Duu,wanawake wa mjini noooomaaaaaa!!!

Sitakutumia tena hela ukiniambia una shida,kumbe ndo ka mchezo kakoeeeeh!!

Ayii wewe, unapohitaji rescue ni lazima utegemee zaidi ya mtu mmoja maana waweza kuwa kwenye Mazingira ambayo ni ngumu kunirescue.

Sasa nikimuomba kaka yangu KIKUNGU kuna ubaya gani, wakati unajua ni kaka yangu!
 
Last edited by a moderator:
Kusimanga ndo asili ya mwanamke, huwa tunajizuia tu kutamka mpaka tuwe tumewachoka kabisa. Yaani hata wewe ukiwa umerudi usiku wa manane, asubuhi mkeo akikuangalia anakumbuka jinsi alipokupenda ukiwa na mashati mawili na pea moja ya kiatu (tena cha plastic). Saa hizi unavaa designer leather boots unajiona mjaanja! Heeh, nshaanza kusimanga!

Point is, kuhonga hata sie tunahonga! Mbona wanaume wanaochukua vyao wakiachana nao wapo?

BAK, njoo best uniwekee ile 'kanunua simu kampa demu walipoachana, kampokonyaaa!'. Natanguliza shukrani.

Wanaume ni wachache wanaopokonya vitu wanawake ila ukikuta mwanamke wameachana na jamaa yake ambae alikuwa anampa support analalamika mpaka anafikia kiwango cha hata kuchanganyikiwa na kukusema kwa watu mpaka utakoma kula vya wanawake lakini mbona kina kaka huwa wanatoa tu wakipigwa chini inwauma lakini maisha yanasonga mbele na akimpata mwingine bado atatoa, tatizo kinadada wengi sio utamaduni wao kumpa mwanaume na hata akimpa wakati mwingine inakuwa kama anamhonga kumshawishi
 
hapo umeona watatu tu waliokuja physically,je waliotuma hela kwa Mpesa au tigopesa ni wangapi?
 
mhh kijana samahani wewe ulisema ulikuwa kwenye foleni.uliwaonaje hao waliokuwa wanakuja na kuondoka?wao walikuwa wanaondoka na barabara ipi wakati kulikuwa na foleni kali mpaka ukapata muda wa kuyaona yote haya?au uliamua kupaki kabisa pembeni ili ushuhudie mpaka mwisho?sijakuelewa mkuu...
 
Mi nashindwa kuzielewa akili za wanawake,badala ya kuzungumzia ujinga wa huyo mwanamke mwenzao wa kushindwa kuwa mwaminifu wao wanaletj excuse. . . . . . . .. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Hapa mtoa mada hajazungumzia kiasi cha bei ya mafuta wala hela alizolipiwa mafuta.Pia hajazungumzia kuhongwa,yeye amezungumzia namna huyo mwanamke alivyo wa hovyo kwa kuwapanga wanaume!

Mtoa mada alikuwa akiangalia kinachotendeka na hivyo hajui kabisa uhusiano uliopo kati ya huyo mwanamke na hao wanaume...hivyo si vema kuconclude kuwa "amewapanga wanaume" na kwamba si mwaminifu. Mtu akipata shida mara nyingi humtafuta mtu atakaye respond kwa haraka... Yamkini mmoja ni kaka yake, mwingine mpenzi au rafiki
 
Leo wakati natoka kwenye mihangaiko yangu,kama kawaida barabara za mjini zinauhusiano mzuri sana na foleni,wakati tupo kwenye foleni kuna gari kama latatu mbele yetu lilikuwa limezimika katikati ya barabara,aliyekuwa anaendesha gari hiyo ni binti mmoja mrembo,bila kuomba msaada alibaki ndani ya gari na kuanza kupiga simu,hata hivyo kulikuwa hamna usumbufu kwetu kwasababu hata hiyo foleni ilikuwa haisogei,mara wakatokea vijana wawili wakaja kuisukuma ile gari ili kuiweka pembezoni mwa barabara,yule dada hakutoa shukrani wala kuongea nao chochote,zaidi ya kuendelea kupiga simu tuu,wale vijana walipoondoka yule dada akashuka akiwa ametilia kimini cha hatari na kufungua boneti kisha kufunga bila kufanya chochote,akaingia tena ndani ya gari na kuendelea kupiga simu.Mara ikatokea AUDI nyeusi akashuka mwanaume mmoja mtanashati mkononi anagalon la mafuta la lita tano wakaweka yale mafuta kisha yule dada akaiwasha ile gari kama anataka kuondoka na yule jamaa ambaye alionekana kama ni mume au mpenzi wake akaondoka,lakini cha kushangaza nikwamba yule mwanamke alilizima gari nakuendeleaa kukaa pale pale,haukupita muda mrefu ikaja prado akashuka mwanaume mwingine huku akiwa amebeba galon kama yule wa mara ya kwanza,yule mwanamke akafanya vilevile,jamaa akaondoka mwanamke akazima gari na kuendelea kubaki hapo hapo,kitu ambacho kilinishangaza ni kwamba lilikuja Mercedes benzi na mbaba mmoja naye akashuka na galon ya mafuta akamuongezea kisha akampa yule mwanamke kitu mkononi bila shaka ni hela kisha jamaa akaondoka,na yule dada naye akaingia ndani ya gari na kuondoka,hii ni kitu iliyotokea jioni ya leo maeneo ya kinondoni karibu na Hugo Bar!!Sasa huyu mwanamke inaelekea muda wote aliokuwa anaongea na simu alikuwa anamdanganya mmoja mmoja kuwa ameishiwa mafuta mpaka mwisho ametoka na lita kumi na tano,duu wanawake wa mjini hawafai,na unaweza kukuta hapo alikuwa na appointment na mwanaume mwingine!!!!

