Butola
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 2,290
- 756
huwezi kuamini kamaTanzania inaweza kuwa na mashujaa wa namna hii.hapa naanza kuelewa kwa nini ulimboka alitekwa na kupigwa kinyama.
Niambieni shujaa mwingine aliyewahi kutokea hapa Tanzania.mwili hauna nguvu lakini msimamo uko palepale!
...Ulimboka anaweza akawa Mpiganaji lakini katika hili kwa sababu anachopigania hakina sifa ya kumpa "ushujaa" kwa sababu amesimama upande wa "maslahi"tofauti na upande wa wananchi maskini wanaokufa sasa kwa kukosa matibabu waliokuwa wanayapata kwa sababu madaktari hawapo kazini....
....Kama angewakumbuka wananchi hawa japo kidogo basi angeungana nao hospitalini bila kupata huduma za Madaktari ili ayasikie machungu wanayoyapata,ila kwa kuwa hayupo tayari kuyaonja machungu hayo kwa sababu hayajali na anajali zaidi uahi wake,amsehindwa kuungana nao naye kukimbilia nje kwenye huduma nzuri zaidi,wananchi hawa maskini hawana pa kukimbia,huua ni Usaliti....
...Ndugu yangu,uhai haununuliwi,hawa wananchi maskini uhai wao hautarudi, machungu watakayoyapata ndugu zao wa karibu hayaelezeki,kushiriki kufanya hicho hakuweza kukufanya kuwa Shujaa bali kunakufanya kuwa Msaliti na Muuaji....