Asiyejua maana, haambiwi maana

Toofast

JF-Expert Member
Dec 23, 2015
435
716
Ikitokea umenunua gari used,kwasababu ni ngumu sana kumiliki zero kilometer basi kuwa makini sana Dereva.

Hakikisha mmiliki wa mara ya kwanza wa gari hiyo,hana funguo ya ziada.

Kuna nyakati gari inachoka na inahitaji service,hakikisha hairudi kwenye gereji ile ile ya zamani.

Kuna gari nyingine huwa haziibiwi bali,hurudi zenyewe kwa mmiliki wake wa zamani.

Pia si unaelewa gari yako mpya,kwa wengine sasa hivi ni ya zamani.

Basi hakikisha yule mmiliki wa mwanzo hana warant ya kudumu ya kuendelea kuiendesha gari hio kila anapojisikia.

Pia tambua kwamba gari ilishawahi kupata ajali,iliwahi kugongwa kwenye mazingira ambayo ilitaka kuwahi wakati barabara ina foleni na mataa hayaruhusu.

Kuna mahali ilikwama Kwa sababu ya kuishiwa mafuta,ikapewa msaada na mpaka leo haijasahau kufungua kioo na kusalimia kila ipitapo.

Kuna sehemu imepigwa sana faini kwa sababu ni nzuri kuliko gari ya Trafiki,aliyoiacha nyumbani kwake.

Kuna sehemu gari yako huwa inapigiwa miluzi kutokana na uzuri wake na wengine hudiliki kuisimamisha Ili tu wapate kujua vigezo na muundo wake kwa undani na kufanya makadirio kama wataweza kuinunua au kuikodi Kwa ajili ya kuiendesha.

Kuna sehemu gari yako mpya,mtaani wanaijua jinsi ilivyokuwa inapigishwa misele,rivasi kama maonesho.

Mwisho kama hautaki usumbufu jaribu kwanza kupima oil na kuiendesha ili ujue mapungufu na uzuri wake kabla hujainunua mazima.
 
_20240227_200958.JPG
 
Back
Top Bottom