Eeee, wajinga ndio waliwao. Ukitaka kula lazima ukubali kuliwa.
 
TUKO WANGAPI? bora mimi kwetu ntuzu ni mkokoteni wa ngo'mbe tu hauishiwi kiwese.
 
Huenda kweli au yote kweli maana unapokuwa observer unaweza sema huyo malaya kumbe unapopata tatizo unaweza kupiga simu kwa watu wanne tofauti wakusaidie na wote waka-respond ukute alivyokuja wa kwanza akamweleza ukweli kuna jamaa mwingine amekuja.


Well said Jodoki...katika observertion nirahisi sana kuwa bias kwa kutafsiri jambo kutokana na mtazamo au imani yako juu ya hilo jambo na hivyo kupoteza ukweli halisi wa jambo lenyewe.
 
Hii ni hadithi ya kutungwa japo ina ukweli ndani yake.
Hmna uongo hata kidogo hakijatungwa kitu,kama unataka kuamini nenda kaulizie madreva taxi pale kinondoni makaburini tena wao ndio walimsaidia kusukuma hiyo gari!!!
 
hizi cctv za mitani bwanaa zina conclude vibayaa
wa kwanza ni chumba wake
wa pili kaka yake
wa tatu baba yake ndo mana akampa na pesa:loco:
 
Duh, hii topic yako imenikumbuka maneno ya King'asti ya jana "Kwani ukifolenishwa una wasiwasi gani wakati wewe ndo unakuwa mwanzo wa mstari? Mtaipata mwaka huu wallah!"

Kaazi kweli kweli......
 
Dah kweli msjini shule, wala huhitaji kutumia nguvu nyingi, ni akili kidogo tu! Na mang'ombe mjini hawaishi hata kidogo, wengine wanakuja kesho, wengine mwezi ujao hadi miaka yote ijayo. Kwahiyo ng'ombe wako siku zote jamani.
 
Kusimanga ndo asili ya mwanamke, huwa tunajizuia tu kutamka mpaka tuwe tumewachoka kabisa. Yaani hata wewe ukiwa umerudi usiku wa manane, asubuhi mkeo akikuangalia anakumbuka jinsi alipokupenda ukiwa na mashati mawili na pea moja ya kiatu (tena cha plastic). Saa hizi unavaa designer leather boots unajiona mjaanja! Heeh, nshaanza kusimanga!

Point is, kuhonga hata sie tunahonga! Mbona wanaume wanaochukua vyao wakiachana nao wapo?

BAK, njoo best uniwekee ile 'kanunua simu kampa demu walipoachana, kampokonyaaa!'. Natanguliza shukrani.

Best king'ast naomba basi title ya wimbo au jina la aliyeimba maana nimetoka kapa kule Utube...Mie niko poa kabisa namshukuru Mungu.

 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada alikuwa akiangalia kinachotendeka na hivyo hajui kabisa uhusiano uliopo kati ya huyo mwanamke na hao wanaume...hivyo si vema kuconclude kuwa "amewapanga wanaume" na kwamba si mwaminifu. Mtu akipata shida mara nyingi humtafuta mtu atakaye respond kwa haraka... Yamkini mmoja ni kaka yake, mwingine mpenzi au rafiki

Wakati mwingine mazingira huzungumza,sio mpaka mtu aseme!
 
Story ya kutunga! "..magari hayasogei,.. kuikaja Aud..ikaja prado..ikaja benz.." ungeniambia ulikua nje ya folen unashuhudia angalau kidogo ungeeleweka japo nayo ingetia shaka kwani kwa hali halisi ya folen ya dar, kuwaita watu 3 toka sehemu tofauti wakaja inachukua muda mrefu

swali la msingi ni kuwa yeye alisimama wapi au iyo foleni ilikuwa inamngoja uyo dada apate mafuta ndo isogee au.
 
Back
Top Bottom