Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Wameniudhi sana. Maana hii ya Lowasa ndo ingekuwa big newz. Sasa watu wapo na kumpokea marehemu Ruge.
Hata hivyo ushawishi wake kisiasa kwa kiasi fulani ulishakwisha lililobaki ni jina tu...

Kubaki CDM na kurudi CCM kwake hakuna anachopoteza...
 
Pongezi kwa watanzania weledi ...!
Slogan ya Magufuli ilikuwa ni hapakazi tu na Slogan ya lowassa ilikuwa mabadiliko.

Leo hii ni muungano mtakatifu kwa ajili ya maendeleo.

Wafuasi wa Team zote mbili tutaombana radhi na sasa tujikite katika kuijenga Tanzania ya Kazi na yenye kubadilika.

Karibu tena Mheshimiwa lowassa.
leo sio oil chafu!?
 
Yeye na Sumaye wote Maboya tu na maji siku zote hufuata mkondo, hivyo fisadi moja limerudi nyumbani kwa mafisadi wenzie.
Fisadi lililogombea urais Chadema hadi Chadema ikafuta list of shame! Brother tuliza akili kidogo otherwise uwe unapata ugali Chadema! Kuna tatizo hapo na inabidi kulitatua kupitia ukweli tu! Tusipingane tu bila dira!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowassa ndio kajimezesha kwa Ruge ili watu wasijadili kurejea kwake CCM.

Kwa matukio ya kesho pale Karimjee Lowassa ndio atasahaulika kabisa na atakia kwenye midomo ya makamanda wa Ufipa tu!
Huko msibani story itakuwa Lowasa tu
Tofauti na ambapo angefanya bila kuwa na tukio la kukutanisha watu
 
Yanazungumzwa mengi kuhusu kuhama kwa Lowassa na kurudi CCM. Mimi nimelitazama katika angle tofauti.
Hii Sasa sii Vita ya CCM na upinzani, la hasha! Mzee mzima kaelemewa huko ndani ya Nyumba Yake. Hali sii Hali, hususani kuwepo kwa harufu ya wenye Chama halisi dhidi ya huyu Mzee. Zipo taarifa za watu kujipanga ndani ya Chama ili kufanya yao 2020. Ni kwa muktadha huu Magufuli ameamua kuwarudisha katika timu the Kings makers EL na RA. Hii Ni kujiandaa na mashambulizi kutoka kwa Mzee Membe ambae ukimya wake katika mikakati kumewavuruga Gweregwere. Kwa Hali ilivyo, Magufuli Yuko tayari kuunga nguvu na yoyote Yule ilimradi pawepo na uwezekano wa yeye kushinda ndani ya Chama 2020.
Team Mangula (Mzee wa mafaili) na Wote mliojitoa ufahamu 2015, mliemchukia KARUDI. MEMBE KAA STANDBY. USIMSAHAU DOGO LAKO NAPE. KARMA lazima iwatembelee 2020!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona mnaota ndoto za mchana? Ni nani CCM mwenye ubavu wa kusema au kufanya lolote kwa Mwenyekiti na Rais wa nchi! Lowassa na kujiandaa kote, na fedha zote na kila aina ya mikakati aliyotumia mwaka 2015 na akawekwa pembeni ije kuwa rais na mwenyekiti?
 
Marekebisho kidogo, wimbo haukuanza kwa Chadema. Chadema waliitikia tu...wimbo ulianza kwa Kamati ya Mwakyembe ili kumlinda fisadi mkuu wa Richmond Jakaya Kikwete.
Magoli yetu yana zege hayabadiliki.
 
IMG_20190228_213106.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.
Siasa ni ngumu kuliko physics

Lowassa aliyeitwa fisadi na CDM baadaye na CCM hatimaye anakuwa msafi. Hakuna atakayemwita tena fisadi.

Kaipigana vita ya ufisadi na ameishinda!
 
Back
Top Bottom