Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

Chal

Senior Member
Oct 7, 2010
128
52
Kwa maneno uake Dr ULIMBOKA ametoa kauli ya kishujaa na kutia shime na hamasa katika mapambano yanayoendelea ya kudai haki katika kuboresha huduma za afya na maslahi ya madaktari

"Naelekea nje ya nchi kwa matibabu, nawasihi madaktari wenzangu wanaobaki waendelee ma mapambano ya kudai haki ambayo kimsingi bado haijapatikana, nawaomba damu yangu iliyomwagika ikawe chachu na hamasa katika harakati hizi za kudai haki, asanteni sana"

Source: ITV HABARI
 
What about damu ya wagonjwa waliokufa kutokana na mgomo?

Ukiwa umepangiwa kufa UTAKUFA TU HATA MGOMO USIWEPO..... satisfied.... ur a failure....!!! 100% & even u failed to understand nani chanzo cha mgomo... ni serikali.... Hivi madaktari wadai vifaa na maslahi kidogo sana say around tshs 21 billions increment SASA AJABU HUJUI ETI SERIKALI IMETENGA TSHS 200 kuleta madr kutoka nje..!!!!!!!!!!!!!!!!?????????? ujue hii ndio upuuzi na ww unatetea
 
Hivi ingekuwaje kama madaktari wangeendelea kuwa kazini ila wagonjwa wanakufa kwa sababu hakuna madawa na vifaa pia hali mbaya za hospitali?
Wengi wanasema kuwa mgomo ndio umeua watu ila tukumbuke bila kugoma hapatakuwa na maendeleo kwenye hospital zetu.
Kama serikali ingekuwa inacare watu wake ingepeleka vifaa na madawa kwenye hospital,pili isingetegemea MNH ingekuwa na hospital kubwa nchi nzima ili kupunguza wingi wa wagonjwa.
 
Na wewe ulipwe kila unalostahili kwa kutoa uhai wa wagonjwa wa Tanzania walio wengi na kuwakosesha haki yao ya msingi ya kuishi na kuendelea kuteseka vitandani wasijue wapi pa kutibiwa.

Kama ungekuwa kweli unawatetea Watanzania usingekimbilia nje mbio mbio kwenda kutibiwa. Ungekaa hapahapa kuonesha ujasiri wako na uyahisi yanayowasibu Watanzania kwa kuhamasisha mgomo kwa manufaa yako na wajivuni wengine wachache wanaojiona wao ni miungu watu.
 
What about damu ya wagonjwa waliokufa kutokana na mgomo?
Madokta wana watoto na mahitaji mengine kama hao mabwana zako Magamba, wanaitaji pesa na kusomesha watoto zao na kuudumia family zao.Wabunge ambao wanalala tu Bungeni na wengine wanaonga vitoto kama Lulu kila mwaka wanajiogezea marupurupu mbona uwaulizi? Wabunge ambao kila bajeti wana pandisha mshaara na kodi at the same time yaani wanafanya madudu tu mbona uwaulizi? Kama kufa utakufa tu
 
Uungwana unaanzia kwako,madaktari damu yao iwe ya ukombozi,yetu iwe ya kusahulika!kunya anye kuku,akinya bata kaharisha,hata raia ni watu
 
Na wewe ulipwe kila unalostahili kwa kutoa uhai wa wagonjwa wa Tanzania walio wengi na kuwakosesha haki yao ya msingi ya kuishi na kuendelea kuteseka vitandani wasijue wapi pa kutibiwa.

Kama ungekuwa kweli unawatetea Watanzania usingekimbilia nje mbio mbio kwenda kutibiwa. Ungekaa hapahapa kuonesha ujasiri wako na uyahisi yanayowasibu Watanzania kwa kuhamasisha mgomo kwa manufaa yako na wajivuni wengine wachache wanaojiona wao ni miungu watu.

kama vifaa vingekuwa pale MNH usingeona ameenda S.Africa
 
Pamoja na mapungufu ya kibinadamu ila dokta ulimboka anahitaji maombi ya wapenda maendeleo wote mbona viongozi wa serikali wanaingia mikataba mibovu inayogharimu maisha yetu sote lakini tupo kimya kwa nini mbunge awekewe mazingira mazuri halafu dokta anayetibu watu asahaulike?
 
You will definately eat coke this time,
Utakunywa boflo kumezea
Na wewe ulipwe kila unalostahili kwa kutoa uhai wa wagonjwa wa Tanzania walio wengi na kuwakosesha haki yao ya msingi ya kuishi na kuendelea kuteseka vitandani wasijue wapi pa kutibiwa.

Kama ungekuwa kweli unawatetea Watanzania usingekimbilia nje mbio mbio kwenda kutibiwa. Ungekaa hapahapa kuonesha ujasiri wako na uyahisi yanayowasibu Watanzania kwa kuhamasisha mgomo kwa manufaa yako na wajivuni wengine wachache wanaojiona wao ni miungu watu.
 
huwezi kuamini kamaTanzania inaweza kuwa na mashujaa wa namna hii.hapa naanza kuelewa kwa nini ulimboka alitekwa na kupigwa kinyama.
Niambieni shujaa mwingine aliyewahi kutokea hapa Tanzania.mwili hauna nguvu lakini msimamo uko palepale!

Meno,kucha kuondolewa unadhani utani? Dr Ulimboka iz great nadhani hakuna kiongozi wa tz amewahi pitia hayo mambo toka tz ianze
 
Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom