Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Mtu mzima kuonekana unayumba kiimani na msimamo ni changamoto ambayo inaweza kuzorotesha heshima yako kwa jamii.
Mh. Lowasa, Edward N. alikuwa mwachama wa CCM tangu enzi zake za uchipukizi mpaka kufikia kupata nafasi mbalimbali za kiutawala kama uwaziri na hata kuwa Waziri mkuu wa JMT. Mimi na wengine wetu wengi nahisi tuliungana katika ndoto mkakati za kimaisha za kutaka kuwa kama Lowasa siku moja maishani,
Kumuona Lowasa akienda upinzania kulinifanya nitafakari ziko wapi zile nasaha za hekima za wazee ambazo tumekuwa tukifunzwa? Niliweza hata kujiuliza ikiwa mheshimiwa huyu atafanya hivi vipi kuhusu vijana wanaochipukia si ndio chanzo cha kuwa na kizazi malaya cha siasa?
Kuamua kwake kurudi nyumbani kwake (CCM) kumenifanya niuone ukomavu wa hekima, utashi na hata busara za mzee huyu. Ni vigumu kwa yeye kusema anarudi kuunga mkono juhudi za Mh. Raisi bali cha msingi ni kwamba anarudi nyumbani kuendelea kukijenga chama cha mapinduzi hasa kwa kuwajenga vijana wa leo wafanane nao wa kizazi cha 'CCM imara' ambacho kilikuwa nyota kwa wote walikuwa ndani na nje ya CCM.
Kutokana na nafasi zake alizoshika kiserikali ameonelea umuhimu wa kushikamana na wale aliowaachia nafasi ili waweze kutimiza malengo yaliyowekwa kijamii kwani uongozi sio mwanzo wa kila kitu.
Nimpongeze pia Mh. Lowasa kwa kuweza kuwaonyesha kuwa binadamu huweza kubabaika kunakotokana na kutokuridhika ama kutotosheka ambako kunawez kumfanya binadamu huyo kuweza hata kukengeuka na kupoteza mwelekeo japo pia anakuwa na nafasi ya kujisahihisha endapo hatochelewa.
Hongera sana Mheshimiwa Edward N. Lowasa
Hongera sana Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.
Hongera sana Tanzania
 

Attachments

  • 1200px-Flag_of_Tanzania.svg.png
    1200px-Flag_of_Tanzania.svg.png
    5.1 KB · Views: 20
  • 52893188_2045096802192764_2698043531305418752_n.jpg
    52893188_2045096802192764_2698043531305418752_n.jpg
    43 KB · Views: 21
Political calculations, he was no longer an asset but a liability. Upepo hauko upande wake tena, kwa nini aendelee kutesekea huku? Bora arudi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Lowassa had already become a spent force in the opposition ranks. Aidha hata yeye alikuwa anajisikia out of place. Isitoshe, kitendo cha Lissu kutangaza kuwa atagombea ni ujumbe kwake kwamba mchezo umebadilika. Only hope ameweza kupata deal kuhusu mashabiki wake waliokuwa victimised na kubambikiwa usaliti bandia. But being a very selfish politician he may have dumped them.
 
Amefanya jambo la heri nakumbuka sana usemi wa mange kimambi ya kwamba

Lowassa ni zigo la mavi chadema toweni huu mzigo"si maneno yangu hayo ni kimambi on air

Lakini mbowe alikuwa mbishi kweli mpaka kimambi akawa anamtumia direct sms mpaka nakutaka kumtukana lakini mbowe alibeba tu huo mzigo aisee zile million 400 alizotia mfukoni ziko wapi leo mbowe mbowe eeeeeh haya ngoja tuone

Kingine nimemkubali sana lowassa maana amecheza ka messi vile yani wakati wa msiba wa boss ruge unatrend yeye ndiyo kang'atuka hahaha dah najikuta najicheka mwenyewe

Kingine alichokosea ni kwamba kawahi sana angesepa mwakani mwezi kama huu alafu tuone upinzani utakuwa na hali gani!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikua mzigo tuu siasa za ukombozi hawezi huyu babu.
Hata mchango kwa chama hana.
Tunashukuru kutupa wabunge madiwani wengi 2015 na jina chadema.sasa ni maarufu kuliko chama cha mafisadi ccm.
Ile mahakama ya mafisadi itapata kesi kweli maana iliundiwa ambao leo ndiyo waliokua mstari na mkiti katibu PM
Alluta Continua


Haaaah....watanzania sjui uwa tunakata nn....leo kachoka mkuu kweli au ndo ushapewa posho ya kuamsha amsha humu kwa jukwaaa?
 
EL ndiye mshindi! CCM na CDM wote ni aibu tu....kwa walio timamu. Hakuna mwenye afadhali. Tena anasema "amerudi nyumbani"....na CCM top brass yote inampigia makofi! Aibu sana. Kama ilivyokuwa kwa CDM mwaka 2015. Ngoja tuone sasa "sifa" atakazo mwagiwa na CCM na "kashfa" atakazomwagiwa na CDM!

Ukweli wa ule usemi unaotuasa kuweka akiba ya maneno unadhihirika vizuri sana katika hizo sarakasi za Mh EL.

Ila binafsi naona ile kesi dhidi ya mkwe wake ina msukumo mkubwa sana katika haya yanayoendelea. Ngoja tuone jinsi mfumo wetu wa mahakama "unavyochezewa".
 
Nasubiri kusikia matamko ya:-

1. Lema
2. Lissu na
3. Msigwa

Hoja inaweza kujengwa kwamba, "-------- wakati alipokaribishwa, na sababu za kukaribishwa kwake kwa wakati huo," uamzi huo ulikuwa 'smart', hata kama haukufanikiwa. Sababu kuu lilikuwa ni lengo la ushindi. Chama chochote cha upinzani lengo lao kuu la kwanza ni ushindi, na wakishashinda, mengine hufuata.

Hawakushinda, na maskini wa watu Mzee huyu anajua wazi kwamba hana lake tena ndani ya chama hicho. Ya nini kuendelea kukaa humo kama hana tegemeo tena la kupewa nafasi ya kupeperusha bendera?
 
Japo nikiri nimeshindwa kumwelewa aliposema haya alimaanisha nini........

#NUKUU "Hatuwezi kugombana na kuchukiana kwasababu ya Kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa hivyo, sisi ni Watanzania Kwanza.Lakini binafsi bado naamini Mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM", - Edward Lowassa
#NipasheMwangaWaJamii
 
Makamanda au nyumbu kwa jina lingine,huwa hawawazi nje ya box hata utikise kama vichwa vyao.
Nyumbu ni wew ambae hujitambui tuambie lowassa kwa sasa ni asset au liability usipojibu wew ni nyumbu tena wa hashi.
 
Pongezi kwa watanzania weledi ...!
Slogan ya Magufuli ilikuwa ni hapakazi tu na Slogan ya lowassa ilikuwa mabadiliko.

Leo hii ni muungano mtakatifu kwa ajili ya maendeleo.

Wafuasi wa Team zote mbili tutaombana radhi na sasa tujikite katika kuijenga Tanzania ya Kazi na yenye kubadilika.

Karibu tena Mheshimiwa lowassa.
Leo ni siku ya kucheka tu... hahaaa Magufuli aungana na fisadi kuu sijui kama Tanzanite zetu zitapona.
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.
Fisadi mpya kampokea fisadi wa zamani😂😁
 
Back
Top Bottom