Dr. Ulimboka live star tv: Afafanua Wizara ilivyosababisha Mgomo

Wenye access na TV angalieni Star TV Mwenye kiti wa kamati ya muda ya kuratibu mgomo wa madaktari anaongea star tv.
 
Wakuu sasa hivi dr Ulimboka anaongelea mgomo wa madaktari sababu zake na madhara yake, JAMANI FATILIENI MAZUNGUMZO HAYA.
 
Wana aininsha, ni kwa jinsi gani daktari anafanya kazi ktk mazingira magumu. Mgonjwa anakufa huku dakatari akiwa anajua kwamba kama dawa fulani ingekuwepo mgonjwa huyu asingekufa. Imeelezwa pia kwamba athari za kiafya na vifo vinavyotokea kila siku maospitalini ambavyo havikutakiwa kutokea ni kubwa mno kuliko hata athari zinazotokea kutokana na mgomo wa Drs.
 
anasema serikali ndio inapaswa kusimamia afya ya wananch wake kwa kuwapa madaktari vitendea kazi, na mishahara
 
Wenye access na TV angalieni Star TV Mwenye kiti wa kamati ya muda ya kuratibu mgomo wa madaktari anaongea star tv.
Siku hizi umeme ni ghali, kwa hivyo tunawasha Tv. kuangalia vipindi muhimu tu zikiwemo taarifa za habari. Hao wachochezi na wauwaji tumeiachia Serikali iwashughulikie.
 
Namfatilia kwa makini sana Dr Ulimboka yupo na mwanaharakati m1 hv machachari sana ana uchungu na nchi yule mwanaharakti
 
Jembe linaelezea jinsi mgogoro mzima ulivyoanza, kwamba mgogoro huu haukuanza kwa mgomo. Anaelezea jinsi viongozi walivyokuwa wanakataa kuonana na madaktari. Waziri aliombwa aje Donbosco kuonana na madaktari, akasema kama wanataka kuonana nae waende anatouglo. Anadhihirisha jinsi viongozi akiwemo waziri, walivyo engineer who mgomo. Kipi rahisi, madaktari woote waende anatouglo wakati wameshakusanyika DB kumfuata waziri au Waziri aende hapo DB?
 
anasema wao walikua wanania ya kukutana na waziri mkuu na yeye mwenyewe alimpelekea waziri mkuu barua nyumbani kwake kumwomba wakutane jumatatu badala ya jumapili kwani ombi la waziri mkuu la kukutana nao jumapili lililetwa jioni na madaktari mengi hawakupata taarifa.
 
Siku hizi umeme ni ghali, kwa hivyo tunawasha Tv. kuangalia vipindi muhimu tu zikiwemo taarifa za habari. Hao wachochezi na wauwaji tumeiachia Serikali iwashughulikie.

Siku ukiungua moto baada ya nyumba yako kuwaka moto na faya kuja kuzima wakati haina maji, wakabaki wakikuangalia ukiungua moto mpaka wananchi walipokunasua, na kukupeleka hospitali, ukafika hospital na kukuta madaktari wapo, na vifaa vya kukuhudumia kiufasaha hayo majeraha yako ili upone haraka havipo, na ukawa unajiona mwili wako ukiendelea kuoza, Ndipo utakapojua muuaji ni nani, serikali au daktari?
 
anasema wao walikua wanania ya kukutana na waziri mkuu na yeye mwenyewe alimpelekea waziri mkuu barua nyumbani kwake kumwomba wakutane jumatatu badala ya jumapili kwani ombi la waziri mkuu la kukutana nao jumapili lililetwa jioni na madaktari mengi hawakupata taarifa.
Na pinda alikuwa anajua kuwa maDOC hawakupata taarifa so hawtakuja ila kuonyesha kuwa hashirikishi akili akatumia gharama za ving'ora na mafuta kwenda kwenye mkutano..
 
Back
Top Bottom