Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Kwa kweli, watu wameshasahau ya Ruge kabla hajazikwa.
Lowassa ana roho mbaya sana na kafanya makusudi ili kupunguza majadiliano mitaani, angetangaza hii siku ambayo hamna tukio lingine ishu ingejadiliwa hadi kwenye masomo ya hisabati shule ya msingi.
Kwa umaarufu Lowasa anamzidi Ruge kwa mbali sana
Huku kijijini watu hata hawajui Ruge ndo nani
 
Ujio wa Lowasa CCM kwa sasa una faida gani katika uimara wa chama hicho? Je, ni upi mtizamo wa viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama hicho?

Je, kwa chadema Leo hii kuondokewa na Lowasa ni faida au hasara? Alikuwa na ushaeishi?

Kwa Mahakama na serikali, ujio wa Lowasa CCM hauwezi kuwa na viashiria vya rushwa hasa pale yatakapotolewa maelekezo ya kuhitimishwa kwa kesi ambazo zinawahusu ndugu na jamaa zake?

Kama ujio wake CCM utapelekea baadhi ya watu kutoka magereza, je haitaleta picha kuwa tumewaweka watu kwa sababu za kisiasa na hivyo kumfanya jaji mkuu na muhimili wake kuonekana unatumika kuwakandamiza wananchi wenye mrengo tofauti na serikali au chama tawala?
Daaaa kwa bandiko hili wale jama hawatatoka tena maana kilankitu kiko hadharni Halfu hivi Rostam na yeye vipi
 
Mstaafu, anahitaji kupumzika na family yake.
Family first, mengineo yatafuata.

Siasa za kipindi hiki hazina urafiki wa kudumu.
 
wanaojua huo wimbo na waliopewa maiki ndio wataanza kuimba, sie wengine tunafuatisha tu.
 
Asalaam aleikum waungwana, kwa wale wenye kumbukumbu ya maneno ya JPM kuwa kila atakae rudi CCM lazima akatwe mkia ili kuwa tofauti na kundi.
Je Edo ana mkia nusu?
Naombeni majibu kwa wenye majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili swali hata mimi linanipa wakati mgumu sana.

Wanasiasa wote wanafik, wapo kwa maslahi yao binafsi na si maslahi ya wananchi kama tunavyojitahidi kuamini.

Watanzania, tusiuane na kujiumiza kwa kushawishiwa na viongozi wa siasa au eti kwa mapenzi ya chama. Hili ni fundisho kubwa sana.
Siasa mbaya Sana!
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.
Marekebisho kidogo, wimbo haukuanza kwa Chadema. Chadema waliitikia tu...wimbo ulianza kwa Kamati ya Mwakyembe ili kumlinda fisadi mkuu wa Richmond Jakaya Kikwete.
 
Back
Top Bottom