yangu

NImeolewa na nani?

NILIOA MKE WA PILI KUMBE JINI

ZAMDA

8. FEBIANI BABUYA
Huyu jamaa pia amekuwa mmoja wa wasimuliaji bora kabisa katika jukwaa la simulizi,ukiwa na msongo bila shaka kwa huyu jamaa utapata tiba ya kiakili ingawaje simulizi zake nyingi nizakubuni,baadhi ya simulizi zake ni hizi hapa

I want to die a judge

Ulimwengu wa Watu Wabaya

Gereza la Hazwa

Innocent Killer

Naweza sema hawa ndiyo majemedari huko kwenye Jukwaa la Entertainment,hawa jamaa simulizi zao ni kuanzia mbili na kuendelea na pia ni za moto,sijawajumuisha waandishi wengine kwasababu wengi unakuta anako kastori kamoja ambako kamevuma kama upepo kisha akala kona.

Sasa kwa mtazamo wako mwana JF uliyebahatika kusoma mikito ya hawa jamaa unadhani nani anastahili kuwa THE ENTERTAINMENT THREAD KING?

Shusha comment yako hapo chini ikiwezekana mtag kabisa KING ili afahamu yeye ni KING

ANGALIZO : Upangaji huu ni holela si kwamba aliyeko namba moja ni bora kuliko wa mwisho,ubora wa simulizi za wahusika ndiyo iwe chanzo cha kuitwa KING
 
Kuna mwamba aliletaga simulizi mwaka juzi hapa ni hatari, utafikiri unaangalia a walking dead.
Alisimulia kwenye harakati walikuwa wanazipita maiti kibao zimekufa kwenye harakati huko.
Jina la uzi na mwandishi nimemsahau.
 
Steve ni mkongwe kidogo na stori zake za kimataifa zaidi.
Ofcoz wengine pia wako njema sababu kutunga story na kupata watu wanakwambia Wana arosto basi uko vizuri sana unahitaji kupewa heko zako
Mkuu mtag KING wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom